Monday, July 28, 2008

NEVER SAY GOODBYE

Wiki iliyopita tulianza kuwatolea Tamthilia ya kusisimua ya Never say goodbye, tuliona jinsi mwanamke mmoja anavyoweza kubadirika na kuwa na sura tatu tofauti, hii yote ni kwasababu ya kutafuta maisha na kulipiza kisasi kwa wale wabaya wake, Je Maki atafanikiwa kuwapata wabaya wake kwa njia hiyo? Endelea kuungana na mwandishi akupatie uhondo.

Polisi wanamfukuza Juan Francisco ambaye anafanikiwa kuwakimbia. Fanny anapoulizwa anasema kuwa hajui ni wapi Juan Francisco amekwenda.Polisi wanaamua kusachi nyumba ili kupata uhakika kama kweli hayupo au amejificha. Florcita anakwenda shule,akiwa na hamu ya kupata clown. Maki ana huzuni kwasababu ameolewa na Ricardo ambaye anataka kuwa naye mpaka mwisho wa maisha yake. Akiwa katika mawazo wanapokea simu kuwa Juan Francisco amepotea. Maki ana wasiwasi na mtoto wake anaondoka kwenda kumuona.

Juan Francisco yuko El Sauce anamuomba Juan Cayo ambaidie kutafuta ukweli juu ya kifo cha Maki. Juan Cayo hamwamini lakini mwisho anakubari kumsaidia. Wanakwenda kumuona Urrutia. Urrutia hamfahamu Juan Francisco ambaye anawaambia kuwa kuna mtu anaitwa Juan Francisco alimlipa ili ampeleke Maki jela.Baada ya kusikia habari hiyo wanaanza kufatilia.

Ramón anakwenda nyumbani kwa akina Fanny na Esther na kuwaambia kuwa Juan Francisco amemuomba awaambie kuwa yeye hana matatizo. Ernesto, ambaye ni mpelelezi anaenda nyumbani pale na kukaa kwa muda na kuwauliza kama wanahabari yoyote kuhusiana na Juan Francisco na kuwaonya iwapo watasikia lolote kuhusiana Juan Francisco wamwambie hasa kama atawapigia la sivyo watapelekwa jela na kuingia matatizoni .

Mshauri wa Juan Francisco anajaribu kumtetea kwa gharama yoyote,lakini Ramón anagundua kwamba kuna kitu kigeni kinachowaunganisha mshauri wa Juan Fransisco na mpelelezi. Wanaondoka Ramón anachukua uamuzi wa kumkimbiza mshauri. Mshauri huyo akaingia sehemu ambayo Ernesto anakwenda pia. Ramón anahisi kuna kitu kibaya kinaendelea.

Ernesto anaongea na mshauri wanatokea kurumbana, mpaka wanaposema kuwa wao ni kundi moja na kwamba Ernesto anahisi kuwa anasalitiwa.wanajaribu kumaliza tofauti zao. Maki anavaa maski yake ili kumuangalia mtoto wake, anafanikiwa kuongea naye kwa muda. Maki anamwambia mchungaji Higinio kwamba Juan Francisco ametoroka hivyo ana wasiwasi na binti yake.

Mcungaji Higinio pia ana wasiwasi na Maki kwasababu ana wasiwasi kuwa ameolewa na mwanaume ambaye hampendi ‘Ricardo’. Mchungaji Higinio anamwambia Maki kwamba hatokuwa na furaha na Maki anamwambia kuwa kikubwa anachokiwaza ni mtoto wake. Juan Cayo anapiga simu kwa mchungaji Higinio kumwambia kuwa Juan Francisco yuko Sauce. Ricardo anampigia simu Saúl kumwambia kuhusiana na rafiki yake Maki. Ricardo ana hasira kwasababu wako kwenyefungate, Maki ameondoka kwenda kumuona Juan Francisco. Kila mmoja ana wasi wasi na Juan Francisco, kwasababu amekimbia bila ya kumtaarifu mtu yeyote ni wapi alipo.

Ricardo anamuomba Saúl aongee katika nafasi yake. Esther anamshawishi Alex kwenda nyumbani kwake. Alex anakataa lakini mwisho anakumbari maombi yake. Juan Cayo anamwambia Maki kwamba Juan Francisco yuko Sauce. Maki anashangaa na kumuuliza ni kitu gani amemwambia. Juan Cayo anamwambia kuwa amemwambia habari aliyomwambia, kwamba yeye si mtu mbaya na kwamba anampenda, na kwamba anatafuta watu walioangamiza maisha yake. Maki anamuomba Juan Cayo amsaidie Juan Francisco. Saúl anakwenda kumuona Ricardo.

Ricardo anamwambia Saúl kwamba anajua kuwa yeye na Esther wanahusika katika kifo cha Maki. Ricardo anasisitiza kwamba anajua kuwa yeye ndio alitoa amri ya kumsababishia Maki aingie katika dawa za kulevya na kwamba sasa amejaribu kumuua Soraya. Saúl akajibu kuwa hausiki na kitu hicho, kitendo kilichosababisha Ricardo aseme kuwa ana ushahidi unaooneshea kuwa ni yeye. Saúl anasema kuwa alikuwa ni Juan Francisco Moreno na Ricardo akamwambia kuwa kile anachosema ndio anataka kiwe na anataka kila mmoja apandikizwe maneno hayo.

Ricardo anasema kwamba Juan Francisco yuko Sauce, akitafuta ukweli na njia nzuri ni kuhakikisha wanamuua.Polisi wanaingia kwa Juan Cayo kumtafuta Juan Francisco lakini Juan Francisco anakuwa amejificha. Ricardo anamsubiri Maki chumbani, anamwambia kwamba hawezi kumsamehe kwa kumuepuka tena.

Maki anakuwa hana uchaguzi tena zaidi ya kukubariana na matakwa yake. Esther anamuona Fanny, akiwa na wasiwasi baada ya kutomuona Alex nyumbani kila siku. Fanny anamuuliza Esther kama tayari anamaelezo juu ya mjukuu. Juan Cayo anakwenda kumuona Meche, hivyo Juan Francisco anaweza kuongea na yeye. Meche anakataa kuongea. Ramón anamwambia Isabel kwamba kuna kitu Fulani zaidi ya urafiki kati ya Aurelio na Carvajal. Saúl na Marina wanapanga mpango wa kumuua Juan Francisco. Marina anamwambia Saúl kwamba maisha yao yako hatarini, Aidha kati ya Juan Francisco na Ricardo,wanaamua kwenda kwa Juan Francisco huko Sauce.

Juan Francisco anakiri wazi kwa Juan Cayo wasiwasi wake wa kutotafuta ukweli juu ya kile kilichokuwa kimemtokea Maki katika maisha yake ya nyuma na kuona kwamba Meche amekataa kumsaidia, Juan Cayo anajaribu kumpa moyo. Maki, akiwa katika harakati za kumkataza Ricardo kumbusu, anaona simu ikiita. Ricardo anaongea na Aurelio na kuamuru atafutwe Juan Francisco ili amsambaratishe moja kwa moja.

Juan Francisco anampigia simu Fanny lakini anakuwa na hamu ya kuongea na Florcita na Fanny anakuwa na hasira kwasababu amekataa kuongea nay eye na ameacha ujumbe kwa mtoto wake tu Ramon anamwambia Isabel kabla hajamfata Aurelio siku inayofuata mchana, anagundua kwamba amepanga nyumba karibu na Ernesto Carvajal kwa mawazo kwamba atampeleka mwanamke pale.

Ernesto anampigia Antonio ofisini kwake kumtaarifu kwamba wamepata uhakika kwamba Juan Francisco yuko Sauce na anataka amkamate. Juan Cayo anamuona Juan Francisco akiongea na picha ya Maki huku akielezea penzi lake kwake , hivyo anaamua kumlazimisha Meche amwambie Juan Francisco kila kitu anachokifahamu. Alex anaamua kuama nyumbani kwa Esther ili kumpa nafasi ya kuficha kile alichokiona Florcita pale walipokuwa wakibusiana kisha mambo yakisha kuwa mazuri atarudi, hata hivyo mwanamke huyo hakukubariana na uamuzi wa Alex. Angie, kwa uzuni anawaambia wazazi wake amepoteza matumaini ya kuwa na mgahawa kwasababu mmiliki wa nafasi ile ameghairi kupangisha anachotaka ni kuuza.

Mchungaji Higinio anamtembelea Maki na kumrudishia boksi lake ambalo alimuachia baada ya kuachiwa na baba yake. Isabel anagombana na Aurelio kutokana na habari alizopewa na Ramon na kuamua kumchukua mbele ya Ernesto ili kurahisisha kila kitu. Ricardo anampigia simu Saul akimuamuru aende Sauce na kumuangalia Juan Francisco kisha amuue ili kuondokana na matatizo. Maki, akiwa na barua ya baba yake mkononi, analia kwa kupotea kwake. Alex anamtembelea Angie akijaribu kutuliza akili yake na pale alipogundua mambo yote yaliyotokea kuhusiana na mghahawa, akaahidi kujiunga na Leopoldo ili kuwasaidia.

Meche anaamua kumwambia ukweli Juan Francisco ambaye anazidi kumuelezea kuwa Saul Robles ndiye aliyepanga mpango wa kumuwekea Maki dawa za kulevya nyumbani kwake. Saul anachanganyikiwa kwa Marina pale alipogundua kwamba akubariani na kifo cha Juan Francisco akidhani huenda ana wivu naye. Juan Cayo anamalizia kwa kumwambia ukweli Juan Francisco kuwa Maki yuko hai Juan Cayo anarudia baada ya kumwambia Juan Francisco kwamba Maki yuko hai kisha anabadiri maongezi. Maki anaamka na kukuta ujumbe kutoka kwa Ricardo, akimwambia akae tayari kwasababu wanatoka pamoja.

Ricardo anachanganyikiwa kwani kila akimwamngalia Maki anahisi ndie marehemu mke wake na kutaka kila kitu kifanyike kama vile hakuna kilichotokea . Maki anafanya kile Ricardo alichotaka afanye, lakini anashangazwa na kile anachofanya. Juan Francisco na Juan Cayo wanakenda kumuona Urrutia bila ya kujua mwanaume mwenye bastola anawafatilia. Ricardo anampatia Maki suti nyeusi na begi kisha anamwambia waende wote sehemu maalum.

Leopoldo anapata uzuni pale alipogundua kuwa Lucila ana wasiwasi na mtoto wake,anajaribu kumchangamsha. Juan Francisco na Juan Cayo wanakimbia kwenye majani. Mwanaume mwenye bastola anawakimbiza. Maki anamkatalia Ricardo kwa mara nyingine na kutoa sababu kuwa ana wasiwasi na Florcita. Mwanaume mwenye bunduki anamshuti Juan Francisco na Juan Cayo anachanganyikiwa baada ya kuona Juan Francisco amezimia. Juan Cayo anataka kumpeleka mjini lakini Juan Francisco anamwambia ampeleke mtoni ili ajifiche mapolisi.

Angie na Leopoldo wanajaribu kumshusha Lucila. Ricardo anampeleka Maki sehemu ngeni kabisa ambako alimwambia apigwe picha za mapozi. Fanny anawacheka Alex na Esther, wanajaribu kumtharau. Mwisho Alex anaondoka na Esther anabaki akiumbana na binti yake, akisema kuwa yeye hajawahi kumchezea Juan Francisco kama yeye alivyomfanyia . Esther anajaribu kumuomba msamaha Fanny kabla ya Alex lakini wanakuwa na marumbano kwasababu ya ukaribu alionao na familia ya Moreno.

Marina ana uhakika kuwa Juan Francisco amefariki hivyo anamwambia Saúl, hivyo anamuacha Ricardo afahamu, Saúl anafikilia jinsi ya kumfanya Fanny ajue. Juan Cayo anampeleka Juan Francisco kijijini anakofanyia kazi Pedro kama nesi, na anajaribu kumuweka Juan Francisco apumzike kwasababu ya hali yake kuwa siriasi. Ricardo anaambiwa habari na kufurahia kifo cha Juan Francisco. Maki haelewi ni kwanini mwanaume huyo ana furaha.

Pedro anamuangalia Juan Francisco na kuamini kuwa hali yake ni mbaya, anamwambia Juan Cayo ampeleke mjini. Juan Cayo anamwambia Pedro kwamba polisi wanamtafuta Juan Francisco,anamuomba kufannya linalowezekana ili kumsaidia Juan Francisco wakati anaenda kutafuta dawa mjini. Isabel na Fanny wanaongelea matatizo yao. Marina anataka kumsindikiza Saúl kumwambia Fanny kwamba Juan Francisco amefariki. Juan Cayo anamwambia mchungaji Higinio kwamba kuna mtu alikuwa akijaribu kumuua Juan Francisco.

Maki anakwenda kumuona mchungaji Higinio ambaye anamwambia habari za Juan Fransisco, Maki anatoroka na kuamua kwenda mjini kuwaona majeruhi. Ricardo anamwambia Aurelio kwamba Juan Francisco amefariki na kumuomba afatilie kama ni kweli.

Aurelio anapiga simu kwa Ernesto, ambaye anamwambia kwamba hakuna mwili wa marehemu yeyote hivyo hakuna ukweli juu ya kifo. Ernesto anaenda kumwambia Fanny ambaye anazimia. Ricardo anagundua hakuna ukweli na kumsukuma Saúl kufatilia kama Juan Francisco yuko hai. Maki anamuangalia Juan Francisco na kupata mshangao pale alipomuita Maki.

EPISODE S–065

Juan Francisco kwa hasira anamuita Maki. Maki anajaribu kumtuliza. Pedro anajaribu kushusha homa ya Juan Francisco. Esther ana wasiwasi na Fanny, anataka kumpeleka zahanati.Mtu aliyekuwa anamuangalia anasema kuwa Fanny ni mjamzito. Lucila anaamua kupiga simu kwa Esther kujua kuhusiana na Juan Francisco. Esther anamwambia Lucila kile wanachokijua kuhusiana na mtoto wake, Leopoldo anajaribu kumtuliza mke wake.

Florcita anahisi mpweke na kwenda katika kampuni ya Alex. Alex anamfundisha jinsi ya kupiga gitaa. Fanny na Esther wanaenda kwa Moreno ambaye anawaambia kwamba Fanny anatarajia mtoto. Wanakaa kimywa kwani hawajui nini kilichompata baba wa mtoto. Ricardo ana wasiwasi kwasababu Maki amepotea, anajiapiza kwamba atamuua Juan Francisco. Juan Francisco anamwambia Maki mambo mengi hakuyajua. Maki anajaribu kumtuliza. Ricardo anakwenda kanisani n akujiapiza kwamba atalipiza kisasi kwa mchungaji Higinio. Isabel anajaribu kumshawishi Fanny hivyo anakwenda nyumbani lakini Fanny anaogopa.

Marina anafika pale nyumbani hauwezi kuamini kama Marina ni mtu mbaya pale anapoongea kuhusiana na Juan Francisco. Maki anaamua kukaa mjini usiku kucha na Juan Francisco. Mcungaji Higinio anaamua kurudi Lima. Wanaahidiana kuzidi kuwasiriana pale atakaporudi Lima. Tere anamuomba Alex ampatie shoo ya faragha na Florcita, ambaye anawasiwasi na hawezi kulala. Saúl na Esther wanaongea ukweli kila mmoja. Maki anakaa akimuangalia Juan Francisco wakati Juan Cayo amepumzika.

Ricardo ana hasira kwani hawezi kulala. Esther anajihisi mwenye furaha pale anagundua kuwa Alex anamuangalia mjukuu wao. Maki anawaaga Juan Francisco na Juan Cayo,anarudi Lima, baada ya kumpatia pesa Juan Cayo kumwangalia mwanaume wake. Alex na Angie wanakutana sehemu sehemu Fulani na kubusiana. Polisi wanaingia mjini Juan Cayo anakosa la kufanya ili kumuokoa Juan Francisco. Pedro anasema kuwa hawezi kumuondoa kwasababu hali yake ni mbaya,laa sivyo atakufa. Maki anarudi jijini na kumuaga mchungaji Higinio, kisha anakwenda kwake kukutana na Ricardo. Juan Cayo anajaribu kumuamsha Juan Francisco, hivyo anamsaidia kumuokoa kwa mapolisi.

Maki anatakiwa kumuona Ricardo hajui la kumwambia mwisho anamwambia kwamba alitakiwa kumsindikiza mchungaji Higinio kwasababu alikuwa na mgonjwa anaumwa sana, Pedro uso kwa uso na polisi,anadai kwamda ametoroshwa. Polisi wanaamini habari yake.wanaondoka pale Juan Cayo na Juan Francisco walipojificha chini ya kitanda

EPISODE S-066

Pamoja na malalamiko ya Aurelio, Ernesto anamwambia anasubiri kumuona Juan Francisco ajue kama yuko hai au amekufa. Esther mwisho kabisa anaukubari ukweli kwamba penzi kati yake na Alex haliwezekani na kwamba halina muda mrefu litavunjika. Pedro anafanya kila njia kumuamisha Juan Francisco sehemu ile akijaribu kumuokoa kwa mapolisi.


Ricardo anamlazimisha Saul kumtafuta Juan Francisco na kujua kama yuko hai au amekufa, Marina anaamua kwenda nyumbani kwa Maki kutafuta ukweli. Angie wanaamua kuwa karibu kama ‘mapatna’ lakini Angie anajua kuwa kijana amezimika sana kwake.Juan Cayo anamuendesha Juan Francisco kwenda mjini akijaribu kumuokoa.


Ricardo anakasirishwa na kila kitu kilichotokea, anahisi kila kitu kimelala, na pale alipotokea Marina akamfokea na kumfukuzia nje, lakini akamtuliza kwa kumwambia kuwa anajua kila kitu kinachoendelea kuhusiana na Juan Francisco hiyo ndio sababu iliyomleta pale ndani ili ajaribu kumpeleleza Maki.


Rogelio anawaendesha Juan Cayo na Juan Francisco kuwaokoa pale walipokuwa wakienda kumsubiri rafiki wa mchungaji Higinio,ambaye ni daktari kwa ajiri ya kumuona Juan Francisco.Juan Francisco anaongea na Fanny lakini ni katika kumjulia hali Florcita na hakuwa na muda wa kuongelea swala lingine. Ernesto anamuonya Antonio kwamba Juan Francisco yuko hai, inavyoonekana walisikiliza simu ya Fanny. Marina anafanikiwa kupata ukweli kwa Maki na kugundua kuwa Juan Francisco yuko hai na kwamba Maki anajua mambo mengi lakini hakutaka kumwambia.


Daktari ana wasiwasi na Afya ya Juan Francisco risasi zimemuathili vibaya na maisha yake yako hatarini, hivyo anamwambia mtoto wake kusafisha vizuri wakati anajaribu kumpatia dawa. Fanny anamwambia Isabel kuhusiana na maongezi yake na Juan Francisco wote kwa pamoja wanahuzunikia maisha yao ya mapenzi. Ramon anashtuka pale anapogundua kupitia kwa rafiki yake Gino kwamba Aurelio ni shoga na inaonekana yeye na Ernesto ni wapenzi.


Akiwa njiani kuelekea nyumbani, Marina anamuona changudoa ambaye mwisho anagundua kuwa ni Niangua, mwanamke ambaye ni mama yake ambaye aliwatupa yeye na kaka yake siku moja huko Sauce. Ricardo bado anaendelea kujifanya mtu mwema mbele ya Maki, anampatia pesa nyingi na kutuma midoli kwa mtoto. Ramon anaongea na Isabel, lakini hakuweza kugundua ukweli wa Aurelio, alichomwambia ni kutomuamini.


Maki, anavaa maski kama boga na kwenda kucheza na binti yake ambaye anampelekea zawadi alizopewa na Ricardo. Saul anamlazimisha Marina kumwambia ukweli kuhusiana na Juan Francisco pamoja na kutompa kampani pale alipojaribu kumuomba msaada. Esther anakwenda nyumbani kwa Saul akiwa na nia ya kurekebisha mambo fualani.

EPISODE S:–067

Esther anamwambia Saúl kwamba anakubariana na mambo mabaya yaliyoko gizani kwani anaujua ukweli wa mtu aliyetoa amri ya kwamba Juan Francisco akauawe.

Alex anagundua kwamba siku zote amekuwa akimfikiria Angie. Angie anamwambia rafiki yake kuwa yeye na Alex wamebusina. Marina ana hasira kwasababu mama yake hakumtambua. Maki Maki amevaa maski anaongea na Flor, ambaye anamwambia kuwa anakaribia kupata kaka.

Anastasia, muuguzi anayemsaidia, Juan Francisco, anachangamshwa na mgonjwa wake,ambaye anamwambia kuwa atapata upendo katika maisha yake. Saúl anatangaza kwamba hausiki na mauji ya Juan Francisco lakini Esther hamwamini. Marina anakwenda kwa Esther na kumwambia kwamba Saúl anampenda Fanny na kutokana na sababu hiyo aliagiza Juan Francisco auawe. Fanny anamwambia Lucila kwamba ameongea na Juan Francisco na kwamba anaumia. Saúl anafukuza Marina nyumbani kwake.


Alex anamuomba Esther watoke lakini anamkatalia. Alex anakuwa na wasiwasi kwasababu hajawahi kumdharau kabla. Saúl anambeza Marina kwasababu kwasababu alimwambia Esther kwamba anampenda Fanny. Juan Cayo anamtembelea Juan Francisco, ambaye alimwambia kuwa amemuona Maki au Soraya pale lipokuwa mahututi.


Esther anatamani kumuuliza Fanny kama aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Saúl. Fanny anakataa lakini Esther anagundua kuwa anadanganya. Flor anamwambia Maki kuhusiana na kaka yake anayetarajia kumpata. Maki anajihisi hana raha bada ya kuambiwa habari hiyo. Saúl anakosa amani na kuona kama mambo yake yamekwama baada ya Esther kujua mpango alionao na Fanny. Maki anasali na kulia kanisani.


Father Higinio anaingia na kumkuta akilia kisha anamwambia kuwa Fanny ni mjamzito. Father Higinio anamuonya na kumwambia kuwa Ricardo amekwenda kumtafuta. Alex anajaribu kumchangamsha Esther hivyo anakwenda naye kwenye conceti. Huko anapandisha hasira na Alex anashindwa kuvumia naye anakuwa na hasira na kuamua kuondoka. Marina analia pale anapomuona mama yake yuko miongoni mwa mafedhuri.


Ricardo anamuuliza mchungaji Higinio kuhusiana na hali ya mpwa wake, mchungaji Higinio anashtuka na kumjibu kuwa yeye hana mpwa. Maki anamuoneshea ishara mchungaji na kuwamwambia kuwa anamaanisha Juan Francisco.Kisha mchungaji Higinio anatunga habari kuhusiana na ukaribu na urafiki aliokuwa nao na Juan ndio maana alimuona kama mpwa wake.
Juan Francisco anamchangamsha Anastasia hivyo anajikuta amepata muamko kuhusiana na maisha ya mapenzi. Ramón anapata huzuni pale anapomkumbuka Isabel.

Isabel anaumia kwani hawezi kuacha kumuwaza Ramón. Esther anampigia simu Alex kwenye simu ya mkononi lakini anashindwa kumpata. Esther anamwambia katibu muktasi wake awasiliane na Angie, lakini anaambiwa kuwa Angie hayuko ndani. Mchungaji Higinio anamhabarisha Maki hali ya Juan Francisco kwa kutumia simu. Ricardo anajaribu kuingia ndani lakini mlango unakuwa umefungwa, Maki anamfungulia kisha Ricardo anamuonesha gauni anayotaka avae usiku wa siku hiyo. Fanny anamfokea Saúl kwasbabu amemwambia Esther kwamba waliwahi kuwa faragha. Saúl anasisitiza kwamba anampenda.

Fanny anamwambia kwamba amechanganywa nay eye baada ya kuwa na uhusiano naye. Juan Francisco anamtakia kila la Kheri Anastasia kwasababu amemuhudumia vizuri na doctor Herrera amemhakikishia kuwa sasa afya yake ni njema. Juan Francisco anamomba Anastasia akatembee,anampeleka na baiskeli. Saúl na Fanny wanakuwa ndani ya marumbano makali ambayo yanaingiliwa na Marina. Saúl anamfukuza Marina aondoke eneo lile kwasababu kilichotokea ni kwaajiri yake. Fanny anaumia pale alipogundua kuwa Saúl alimwambia Marina kuhusiana na uhusiano wao walipokuwa vijana. Marina anamkaribisha Fanny kupata kinywaji. Fanny anamwambia kuwa hawezi kunywa kwani wana mimba. Marina anawaambia kwamba yeye si mjamzito.wakati huo huo mwanaume mwenye siraha anamsubiria Juan Francisco kumuua kwani amejificha shambani.

EPISODE S–068

Saúl anawasiriana na mwanaume mwenye siraha kwa njia ya simu na kumlazimisha afanye kazi yake mara moja. Fanny anakumbuka pale Esther alipomuuliza kuhusiana na uhusiano wake na Saúl na kujaribu kushuka. Isabel anaingia ndani na kumwambia Fanny kwamba anafikilia kwamba ni mjamzito. Saúl anasoma barua moja wapo aliyowahi kuandikiwa na Fanny alipokuwa kijana. Maki anakwenda kanisani kumuombea Juan Francisco. Saúl anachoma baadhi ya barua ambazo aliandikiwa na Fanny na Marina anaingia ndani na kumtharau kwa kitendo anachofanya. Akamlaumu kwa kile kilichotokea.

Esther anatembea mtaani na kumuona Alex akiwa na furaha huku akiongea na Angie, anajikuta akijilaumu mwenyewe kwasababu Alex amekuwa mbali nay eye. Esther anatamani kumfanyia vitu Angie ili awe karibu nao tena.

Alex anaondoka eneo lile na Esther anafanikiwa kumkamata kisha anamkumbatia huku akimwamgaria Angie. Anastasia anatembea pembeni mwa Juan Francisco maeneo ya nyumbani anakumbuka kilichotokea. Wakiwa njiani mwanaume mwenye bastola bado anawafatilia akiwa na nia ya kumuua Juan Francisco, lakini Anastazia anamuinamia Juan Fransisco na kumziba. Hivyo mwanaume mwenye bastola anashindwa kumuua.Mwanaume huyo anajificha kwenye kichaka na kuangalia kinachoendelea. Antonio anaingia ndani ya nyumba ambapo docta Herrera anamhudumia Juan Francisco.

Maki anaangalia gauni alilopewa na Ricardo na kupatwa na shaka pale Ricardo alipoingia ndani ya chumba. Juan Francisco anaweka maua karibu na Anastazia pale anapokuwa amefumba macho. Juan Francisco anamuomba afungue moyo wake. Marina anapata maumivu na kwenda kumuona Ricardo lakini Maki anamwambia kwamba amekwenda kucheza tennis. Marina anamwambia Maki kwamba amekua ni muovu na fisadi kwake.

Esther anajiangalia kwenye kioo, anagundua kwamba uso wake umekuwa na alama fulani, na kufikilia kwamba anatakiwa kufanya kitu kwani atashindwa kufanana na Angie. Juan Francisco na Anastasia wanamsikia mwanaume anayewafatilia akikoki siraha yake na kumtafuta
Anastasia anapiga kelele na bunduki inamlenga Juan Francisco, ambaye anaanguka chini.Wakati huo huo wanasikia wanasikia mlio mwingine wa bunduki baada ya ule wa kwanza, ambaye anakuwa ni Antonio aliyemuua mwanaume mwenye siraha.

Aurelio anakwenda sehemu ile anakuwa na wasiwasi kwasababu yuko katikati mwa mtaa. Anastasia anamuuliza Juan Francisco kama yuko sawa, Juan Francisco anamwambia kwamba kidonda chake kimefumuka. Anastasia anamlaumu Antonio kwasababu amemlenga Juan Francisco, na Antonio akamwambia kwamba anatakiwa kuwa muangalifu kila siku ni kutokana na mwanaume aliyemuua na kisha akadai kuwa hatomuachia Juan tena kisha akamfunga pingu.

EPISODE S–069

Mwanaume aliyekuwa na siraha amempiga Juan Francisco lakini Antonio amemuua kwa niaba. Antonio anamfunga kamba Juan Francisco. Anastasia anamuomba asimchukue kwasababu ni mtu mwema. Juan Francisco anamwambia Antonio kwamba anatamani amchukue kwani mungu ndivyo amepanga kwa upande wake alikuwa akitafuta ushahidi kuwaonesha kuwa yeye ni mwema. Anastasia anamuomba Antonio asubiri kwani baba yake anakuja kumtibia kwenye kidonda kilichofumuka,na kwamba anaweza kumpeleka mbali baada ya hapo. Antonio yuko kwenye hall akisubiri mpaka docta Herrera atakapomuona Juan Francisco.

Juan Cayo anafika eneo lile na Antonio anamwambia kuwa Juan Francisco anamaumivu mengine baada ya kuvamiwa. Juan Cayo anaingia ndani ya chumba ambako docta Herrera anamtibia Juan Francisco. Docta Herrera anaondoka chumbani, Anastasia na Juan Francisco wanapanga mpango wa kukimbia.Anastasia anatoka ndani ya chumba na kulaumu kuwa kuna mtu amempiga jiwe kupitia dirishani na kumuumiza.

Antonio anatoka nje kuangalia kinachoendelea. Jacinta anaendelea kunywa wakati Maki na Marina wanawaangalia kutokea kwenye gari.Wanaongelea ujio wa watoto wao na jinsi watakavyofanya. Maki anatoka nje ya gari na kumlazimisha Marina kumsindikiza kwqenda kuongea na Jacinta. Antonio anaingia ndani ya nyumba, anagundua kuwa Juan Francisco amekimbia na aliyemsaidia ni Anastazia Juan Francisco anakimbia mpaka pale aliposubiriwa na Juan Cayo kwa ajiri ya kumpatia msaada. Ilikuwa ni majira ya usiku pale Marina alipogundua kuwa nyumbani kwake pamepambwa na maua rozi kila mahala, akaenda chumbani kwake ambako anahisindio muhimuzaidi.

Huko anakuta Saúl anamsubiri na Marina anamuuliza anafanya nini pale. Anambusu lakini anamdharau, kisha anamtisha na kumwambia asijaribu kumbusu. Ricardo na Maki wanakwenda kupata chakula cha usiku huku Maki akiwa amevaria gauni alilopewa na Ricardo. Walikuwa wakila chakula pale Juan Cayo alipokuwa akimpigia simu na kumuelezea atafute sehemu ambayo wataenda kumficha Juan Francisco.

Alex anamchukua Esther kwenye nyumba yake wanaongea mpaka hapo alipomuuliza kama bado anataka kumuoa. Wakati wa chakula cha usiku mmoja wa wateja anakuwa karibu na Ricardo ambaye anamtambulisha kwa Soraya kama mke wake. mwanamke anayeoneshwa sura ya Soraya anaumia kwani sura hiyo imefanana na ya Rosaura. Soraya naye anaumia.

Mwisho, mwanamke anaondoka na kusema tena kwamba sura ya Soraya ni kama ya Rosaura. Flor anamkumbatia tumbo la Fanny wanaongelea majina ya kumpatia mtoto pale atakapozaliwa. Maki anapata hasira baada ya kuambiwa na mwanamke kuwa amefanana na Rosaura kiasi cha kusababisha akose hamu ya chakula, Ricardo naye akawa anasisitiza kwamba wamsahau Rosaura.

EPISODE S–070

Ricardo na Maki wanarudi nyumbani kwao na Ricardo anamuuliza nini kimetokea. Maki anadai kuwa amechoka. Ricardo anamwambia kuwa asiyasikilize maneno ya mwanamke wa kwenye mghahawa. Soraya anamuomba amuoneshe picha ya Rosaura lakini Ricardo hakutaka kumuonesha picha hiyo. Ricardo anasema kwamba hana picha ya mwanamke huyo, lakini Maki anataka kujua anafananaje. mwisho Ricardo anakiri kwamba ni Fabiola ambaye alimuua Rosaura kwasababu alikuwa akimpenda yeye.

Ricardo anaelezea kwa Soraya kwamba hakuweza kumsema Fabiola kwasababu alikuwa rafiki wa karibu na wazazi wa Fabiola. Saúl anakutana na Marina,ambaye amekaa kwenye ‘garden’ ya kwenye jengo, anamuuliza ni nini kimetokea.Akamjibu kwamba kuna vitu vinamchanganya.Soul hakuishia hapo akaendelea kumwambia kuwa anataka kujua kinachoendelea, Ingawa anajua kuwa anahisia kwa Fanny lakini amekuwa muwazi pale alipombusu.Saúl anamuuliza kwanini amemkatiza, akamjibu kuwa hawezi kujifungua mtoto na hakuna kinachoweza kumbadirisha. Maki anapiga simu kwa mchungaji Higinio kumuomba amsaidie kumficha Juan Francisco, lakini mchungaji Higinio anaogopa kuendelea kumsaidia na kumwambia kuwa wakutane siku inayofuata ili kuamua nini watafanya.

Siku inayofuata, mchungaji Higinio akamwambia Maki kwamba atamsaidia lakini anatakiwa kusali. Baada ya hapo wanakwenda sehemu ambayo wanakwenda sehemu ambayo watamficha Juan Francisco. Maki anamwambia mchungaji Higinio kilichotokea kwa Ricardo na mchungaji Higinio anamwambia kuwa kuna kitu kimefanyika kwasababu mara ya kwanza alipoangalia picha ya Rosaura alipata mshangao wa ajabu.

Juan Cayo anampigia simu mchungaji Higinio ambaye anamwambia ampeleke Juan Francisco uamiaji. Juan Cayo anamshukuru. Mchungaji Higinio anamwambia amshukuru Maki. Juan Francisco anashangaa pale anapomuona Soraya, anamuomba waongee kabla hajaondoka. Alex anajibu simu. Marina anaingia ndani ya mghahawa,anamchangamkia Jacinta, japo mhudumu hawezi kumuacha alipe bili ya kile alichokitumia. Marina anapata hasira sana ambazo zinamuogopesha Jacinta. Jacinta anashtushwa na hasira za Marina. Marina anamwambia kwamba yeye ni mama yake, anamuonesha picha alizonazo.

Esther anapiga simu kwa Alex lakini anashindwa kumpata. Alex anapata chakula na Angie. Esther anajaribu kuwasiliana na Alex kupitia simu ya mkononi lakini hawezi kujibu simu hiyo. Angie na Alex wanaongea kuhusiana na kila kitu,ikiwa ni pamoja na matatizo ya Esther. Jacinta anaangalia picha akijiuliza ni wapi alipokuwa yeye na Marina na kugundua kuwa ni binti yake. Jacinta anamkumbuka Carlitos na Marina, Marina anamwambia kuwa Carlitos alifariki dunia. Jacinta anakiri kwamba alikuwa akimtafuta kwasababu anamuhitaji. Saúl anaingia ndani ya ofisi yeye na Esther kisha anamuomba katibu muktasi kuwapisha. Saúl anashtushwa na shangazi yake baada ya kumwambia anatafuta nini ofisini kwake, anamdharau kwa kile kilichotokea kwa binamu yake,na kudai kuwa anamsaliti mjomba wake.

Esther anamuomba achukue vitu vyake kisha aondoke ndani ya ofisi. Saúl na Angie wanaendelea kuongea na anajaribu kumbusu lakini anamkwepa. Saúl anachukua vitu vyake , anawauliza wafanyakazi wa pale kama walipewa amri ya kumuangalia wakati anaondoka.
Maki anakwenda kumuona mchungaji Higinio, ambaye anakiri kwamba hakuwa mjwepesi pale alipomwambia kuhusu mke wa Ricardo. Mchungaji Higinio anachukua picha ya Rosaura na kuionesha kwa Maki, ambaye anagundua kwamba sura yake imefanana na ya Rosaura .
Mwisho.

No comments: