Tuesday, July 29, 2008

KESI YA ZE COMEDY, KUBENEA NA GHOROFA LILILOANGUKA ZANGURUMA.

Bw. Alfred Moshi ambaye ni mshitakiwa wa tano katika kesi ya ya kummwagia Tindikali mhariri wa Gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea, yuko nyan’ga nyang’a baada ya kugongwa na gari leo asubuhi.

Mbele ya Hakimu Mkuu mkazi wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam ilidaiwa na mwendesha mashitaka mkuu kanda maalum ya Dar es Salaam Charles Kenyela, kuwa mtuhumiwa huyo ambaye yuko nje kwa dhamana aligongwa na gari akiwa njiani kuelekea mahakamani hapo.


Kenyela alisema kuwa mtuhumiwa amelezwa katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, kitengo cha mifupa (MOI), kufuati ajali hiyo, Hakimu Lyamuya aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti mosi mwaka huu.

Wakati huo huo, washitikawa watatu katika kesi ya Ghorofa lililoanguka maeneo ya Kisutu hivi karibuni wameachiwa kwa dhamana na mahakama hiyo.Watuhumiwa hao ni James Mndeme, Kantilal Premij Raxman na Satish Gordhan Naran.


Aidha kutoka Mahakama ya Biashara Jijini Dar es Salaam, taarifa zinasema maamuzi katika kesi ya Ze Comedy na Channel 5 yamesogezwa hadi Agosti 15, 2008 kufuatia kile kilichodaiwa na mahakama hiyo ni kuonekana kuwepo kwa kasoro katika hati za viapo vya walalamikaji ambao ni kundi la Ze Comedy. Mahakama hiyo imeliagiza kundi hilo kuwasilisha viapo vipya Agosti Mosi mwaka huu.

Pichani Mhariri wa Gazeti la Mwana Halisi, Saeda Kubenea (Kulia) akiongea na mwandishi wa habari wa Gazeti la Habari Leo Halima Mlacha nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam baada ya kesi yake kuahirishwa leo.


2:Baadhi ya wasanii wa kundi la ucheshi la Ze Comedy wakitoka nje ya Mahakama ya Bishara Jijini Dar es Salaam leo baada ya kesi yao kurushwa hadi Agosti 15, mwaka huu.

3: Baadhi ya wahandisi ambao ni watuhumiwa katika kesi ya kuanguka kwa ghorofa eneo la Kisutu Jijini Dar es Salaam hivi karibuni, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu wakisubiri kesi yao kuanza kusikilizwa. PICHA ZOTE NA CHRISTOPHER LISSA/SAJUM

No comments: