Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni katika masuala ya Miundombinu, Zitto Kabwe ameitahadharisha serikali ya Chama Cha Mapinduzi kuwa, watanzania wataipumzisha na kuwapatia wapinzani waongoze nchi, katika uchaguzi ujao.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, alisema hayo jana wakati akiwasilisha hoja ya upande wa upinzani juu ya Bajeti ya Wizara ya Miundombinu iliyosomwa bungeni na Waziri, Shukuru Jumanne Kawambwa hivi karibuni.
“Kambi ya upinzani inatoa mawazo mbadala ili walioko madarakani wayafanyie kazi, lakini kama watashindwa wananchi watawapumzisha, na sisi tutapewa kazi hiyo (kuongoza nchi), uwezo wa kufanya hivyo tunao.
“Viongozi walioko kambi ya upinzani wana macho wanaona, wana masikio wanasikia, wana midomo, wanasema na wana ngozi hivyo wanahisi.
Ndio maana hata matendo yote ya ufisadi nchini ambayo wameyasema yameonekana kuwa ni ya kweli,” alisema Mbunge huyo kijana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment