Wednesday, July 2, 2008

SERIKALI SIKIA KILIO CHA WANANCHI WILAYANI RORYA

Wananchi wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, wameiomba Serikali kuingilia kati wizi wa mifugo hususan Ng'ombe unaofanyika katika wilaya hiyo.

Baadhi ya wawakilishi wa wananchi hao leo walitinga Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam, kuzungumzia tatizo hilo mbele ya Waandishi wa Habari, ili kufikisha kilio hicho kwa wahusika, ambapo walisema tatizo hilo sasa limekuwa sugu wilayani humo ambapo wamewatuhumu wananchi wa Kenya, wasiyo waaminifu kujihusisha na vitendo hivyo huku wakitumia siraha kali na kiwaua wananchi hao.

Pichani msemaji wa wananchi hao Bw. Martin Ochoro Ndira (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika mkutano huo leo mchana, kulia ni Bw. Andrea Nduko, mmoja wa wakazi wa wilaya hiyo.

No comments: