Thursday, July 3, 2008

Mtangazaji ajibu mapigo

Siku chache baada ya gazeti hili kuandika habari ya aliyekuwa Mtangazaji wa Channel 5, Teddy Kalonga ‘TK’ kudhalilishwa mtandaoni, mwanadada huyo amejibu mapigo na kueleza kuwa, licha mrembo mwenzake Mange Kimambi kumchafua bado anaamini kuwa yeye ni msafi kuliko yeye.

Kwa mujibu wa barua pepe aliyoituma kwa gazeti hili hivi karibuni akiwa nchini Marekani, Teddy alisema kuwa maelezo yaliyoandikwa na Mange kupitia mtandao wake wa www.mangekimbi.blogspot.com yaliyolenga kumchafua ni ya kupuuza.


TK alisema, hata kama rafiki yake aliamua kumvunjia heshima mbele ya jamii, bado anaamini kwamba watu wanafahamu ukweli juu yake na jinsi asivyoweza kulingana na Mange kwa sifa nzuri.

“Hata kama kaamua kunichafua bado hana sifa nzuri ya kujilinganisha na mimi. And I do respect myself. I am smart and hard working,” alisema Teddy akimaanisha kwamba yeye anajiheshimu. Akizungumzia madai ya kwamba hajasoma na kiingereza anachokizungumza ni cha kubabaisha, mtangazaji huyo alidai kuwa maelezo hayo sio ya kweli kwani alisoma hadi kidato cha sita na sasa anaendelea na masomo.

“I completed A-Level even though I didn’t do my last exams kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu. Lakini sasa niko Chuo naendelea na masomo. So, whatever has been said naona kama kuna ukuta mkubwa unanitenganisha the real me and that lies,” alisema Teddy akichanganya na ung’eng’e kuonesha msisitizo.

Hata hivyo, Teddy alikiri kuweka picha ya Mange kwenye mtandao wake wa www.totalknockout1.blogspot.com bila idhini yake, lakini alitanabahisha kuwa, alifanya hivyo kwa kuwa anamjua rafiki yake huyo anapenda sana ‘promo’.

“Ni kweli nilimweka kwenye blog yangu bila ya ruhusa yake huku nikiwa na lengo la kumpromote kama alivyokuwa akiniomba nimfanyie mahojiano nilivyokuwa EATV lakini matokeo yake...nimeishia kutukanwa matusi,” alisema Teddy.

Katika gazeti letu la wiki iliyopita tuliandika habari iliyokuwa inahusu kudhalilishwa kwa Teddy mtandaoni kufuatia picha yake akiwa nusu uchi kutundikwa mtandaoni pamoja na kutukanwa matusi ya nguoni na rafiki yake aitwaye Mange.

2 comments:

Anonymous said...

Dada Tk don't worry, mange ni msenge, mshamba anasura mbaya kama kopo la chooni, shapeless, hajui kuvaa kaolewa na mzungu chokora ngozi imechoka na sura mbaya kama kizee. Check mtoto TK alivyotulia na muwe handsome na ni kijana.

Anonymous said...

Tk why did you have to start a fight with Mange? Ya'll adults and popular and what you doing might play an unsignificant role for the rest of your life... Nobody has ever chocked from swallowing her pride so swallow yours and apologise to Mange... A lady would apologise... Let me see if you are a man