Thursday, July 3, 2008

Kumruhusu mumeo kuruka ukuta ni ushamba wewe

Wiki hii shoga yangu acha nizungumzie tabia ambayo baadhi ya wanawake wenzetu wamekuwa nayo huku wenyewe wakiamini kwamba, eti kufanya hivyo watakuwa wakiwabana waume zao wasitoke nje ya ndoa.

Ni hivi karibuni tu niliongea na mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la mama Faiza ambaye yeye aliomba nimshauri kwamba, amekuwa na tabia ya kumruhusu mumewe ‘amruke ukuta’ na kwa muda mrefu akawa amezoea na kujisikia raha huku mwenyewe akishindwa kuacha kwa lengo la kutaka kumzuia mumewe asitoke nje ya ndoa.

Wasomaji wangu wengi walimshauri kuacha tabia hiyo chafu kwasababu ina madhara makubwa. Kimsingi wanawake wanaowaruhusu waume zao kuruka ukuta kwanza niwaeleze tu kwamba, kufanya hivyo sio njia ya kumbana asitoke nje ya ndoa, usipojua kumshika vilivyo hata kama unamrukisha ukuta anaweza pia akakusaliti.

Lakini pia wanaofanya kamchezo hako wanapata hasara zifuatazo:
Kwanza mumeo licha ya kwamba atakuwa anafanya lakini pia atakudharau kweli.

Atakuona ni mwanamke usiye na uelewa kwa kuwa unafanya vitu ambavyo vina madhara makubwa
pili ukishazoea mchezo huo utakuwa husikii raha yoyote pale utakapokuwa unafanya tendo la ndoa kupitia njia ambayo ni halali na matokeo yake ikitokea huyo mumeo akakuacha ama akafariki na ukaolewa na mwanaume asiyeupenda mchezo huo.

Lazima atapata tabu na unaweza kufikia hatua ya kumlazimisha akuruke wakati yeye hapendi mchezo huo, shosti utaiona ndoa ni chungu.

Tatu ni pale utakapofika wakati wa kujifungua. Unaweza ukashanga unajifungua kwa operesheni na hapo ndipo utakapojikuta unaambulia mitusi kutoka kwa manesi ambao watabaini tu kwamba unalazimika kujifungua kwa njia ambayo sio halali kwakuwa umekuwa na tabia ya kumruhusu mumeo kuruka ukuta. Ni aibu shosti hivyo kama wewe ni mmoja wa wanawake wenye tabia hiyo iache mara moja.

Labda mwisho nikuulize wewe mwanamke mwenzangu mwenye tabia hiyo, hivi huoni kwamba ni kujidhalilisha kufanya hivyo? Hivi huoni kwamba unamkosea Mungu? Jamani mambo mengine tunayafanya lakini tufikirie na madhara tunayoweza kuyapata baadaye.

Sio unafanya tu eti ili kumridhisha mumeo. Mumeo ndio akufanye uyahatarishe maisha yako kweli? Hata kama ndio kumpenda kumbuka mwanaume mwingine hatosheki hata ukimpa nini bado unaweza kushangaa anakuwa na tamaa ya kutoka nje.

Tujithamini shoga zangu, kwani wanaume wanaotufanyisha mchezo huo hawatupendi na nikunong’oneze kitu, mumeo akikutaka aruke ukuta, mwambie akupe talaka yako, hafai huyo kuwa mumeo.

Ni hayo tu kwa leo, tuonane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.

No comments: