Monday, June 30, 2008

MORE THAN LOVE


Tamthilia hii inaanza ikiwa ni upepo mkali, inaonesha mwanaume mmoja anapigwa risasi na mwanaume mwingine ambaye hajulikani anajaribu kukimbia huku, pale anapopigwa risasi anadondoka anamdodosha mtoto mdogo aliyekuwa analia, kwa bahati nzuri mtoto huyu anaanguka ndani ya beseni karibu na mto. Hadithi inaendelea miaka mingi baadae.

Mtoto huyo ambaye ni Eli kwa sasa amekua na kuwa mwanaume mkubwa. Anakuwa ni mwanaume wa kujitolea na mtafutaji, anajitolea kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya familia yake.
Wahusika wanne wakuu wa tamthilia hii wanakutana kwa mara ya kwanza katika sherehe maalumu : ikiwa Eli anafanya kazi kama mhudumu wa baa; JB akiwa ni mkubwa katika kampuni ya meli ya mama yake aliyokuwa akiifanyia kazi; Jackie mpenzi wa JB na mtoto wa tajiri mkubwa anayemiriki Benki, ambaye anajaribu kuwa binti mwema katika familia na msichana anayejitahidi kuwa mwema kwa mpenzi wake. Celine naye amecheza kama binamu wa Jackie, ambaye matendo yake mengi yanaendana na ya Jackie. Pia kiungo kingine kinakuwa ni Pong, kaka yake Eli ambaye anamtorosha Jackie lakini anashindwa kufanikiwa.

Week 1
Baada ya kutoroshwa kwa Jackie familia ya Madrigal, Magsaysay, ya akina Jackie inaamini kuwa binti yao kipenzi amefariki. Eli anafanikiwa kumficha Jackie katika kijiji kimoja ‘kusikojulikana’, wakati Pong akijaribu kumshawishi Dadoods kuondoka. Jackie anafanikiwa kuamka lakini anakuwa amepoteza kumbukumbu zake hajui kilichowahi kumtokea, anajitahidi kuwa mke mwema kwa Eli akiamini kuwa Eli ni mume wake. JB baada ya kuamini kuwa mpenzi wake amefariki anaamua kutafuta amani na kuwa karibu na Celine.

Week 2
Ndani ya wiki hii, Eli anagombana na mtu akiyekuwa na makosa wakati Jackie anaangaika na maisha ya kimaskini ya kijijini,. Jackie bado ana maswali mengi kuhusiana na kusahau yaliyotokea zamani, lakini anajikomiti kuwa mke mwema wa Eli. JB anamuona Celine ni mtu wa maisha yake katika maisha yake mapya hivyo anakuwa karibu naye wakati wote huko kisiwani. Celine anaamua kuendelea na maisha yake baada ya kumuona JB aelekei na kudai kuwa hawezi kupingana na kumbukumbu za Jackie kwa JB, lakini inaonekana kuwa JB ana wazo jipya la kwake peke yake. Aling Bebeng anamtafuta binti yake anampeleka Jackie Manila, ambako Celine anamuona.

Week 3
Wiki hii,Celine anamuona Jackie bandarini lakini hamshawishi mtu yeyote kama binamu yake yuko hai. Eli anahangaikia pendo lake na Jackie akitamani kulitengeneza penzi hilo liwe jipya kwa kufuata sheria za ndoa. Mlinzi wa Eli anaona kidani cha Eli kwenye mkufu aliokuwa nao na kuonesha kama anakifahamu,hivyo anaamua kutokiachia. JB anampa ofa ya kazi Celine, na kukubari kuwa anamuhitaji katika kutafuta uhuru.Ingawa alikuwa na wasiwasi kuhusiana na mambo aliyomfanyia, Celine anaamua kukubari kazi ya JB anajitolea kufanya kazi ka offer to run the next major event for his luxury liner. JB's backstory is revealed in flashbacks from his childhood, and new tensions arise between JB and his mother.

Week 4
Katika wiki hii, uhusiano kati ya Eli na Jackie unaendelea kukua, mpaka hapo Jackie anaamini kwamba hakuwa mwema kwa Eli. Celine anapokea matokeo mazuri katika kazi yake mpya, na kumshinda Corazon aliyekuwa akimpinga. Eli anampeleka Jackie Manila, akiwa na dhumuni la kumrudisha katika familia yake, lakini mipango haendi kama alivyopanga. JB na Celine wanazidi kuwa pamoja,JB anaanza kufikilia kama yuko tayari kuendelea na maisha bila ya kuwa na Jackie .
Week 5

Jackie anajitengenezea upendo kwa Dadoods na Pong, na kisha anamfanyia Eli sherehe ya kuzaliwa kwake. Eli anafuata ushauri wa baba yake wa kuendelea kumdanganya Jackie. Kevin Romero anamfukuzia Celine, na kudai kuwa hawezi kumuachia kiurahisi hivyo. JB anajaribu kumuweka akilini Celine, na kukubari kuwa anamuonea wivu. Jackie na Eli wanarudi kijijini. Celine anajaribu kupigania maisha yake ya baadae,baada ya kuona kuwa anaangushwa.

Week 6
Wiki ya sita ,Jackie anaendelea kukumbuka mambo mengi ya nyuma, lakini pamoja na kukumbuka bado anatamani kuendelea kuwa na Eli. Eli anampatia Jackie kidani chake, pia anatafuta njia ya kumnunulia Jackie pete ya ndoa. Imelda anataja uhusiano wa zamani kati ya Corazon na Fidel. Pale JB na Celine walipoenda kambini, Celine akaelezea penzi lake kwa JB, naye akakubari kuwa anamuhitaji. Celine na Jackie wanakutana mjini na kugongana kila mmoja, lakini Jackie anakimbia mbali. JB anachanganyikiwa pale Corazon anapomuonesha picha.

Akiwa amechanganyikiwa, Celine anaendesha gari haraka sana hakuona kama kuna gari kubwa linakuja. Jackie anagonga kichwa chake na kukumbuka kila kitu pale anapoamka. Baada ya hapo anaingia ndani ya basi na kurudi nyumbani kwa baba, Fidel alipokuwa akiangalia nje ya dirisha akamuona.

Week 7
Wiki hi ukurasa mpya unaanza pale Jackie alipokumbuka mambo yake ya nyuma na kurudi kwa baba yake, mbaya zaidi hakumbuki kuwa karibu na Eli tena. Celine anavunjika moyo baada ya kumuona Jackie, lakini anamwambia JB anatakiwa kusubiri mpaka hapo atakapomwambia Jackie ukweli kuhusiana na wao. JB anajikuta akiumizwa na uhusiano wake.

Corazon anamwambia JB anaweza kuchagua kati ya Jackie ama Celine. Eli ana maumivu pale anapogundua kuwa Jackie hakumbuki chochote kuhusiana nay eye, Ingawa habari hiyo inawapa nafuu akina Pong na Dadoods. Jackie anamshangaza kila mmoja kwa tabia zake mpya na upendo kwa mama yake, Monique anajaribu kuongea na Jackie, lakini Fidel anamuonya akae mbali naye. Eli hawezi kukaa mbali Jackie hivyo anaamua kumfata kwenye chakula cha usiku na JB.


Week 8
Katika wiki hii, JB anaendelea kutoneshwa na Celine na Jackie,wakati Celine anajiandaa akisubiria kwa hamu Jackie ajue ukweli juu yao. Eli anaugulia maumivu ya kupoteza uhusiano wake na Jackie, mpaka hapo alipolala na kupata ndoto kutoka kwa mama yake ambayo ilimsababishia ashtuke na kupata akili. Fidel anajikuta ni mgumu kusema hapana pale Jackie anapohitaji kujenga uhusiano na mama yake, Monique. Kwa niaba hiyo anamaua kumpeleka Jackie US kutafuta matibabu ili apate kumbukumbu zake, kisha baada ya kufanya hivyo akamtuma Imelda aende kumuonya Monique asihudhurie sherehe ya Jackie.

Week 9
Katika wiki hii ya tisa:, tunaoneshwa mambo ya nyuma jinsi Celine na JB walivyokutana mara ya mwisho kama vijana kipindi cha joto, na JB akamwambia Celine kwamba yeye ni msichana ambaye siku moja atamuoa. Lakini Corazon akaingilia na kuwakutanisha JB na Jackie. Eli anarudi kijijini kwa Mang Simo, na kumwambia kila mmoja kwamba Jackie anatakiwa kurudi Manila kwa ajili ya kazi. JB mwisho anakumbuka mambo yake ya zamani na Celine na kumchagua Jackie... ndipo Celine alipoamua kuachana naye na kwenda kwa Romero.Eli anakutana na waarifu na kupata kipigo,ambaye kwa mara ya kwanza anakutana na JB na kupata ugeni kutoka kwa Jackie ambaye haoneshi kumkumbuka.

Week 10
Celine anamwambia Jackie kwamba amemuaribia kila kitu. Celine anamwambia Imelda ampeleke mbali asione mambo yanayotokea. JB anadondosha simu yake ndani ya bwawa. Gio anamwambia Celine asipoteze maisha yake kwa mwanaume. Jackie anachanganyikiwa kuona JB amepoteza namba ya Pong. JB anagundua kuwa Jackie ndiye mwanake anayemfaa.

Jackie anasisitiza kuvaa kidani cha Eli. Monique anafika katika sherehe ya Jackie lakini anasema kuwa hawezi kukaa. Fidel anafungua sherehe Jackie anamshukuru kila mmoja. Corazon anamuomba Fidel wacheze pamoja, lakini wanaacha kucheza baada ya Fidel kuuona uso wa Monique. Jackie anamwambia JB hana uhakika kama anampenda.

Fidel anamshauri Jackie aolewe na JB. Celine anamwambia Imelda anajua kuwa Jackie yuko hai. Akina Davides wanaiona sherehe ya Jackie kwenye TV. Eli anaichoma kadi ya JB, lakini anashindwa kuchoma picha ya Jackie.ndani ya miezi mingine sita, Eli anajiendeleza kimasomo kwa msaada wa Mang Oca.

Fidel na Jackie wanatafuta matibabu huko US, JB anaungana nao; wakati Celine naye yuko huko Amsterdam.

Ukirudi Manila, Jackie anatamani kuanza biashara. Mang Oca anahasira pale anapogundua kuwa kidani cha Eli kimepotea. Jackie anamtafuta mama yake na anashtushwa na kile anachokipata. Huu ni mwanzo tunaomba maoni yake je unahitaji muendelezo wa tamhilia hii?…

No comments: