Monday, July 28, 2008

'TILL MORNING COMES' Darating ang Umaga'

By Hamida Hassan.

Story:
Darating Ang Umaga ni hadithi inayohusu mapenzi,maumivu,pia inahusisha familia moja ambayo inazungukwa na usaliti wa hali ya juu kati ya wanadada wawili waliotokea kusalitiana kwa sababu ya penzi, wanadada hao ni Mira (Eula Valdez) na Arriana (Vina Morales). Mmoja wa wanadada hao anatokea kuwa tajiri mfanya biashara wa kike, wakati mwingine ni maskini wa kutupwa.

Hadithi inaanzia huko San Mateo, ambako wanadada hao wanafanya kazi kama watumwa kwa Don Lucio (Dante Rivero),mwanaume katili aliyekuwa akimpiga mama yao, Milagros (Daria Ramirez). Arriana anafanikiwa kupata vito vya dhahabu na kumpata mpenzi ambaye ni mgeni katika mji huo naye ni, Abel (Ian Veneracion) pale baba yao (Spanky Manikan) alipokuwa hospitali anaumwa baada ya kupata ajali mgodini mkewe, Milagros akawa hana njia zaidi ya kumtoa mtoto wake wa kike kwa Don Lucio ajili ya kuokoa maisha ya mumewe. Walipokuwa holini walipokuwa wakiishi kama watumwa wanadada hao wakapanga njia ya kutoroka, na kutokana na usaliti aliokuwa nao, Mira anaondoka na kumuacha Arriana pembeni.

Hapa ndo hadithi inaanza kunoga kwani miaka ishirini inapita baada ya wanadada kutengana na familia yao kwa muda na wao wakiwa kipekee kwa kila mmoja. Je hii ni sababu ya dhahabu na utajili aliokuwa nao mmoja wao? Je Arriana atatafuta suluhu na kuunganisha familia yake na kuwa na amani kama mwanzo?
Washiriki ndani ya Tamthilia hii ni: Eula Valdez Vina Morales Ian Veneracion aliyecheza katika (Ikaw Lang Ang Mamahalin), Patrick Garcia yeye amecheza katika (Pangako Sa 'Yo), Jodi St. Maria (Pangako Sa 'Yo), Danilo Barrios (Sa Dulo Ng Walang Hanggan), Aiza Marquez (Sa Puso Ko Iingatan Ka), Sharmaine Suarez, Daria Ramirez (Tabing Ilog), Dante Rivero (Recuerdo de Amor), Glydel Mercado (Sa Dulo Ng Walang Hanggan) na Maribeth Bichara, naye amecheza katika (Pangako Sa 'Yo). Fuatilia Tamthilia hii....

No comments: