Tuesday, September 9, 2008

Foxy brown atinga jukwaani akiwa mjamzito

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Foxy Brown kwa sasa ni mjamzito. Habari kutoka mitandao mbalimbali nchini humo, zinasema kuwa mwanamuziki huyo ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki mwenzake wa Hip Hop, Rick Ross inawezekana akawa mhusika wa ujauzito huo.
Hivi karibuni, Foxy alitinga katika tamasha la utoaji tuzo za MTV katika jiji la New York akiwa na ujauzito wake. Msanii huyo ambaye kipindi cha nyuma alitamba na nyimbo zake kali, alikaa kimya na kuwafanya mashabiki wake ambao hawakumuona kwa muda mrefu katika onesho lolote kuhisi aliishiwa kisanii lakini aliwashangaza pale alipopanda jukwaani katika tuzo hizo na kufanya vitu vyake .

No comments: