Friday, July 25, 2008

WAREMBO MISS TZ WALIVYOJIACHIA JIJINI

Leo warembo wote 27 wanaotarajia kushiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Vodacom Tanzania 2008 walipewa ruhusa ya kutembelea ndugu jamaa marafiki na kufanya matanuzi katika maduka mbalimbali.Pichani Baadhi ya warembo wakiteremka kutoka katika Bus lililowaleta jijini Dar es salaam wakitokea Bagamoyo ambako wameweka kambi katika hotel ya Paradise.

Warembo Johari Abubakar, Beatrice Bengenesa na Florence Josephat wakiwa nje ya ofisi za kamati ya Miss Tanzania, wakisubiri bus lao ili kuwarudisha kambini kwao Bagamoyo baada ya kumaliza Matanuzi mjini.

Mwalimu wa warembo hao Richa Adhia akinawa maji baada ya kupata msosi katika mgahawa mmoja uliopo maeneo ya Posta jijini Dar es salaam.

No comments: