Tuesday, July 22, 2008

WAZANZIBAR AMKENI!

Hii inaonesha wazi kuwa nchi hizi mbili ziliungana kwa upendo na makubaliyano kati ya hayati Mw. Julius Kambarage Nyerere na hayati Bw. Abeid Amani Karume .Muungano huo kwa sasa umekuwa gumzo kwa Wazanzibar, kwani kimtazamo na masilahi ya Wazanzibar hauna ila ni kuwakandamiza tu,wako watu ambao wanajiita wanzanzibar lakini niwasaliti tu hawaitakii mema bali wanahitaji masilahi yao binafsi tu, na kuna wengine kwa upeo mfupi wao wanafuata mkumbo na kudiriki kusema mimi nataka ipepee tu, watu kama hawa niwakuogopwe kwani ndio wanayoipeleka Nchi pabaya. kwa sasa uchumu wa Zanzibar sio nzuri, maisha ni magumu katika kila nyenja mbalimbali za kiuchumi na zakijamia. Kwa sasa Muungano umebadilika Watanzania wao ndio wenye see wa kila kitu, hii inaonyesha wazi kuwa iko haja ya kuangalia vizuri masihi ya Wazanzibar na kuangalia upya Muungano huu kwa mtazamo mwengine, ili ulete haki sawa kwa Wazanzibar na Watanzania . Hii inaonyesha wazi kutoheshimu makubaliano ya Nchi hizi mbili. Jee hii leo sio Nchi na kama sio Nchi, huu Muungano uliunganishwa na Wilaya au Mkoa....
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere akichanganya mchanga wa Tanganyika na Zanzibara kuashiria muungano wa nchi mbili hizo na kuwa Tanzania Aprili 26, 1964, (Kulia) ni Makamu wa Pili wa Rais, Rashidi Kawawa na kushoto ni Makamu wa Kwanza na Rais wa Zanzibar, Abeid Karume .

No comments: