Friday, July 25, 2008

NEVER SAY GOODBYE

EPISODE S-071

Saul anamwambia shangazi yake kwamba wakati anafanya mambo yalie alikuwa bado ni kijana mdogo.Esther anamwambia kwamba hakuwa mtoto pale alipotoa amri Juan Francisco auawe.Anamwambia kuwa alifanya vile ili kumuokoa yeye , kisha akamuomba amuelewe na kumwambia kuwa alikuwa na ndoto na kama alizokuwa nazo yeye na mjomba wake kabla hajamgeuka.Akamwambia kwamba wao ndio familia pekee aliyonayo na hakutaka kuachana nayo. Esther baada ya kusikia maneno hayo anasimama na kumkumbatia wakati Saul akitabasamu na kujifanya mwenye furaha.

Ricardo anampigia Saul na kumlalamikia kwasababu amri yake haikufanyika. Saul anaelezea kwa Ricardo kwamba ana matatizo fulani lakini Ricardo anamwambia kwamba yeye hajari atampeleka jela kama atofanya vile alivyomueleza.

Pale Ricardo alipomaliza kuongea kwenye simu, Aurelio akafika kwenye ofisi yake na kumuomba ampigie patna wake kutafuta kile anachokijua. Saul anafikilia kuhusiana na hali aliyonayo katika matarajio yake kuwa na Fanny inamsababisha ashawishike kwamba hatakiwi kuwa na wasiwasi kwasababu amefanya kila kitu kwa ajili ya Esther. Juan Francisco anampigia simu mama yake kjumwambia kwamba yuko sawa.

Maki anakwenda nyumbani na kuongea na Ricardo ambaye aliomba msamaha kwa tabia yake na kukiri kwamba amemfananisha na Rosaura. Maki anasema kwamba ana uhakika kwamba Juan Francisco hana hatia kwasababu hakurudi na kwamba yeye anachojari ni mtoto wake. Ricardo anamwambia kwamba yeye anachohitaji ni kumsaidia kumpata mtoto wake.

Maki anaangalia katika picha ya binti yake na kufikulia kama siku moja binti yake akiwa na picha harisi ya wazazi wake. Ricardo anaingia chumbani na kumwambia Maki kwamba wakala wa usafiri ana wasiwasi na wao lakini Maki akamwambia kwamba hatokwenda popote mpaka amempata mtoto wake. Ricardo anamwambia kwamba itachukua muda kumpata mtoto wake na kwamba anatakiwa kupumzika. Akasisitiza kwamba anatakiwa kumchukua mtoto wake, Ricardo akamwambia kwamba atamrudisha mtoto wake lakini anatakiw akusubiri.

Maki ana wasiwasi, Ricardo anamkaribisha kumtembelea Florcita na kumpa chakula kuhakikisha wanakuwa karibu kila siku. Esther yuko kwa daktari ambaye anashauri apigwe sindano ya Botox lakini Esther anaanza kulia na kusema maisha yake yanamchanganya na kuna kitu anaweza kufanya kuhusiana na hilo. Alex na Angie wanabusiana kila mmoja. Francisco na Ramon wanajificha pembeni mwa mti kumuona Florcita huko shuleni pale Maki na Ricardo walipofika shuleni. Maki amevaa kama jokeli wakati Ricardo anaongea na Flor. Ramon anamtongoza Isabel huko ofisini na kugundua jinsi alivyo ambaye anamwambia kuwa hayuko sawa nayeye anamwambia kuwa yuko sawa.

Carvajal na Aurelio wanaongea kuhusiana na matatizo waliyonayo. Aurelio anamwambia Carvajal kwamba Ricardo anajua kila kitu na kwamba amemtishia kuwa atampigia simu bosi wake. Marina anampeleka Jacinta hotelini. Ricardo anakiri kwa Maki kwamba atafanya kila kitu anachoweza kumpatia Flor na Maki familia.



EPISODE S-072

Marina anampeleka Jacinta clinic daktari anakuja kuongea na wao wakati Jacinta anajaribu kuiba kitu fulani. Pale Jacinta aliposikia kuwa anapelekwa chumba cha matibabu, anamuuliza Marina wapi anapompeleka.Baba wa Juan Francisco ana furaha na anaanza kucheza na Angie baada yu ya kufika nyumbani. Pale Angie alipomuuliza sababu ya kuwa na furaha, akasema kuwa ni kwasababu Juan Francisco yuko hai.

Angie anapata furaha pia baada ya kupata habari hizo kwasababu Alex anamkosea adabu ,hata hivyo baba yake Juan Francisco anamwambia kuwa Alex bado anaishi na Esther. Angie anamwambia kwamba halazimishi kitu chochote anaendelea kucheza kwa furaha. Jacinta anagundua mahali alipo na Marina anajaribu kuelezea pale wagonjwa wengine walipompeleka Jacinta sehemu nyingine. Esther anaenda nyumbani kwa Alex na kumpa kitu chakula na kumuuliza nini amefanya. Alex anafikilia kwamba amwambie ukweli.

Isabel anakwenda nyumbani na kumuona Aurelio akifanya kazi na computer.Pale Isabel alipokwenda kupata kahawa, simu yake ikaita, Aurelio akafungua begi lake kujibu simu ndipo alipoona kipimo cha mimba. Akamuuliza maana ya kipimo kile. Juan Francisco anampigia simu Fanny ambaye ana furaha kujua kuwa anaendelea vizuri.

Fanny akamwambia kuwa ni mjamzito lakini kitu hicho hakikumfurahisha. Isabel anamwambia Aurelio kipimo cha mamba ni cha Fanny. Alex anakwenda kuongea na mchungaji Higinio ambaye anaamwambia Alex kwamba anachezea hisia za watu wawili kitu ambacho hakifai. Anamshauri Alex kujiuliza yeye mwenyewe ni kitu gani anataka.

Juan Francisco ana wasiwasi pale anapofungiwa anataka kumuona Soraya pale Maki anapotokea. Maki anamwambia kuwa amemnunulia vitu fulani.Anamwambia Maki amekwenda kumuona mtoto wake, Maki akamlaumu kwa kufanya hivyo. Juan Francisco pia akamwambia kuwa amemuona yeye na mume wake akamwambia kuwa anataka kumsaidia baada ya baba yake kupotea.

Juan Cayo na mchungaji Higinio wanaongea pale majambazi walipoingia ndani ya kanisa. Maki na Juan Francisco wanasikia kelele nje ya nyumba wanatoka nje kwenda kuangalia. Akakiri kwa Maki kuwa amekuta vitu vingi huko. Esther anafika ofisini, Angie anamuuliza mbona yuko kimya lakini cha kushangaza ni kwamba Esther anaamua kumfukuza kazi na wanakuwa na majadiriano kuhusiana na hali ile.

Baada ya Angie kuondoka, Esther akampigia Alex kumuangalia. Juan Francisco anamwambia Maki kila kitu anachokijua na anapata mshtuko kujua kwamba watu anaowahusisha na kesi yake walimdanganya yeye pia.

Maki anamwambia kuwa alisalitiwa kwasababu Marina hawezi kuhusika na kesi. Marina anaongea na Saul na kulalamika kwani afanyi kitu kwa ajiri yake ‘Marina’ bali anafanya kwa ajiri yake mwenyewe.Saul anaamisha pesa katika akaunti ya Coalminer kwenda kwa akaunti ya Juan Francisco hivyo basi anaweza kuhamisha kwenye benki nyingine.

Maki anaendelea kurudi nyumbani na kumwambia Ricardo anakwenda kuoga lakini Ricardo anamuomba asiende kwanza kisha anamuonesha picha ya Rosaura. Maki alipoiona picha ile akagundua kuwa imefanana na ile ya mchungaji Higinio kisha anamwambia kuwa mwanamke huyo si Rosaura.


EPISODE S-073

Marina anakwenda kumtembelea Jacinta, nesi anamwambia kuwa Jacinta alikuwa na wakati mgumu kwasababu kurudi katika hali yake ni vigumu. Pale nesi alipoenda kumchukua Jacinta akagundua kuwa mwanamke huyo amepotea. Isabel anafika cliniki kutoa mimba.

Ricardo anapata hasira na kumwambia Maki amrudishie picha lakini Maki anamwambia kuwa ameipata kwenye mtandao. Ricardo kwa hasira anamwambia ampeleke kwenye compyuta akamuoneshe kwani kuna majina yanayofanana. Saul anakunnywa pombe pale anapodhani kampuni ya Coalminers´ itafilisiwa kwasababu wanastahili. Isabel anakimbia katika upasuaji na kuingia ndani ya gari yake kisha analia.

Carvajal anampigia Aurelio na kumwambia kwamba hatoamini uongo wa Ricardo, Aurelia naye anajibu kuwa anamuangalia Ricardo. Fanny anakwenda kwa Isabel na kumwambia kwamba alikwenda kutoa mimba. Marina anamkuta Jacinta akinywa pombe mtaani na Jacinta anamwambia kuwa alimwamini na kukubari kuwa alimkumbuka lakini hakumjua kwani aliamini kuwa atampeleka nyumbani. Marina akavunjika moyo na kuamua kuondoka.

Jacinta anampigia simu. Ricardo anaongea katika simu na kuomba msamaha kwa tabia aliyoionesha. Ramon anamtembelea Juan Francisco na kumwambia kwamba kuna uhakika wa mambo mengi lakini ataendelea kumtetea.ndani ya kuda huo Gino akapiga simu. Jacinta akaelezea kwa Marina kwamba alikuwa ndani ya baa maisha yake yote na atarudi katika hali yake taratibu.

Jacinta anamuomba Marina pesa anakubari kumsaidia kurudi katika hali ya kawaida. Marina anampatia pesa kulipia nafasi ya kuishi wakati wa usiku. Alex anampigia simu Esther lakini anamwambia kwamba yuko bize hawezi kuwa na muda na yeye. Esther anaongea na meneja wa benki kutafuta kilichotokea katika pesa zake, wakasema kuwa wataanza upelelezi.

Marina analia pale alipofika nyumbani kwa Maki na kumwambia kwamba ana kitu anataka kukiri kwake. Maki anamwambia kwamba pia ana kitu anataka kukiri kwake lakini hana uhakika kama ni Marina au Juan Francisco aliyemsaliti. Marina anachanganyikiwa kwani hajui afanye nini juu ya mama yake, Maki anamuuliza nini kilichotokea. Marina anamwambia kuwa yeye ni rafiki yake anaomba amwamini.


EPISODE S-074

Esther na Saul wanaongelea yale waliyoyafanya. Fanny anafika ofisini na kumuuliza Saul kama bado anafanya kazi pale. Ester anawaambia kuwa waigize kama wameibiwa,Fanny anawaonya na kuwaambia wafanye haraka. Saul anafikiria kwamba anefanya kazi nzuri ambayo kwasababu hakuna mtu anaweza kuhisi ni yeye. Aurelio anafika baada ya kuambiwa na kumshauri Esther kumpigia Ricardo ambaye pia alikuwa ni mwenza katika biashara.

Ricardo anauza pete wakati Maki anaandaa begi lake. Esther anampigia simu Ricardo na kumuomba aende haraka iwezekanavyo kwasababu anataka kuongea naye kuhusiana na kitu fulani muhimu. Ricardo anamuomba Maki kwenda naye ingawa hataki kudili na watu wale. Ricardo anamkumbusha kuwa pia ni mwanashea na mmoja wa wahusika wa kwenye bodi. Ricardo anafika katika ofisi ya Esther na kuwauliza tatizo ni nini wakamwambia kuhusiana na mtu aliyekomba pesa za kampuni kwenye akaunti benki.

Ramon anamuona Isabel na kumbusu naye anarudishia kwa kumbusu. Ricardo anamwambia Esther aelezee kilichotokea. Esther anamwambia kwamba ni yeye tu ambaye anaweza kuwasaidia kwasababu benki imewataarifu kuwa itafanya upelelezi ambao utachukua muda wa miezi miwili anachotakiwa ni kufanya makubariano ya haraka.

Kwasababu Ricardo ndio mtu pekee ambaye anaweza kuwasaidia hivyo anachukua nafasi hiyo kuwasaidia lakini tu kama ata pata jengo la Casa Paris kama thamana.Ramon anamuomba kumuoa Isabel. Ricardo na Maki wanaongea faragha wakati Esther anaongea na Fanny, ambaye anamwambia kwamba hataki kufanya kazi kwa Ricardo Alvarez, lakini Esther anamuomba afikilie kuhusiana na familia. Maki anamwambia Ricardo kwamba kuna kitu hakitaki katika familia hiyo. Ricardo anakuja karibu na Esther na kumuuliza kama wamefanya maamuzi.

Ricardo anataka kusherehekea baada ya kupata dili hilo. Esther anampigia simu Alex pale anapokumbuka wakati mzuri aliokuwa nao kwake, Alex hakujibu kwasababu alikuwa kitandani na mwanamke mwingine. Saul yuko tayari kwenda kazini pale alipomuona Marina amebebelea majivu ya Carlitos. Juan Francisco na Ramon wanapata kikombe cha kahawa na kumuongelea Isabel. Alex anashtuka pale alipomuona mwanamke kitandani.

Ramon anapatia Isabel juisi alipokuja Aurelio akamuuliza kama Isabel alimwambia kuwa ni mjamzito,Ramon anashangaa baada ya kusikia habari zile. Esther anamsubiri Ricardo asaini mkataba, pale document zilipofika fanny akakataa kuzisaini, kwasababu ayuko tayari kupoteza kampuni kabla haijamilikiwa na Soraya.


EPISODE S-075

Fanny anaondoka kwenye mkutano bila kutarajia. Esther anampigia simu Fanny ili akae katika kikao lakini anadai kuwa ni lazima ajibu simu. Anaacha mkutano kwa ajili yakwenda kuongea na Juan Francisco na kumwambia kila kitu kinachoendelea. Juan Francisco anamwambia amuamini Esther katika mambo hayo kwani ndio muhusiaka mkuu.

Baada ya kupokea simu anajiuliza ni kwanini Kampuni iwe na jina la Soraya. Ramon ana hasira na Isabel kwasababu hakumwambia kuwa ana ujauzito na hakutaka kusubiri majibu yake. Jacinta anamsubiri marina kama walivyokubariana. Jacinta anamwambia hawezi kupanga nyumba, kwasababu sehemu waliyokuwepo haivutii na kumwambia Marina ampeleke kwenye hoteli nzuri, lakini Marina akamwambia kuwa hatofuata uongo tena.

Esther mwisho anasaini mkataba wakati Fanny analia huku Ricardo na Soraya wakimuangalia jinsi anavyolia, Ricardo anatabasamu. Alex anaongea na mwanamke aliyelala naye na pale alipoondoka chumbani simu yake ikaita mwanamke yule akaipokea.

Alikuwa ni Esther ambaye alimuuliza mwanamke yule kama ni mfanyakazi, anamcheka kwa swali lake na kumwambia kuwa yeye si mfanyakazi kisha akamwambia kama anaujumbe amfahamuachie yeye atampatia Alex. Marina anakunywa pombe na kuanguka chini ovyo naye Jacinta anashikuru na kuondoka kwani hawezi kumuona.

Esther anamfikilia mwanamke aliyepokea simu ya Alex na pale alipoambiwa na Maki kwamba abaki katika kampuni mpaka pale watakapomaliza matatizo akakataa kutoa msaada huo. Mwanamke aliyekuwa katika chumba cha Alex anamuonya Alex kuwa karibu na Esther. Fanny anamsikia Maki akiongea na kujikuta anapandwa na hasira. Maki anagundua kwamba Fanny amekunywa na kumkumbusha kwamba ana mamba na pombe si nzuri kwa mtoto.

Maki anampigia simu Ricardo na kumwambia alikuwa sawa kuhusiana na wale wanawake wawili, Ricardo anamwambia anatakiwa kujiamini yeye mwenyewe na kwamba atahesabu mchango wake. Pia anamwambia Maki kuwa anatakiwa kwenda Spain na kisha atampigia simu akitaka kurudi. Fanny anatoa malalamiko yake kwa Isabel na kumlaumu Soraya kwa tabia yake baada ya kutoa malalamiko hayo akazimia, Isabel anamuomba Saul amsaidie kumbeba pale Maki atakapoingia ndani, kisha anamwaambia kuwa ameshamwambia asiwe anakunywa Esther anakwenda katika jengo la Alex na kumbusu kwenye midomo yake.

Marina anaamka akiwa amekunywa, Jacinta anampatia juisi imsaidie ajisikie vizuri. Marina mwishi anamwambia mama yake kwamba ataishi naye. Maki anamtembelea mchungaji Higinio pale Juan Cayo alipowakatisha na kuwaambia kuwa Juan Francisco amekubwa na kitu kibaya. Esther anataka kuongea na Alex ambaye anamuuliza kama hana hasira kwasababu mwanamke amepokea simu yake. Mchungaji Higinio anawaambia kuwa wanatakiwa kumuita daktari. Maki anakwenda kumuona na kumkuta ana homa kali.

Mchungaji r Higinio anamwambia Soraya kwamba wanatakiwa kufanya vile walivyoelekezwa na daktari, lakini anawaonya kuwa kama homa haitashuka wanatakiwa kumpeleka Juan Francisco hospital, lakini Soraya anakuwa kinyume na wazo lile. Mchungaji Higinio anamwambia kwamba anatakiwa kurudi lakini hawawezi kujishusha na kumuomba Juan Cayo kumuhudumia Juan Francisco. Anamwelezea mchungaji Higinio kuhusiana na picha aliyooneshwa na Ricardo, na kwamba ameona kuwa hawafanani kabisa na yeye, Mchungaji Higinio anashangazwa na majibu hayo, lakini Maki bado anamwambia kuwa hana sababu ya kumshuku.

Esther anamwambia Alex kwamba yeye hajari kama mwanamke amepokea simu yake. Ricardo anamuona Fabiola huko Spain na kuongea naye kuhusiana na kitabu na kisha anamuomba arudi naye lakini anakataa. Ricardo anamwambia kuwa anamuhitaji na anatakiwa kufuata vile anavyotaka. Marina anampeleka Jacinta maliwatona na kumwambia kuwa aingie aanze kuoga. Alex na Esther wanaongea na mlango unagongwa.

Wanawake hao wanajikuta wamefahamiana mmoja wao anasema amesahau kitu ndani ya nyumba, Esther anajaribu kumuonya mwanamke anayemtuhumu kuwa anamchukua mume wake na kumwambia akaembali na Alex, lakini hakujari. Meneja wa benki anakwenda Casa Paris kuongea na Saul na kumfahamisha kwamba wamegundua kuwa mwizi wa pesa ametokea kwenye kampuni yao.

Itaendelea wiki ijao...

No comments: