Wednesday, August 13, 2008

AFYA YA JAMII

UAMBUKIZO TUMBONI (ARO ENERITIS)


Uambukizo tumboni ni tatizo linalotokea katika tumbo la chakua. (Acute information of the lining of the stomach and intestine) uambukizo huu husambaa kuanzia katika tumbo la chakula hadi katika utumbo mwembamba na mkubwa.

Uambukizo huu huwa mkali (Acue gastroenteritis) inaweza kusababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi (Excusive indulgence in alcohol), uambukizo wa (virus, bacteria ingredients of food and dinks), mzio unaweza kusababishwa na vyakula na vinywaji. Pia zipo baadhi ya dawa zinazoweza kusababisha mzio pia yapo magonjwa mbalimbali yanayosababisha tatizo hili la uambukizo tumboni kama vile ugonjwa wa maumbo (typhoid fever), ugonjwa wa kuharisha damu, kipindupindu, kuungua mwili mzima na moto (Extensive burn).



DALILI ZA TATIZO


Dalili za tatizo hili huanza ghafla, mgonjwa huwa mchovu, hukoa hamu ya kula, hupatwa na kichefuchefu mara kwa mara, hutapika, tumbo huuma sana (Abdominal amps) ambapo misuli ya tumbo hukaza, uharisha, na mwili hulegea, uhisi moto au joto katika tundu ya haja kubwa (Retail burning and tenesmus), wakati mwingine hutokwa na majimaji yenye utelezi na damu katika njia ya haja kubwa. Mgonjwa hupata homa mgojwa akitapika na kuharisha sana hupoteza maji mwilini na kusababisa apoteze fahamu. Mgojwa huumwa kichwa, misuli hukaza na kuhisi ganzi mwili mzima.Tumbo huvimba na kujaa na akibonyezwa uhisi maumivu makali hasa chini ya kitovu.


UCHUNGUZI

Uchunguzi utategemea historia ya ugonjwa kama kuna kitu ulikula mfano pombe, maziwa, samaki, nyama au chakula chochote ambacho kilikutibua tumbo. Vipimo mbalimbali kama vipimo vya damu, haja kubwa na vipimo vingine ambavyo daktari ataona vinafaa. Mgonjwa atachunguzwa tumboni kuona athari zilizopo kwa kufanyiwa vipimo kama Ultrasound na sigmoidoscopy. Ugonjwa huu huathiri kuta za utumbo na hufanana na maradhi mengine kama ulcerative colitis na Amoebic dysentery.Ugonjwa huu pia hufanana na ugonjwa wa kidole tumbo na saratani ya utumbo (colonic malignancy)


MATIBABU

Mgonjwa apumzishwe, atapimwa vipimo mbalimbali kama vya damu, haja kubwa, shinikizo la damu, na mgonjwa ataongezewa maji. Atapatiwa tiba kufuatana na jinsi tatizo linavyojitokeza. Mgojwa atapewa dawa za kutuliza maumivu, kuzuia kuharisha na kutapika.


USHAURI

Ni vema uwahi hospitali kubwa kwa uchunguzi na tiba, kama tulivyoona, uchunguzi ni muhimu ili kujua chanzo cha tatizo na kukabiliana nacho. Epuka vyanzo vya tatizo zingatia tiba na kula chakula bora. Kunywa maji safi na salama. Kula chakua bora.

No comments: