Tuesday, September 9, 2008

Fabulous ajiachia mitaani na mwanae

Ebwana hii itakuwa kali zaidi kwani hivi karibuni msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Fabolous hivi karibuni amebambwa na mapaparazi akiwa na mzazi mwenzake ambaye ni raia wa kilatin kimya kimya. Tukio lilitokea hivi karibuni huko New York nchini Marekani, ambapo mwanamuziki huyo akiwa na mwanadada huyo aliyezaa nae bila yeye kujijua.


Fabolous ameonekana kufurahishwa kuzaa na mlatino huyo ambapo kila mara msanii huyo amekuwa karibu na mwanae kitu ambacho kwake anakiona ni furaha kubwa. Lakini wadaku wanasema kuwa msanii huyo alikuwa hapendi watu wajui kama ana mtoto kutokana na kumficha ili mapaparazi wasijue.

Hata hivyo imeshindikana kumficha mtotot huyo kutokana na mashabiki wake kujua kinachoendelea na mwanadada huyo ila watu wanajiuliza msanii huyo aliyekuwa hapendi watu wajue ana mahusiano na mtu yeyote kwani alikuwa ni mzee wa totoz.

No comments: