Monday, June 30, 2008

Miss Tz kiziwi

Issa Mnally na Amina Salim
Miss Tanzania 2008, huenda akawa mlemavu endapo majaji wa mashindano ya kumtafuta mnyange wa Kanda ya Kinondoni, watampitisha mrembo Caroline Emmanuel Mwakasoka kwenda fainali za kitaifa na baadaye kushinda.

Caroline, anapewa nafasi kubwa ya kushinda kwa kuwa anavyo vigezo karibu vyote vya urembo, isipokuwa kasoro ya ulemavu wa kusikia (kiziwi) ambayo inaelezewa kwamba inaweza kuwafanya majaji wamnyime nafasi ya kuiwakilisha nchi Miss World.

“Nadhani majaji wataona akishinda Miss Kinondoni na Miss Tanzania, atasumbua kwenye ushiriki wa Miss World kwa sababu italazimika awe na mkalimani wa viziwi, vinginevyo sifa zote anazo,” alisema mmoja wa waratibu wa Miss Kinondoni (jina kapuni) ikiwa ni maoni yake binafsi.

Shindano la kumtafuta Miss Kinondoni mwaka huu, litafanyika Ijumaa hii (Julai 4) katika Ukumbi wa Msasani Club, Dar es Salaam ambapo Bendi ya Akudo Impact ‘Pekechapekecha’ na mwana-Bongo Flava, Mwasiti Almas anayetesa na wimbo wake Hao, watafanya makamuzi ya kusindikiza warembo.

Siku mbili baada ya kinyang’anyiro hicho, yaani Jumapili hii kwenye Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe, jijini, kutafanyika ‘shoo’ ya kumtafuta Miss Temeke 2008 sambamba na kuwapata wawakilishi watatu wa kwenda kwenye Fainali za Miss Tanzania 2008.

No comments: