Aliyekuwa mshiriki wa mtanange wa kumsaka Miss Ilala mwaka 2008, Dotto Msoka, hivi karibuni amejikuta akiangua kilio ukumbini baada ya kushindwa kuingia katika hatua ya kumi bora katika mashindano hayo kama alivyotarajia.
Dotto alitoa kali hiyo ya mwaka ndani ya Ukumbi wa City Garden (Railway Club) uliopo jijini Dar es Salaam, kulikofanyika mashindano hayo ambapo ilidaiwa kuwa mrembo huyo alijiamini sana kwamba angeingia katika hatua ya kumi bora na kunyakua taji.
Awali, mrembo huyo mwenye mvuto wa hali ya juu alionekana akitabasamu wakati wote huku baadhi ya watu wakimpa asilimia nyingi za kuibuka mshindi, lakini baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga kutaja majina kumi bora na Dotto kutosikia jina lake, aliingia katika chumba cha kubadilishia nguo na kuanza kulia.
Aidha, baadhi ya warembo wenzake walilazimika kutumia nguvu kubwa kumtuliza na kumtaka akubali matokea lakini ilishindikana, kwani alizidi kulia kwa sauti kubwa na kuwafanya watu waliokuwa ukumbini hapo kupigwa na butwaa.
Hata hivyo, baada ya kupita muda mrefu mlimbwende huyo alipunguza hasira zake na kunyamaza lakini alionekana kusisitiza kutokukubaliana na matokeo.
Katika mtanange huo Slyvia Mashuda aliibuka kidedea na kutawazwa kuwa Miss Ilala 2008.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment