Saturday, June 28, 2008

MISS ILALA 2008

KIPUSA CHA ILALA

Usiku wa kuamkia leo wadau wa mambo ya Ulibwende walifurika ndani ya Ukumbi wa City Garden, Gerezani Jijini Dar es Salaam, kushuhudia mpambano wa kumsaka Miss Ilala 2008, ambapo Sylvia Mashuda aliibuka kidedea na kulitwaa Taji hilo. Pichani Miss Ilala Sylvia Mashuda, (katikati) akipunga mkono kwa furaha baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Miss Ilala katika mpambano mkali uliofanyika usiku wa kuamkia leo, kwenye Ukumbi wa City Garden, uliopo Gerezani jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa pili Nelly Kamwelu na mwingine ni Aneth John.

No comments: