Tuesday, September 9, 2008

Ay na P-square ndani ya studio za Hammy B

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yessaya ‘AY’ ameshakamilisha wimbo wake aliokuwa anataka kufanya na kundi la P-Square ambao hakutaka kuutaja, anashuka nayo Catherine Kassally.

Akichonga na Showbiz jijini Dar es Salaam, msanii huyo amesema kuwa wimbo huo umeshakamilika na ameufanya ndani ya studio za Hammy B za jijini Dar esa Salaam. AY amesema kuwa wimbo huo umeshakamilika na sasa yuko katika maandalizi ya kufanya video yake na kuongeza kuwa hivi karibuni anatarajia kwenda Lagos, Nigeria ambako ni makazi ya wasanii hao wanaounda kundi la P-Square linaloundwa na ndugu wawili ambao ni Paul na Peter.

Amesema kuwa wimbo huo hataki kuutaja jina kwa sasa kutokana na baadhi ya wasanii kuwa na tabia ya kudai nyimbo zilizotungwa na wenzao ni zao au mawazo yao.
“Unajua dunia imeharibika hasa kwa baadhi ya wasanii wanapoona mwenzao ametoa wimbo basi wanasema ni wao ndiyo maana sitautaja jina kwa sasa mpaka nitakapomalizia video yake na kuuachia katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni ndiyo nitautaja jina lake,” alisema.

AY amesema mbali na kufanya wimbo huo yuko katika maandalizi ya albamu yake mpya ambayo ndani ya yake amewashirikisha wasanii mbalimbali wa hapa nyumbani na Kenya, Uganda na Afrika Kusini na amewataja kuwa ni pamoja na Chameleone, Nameless na Redson.

No comments: