MADA YA WIKI HII
Wewe na mkeo mumejaliwa kupata watoto wanne, miongoni mwao yupo wa kiume mmoja.
Binti yako wa kwanza ana umri wa miaka 23, wa pili 20, wa tatu miaka 19. Mtoto wako wa kiume ana miaka 15.
Baada ya kuhitimu elimu ya msingi hakuna aliyebahatika kuendelea na sekondari, mkiwa kama wazazi wa kipato cha chini mliamua kuwapeleka VETA ili wajifunze ufundi.
Wakiume anasomea ufundi Seremala na dada zake wawili wamejifunza upakaji rangi na aliyebaki anajifunza ufundi bomba.
Hivi karibuni mabinti zako walikuwa katika hali isiyo ya kawaida, kufuatia hali hiyo mkeo aliwatilia mashaka na kuamua kuwabana ndipo wote walibainika ni wajawazito.
Mlipowabana wawaeleze wahusika, wakamtaja binamu yao ambaye hivi karibuni amerejea nchini kutoka Ulaya.
Ungekuwa wewe ungefanya nini?
No comments:
Post a Comment