Tuesday, July 1, 2008

TIGO, YAIPA BIG UP GLOBAL PUBLISHERS.

Kampuni ya Simu ya mikononi ya Tigo imesema kuwa itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Global Publishers & General Enterprises inayojihusisha na uchapishaji wa magazeti pendwa ya Ijumaa , Risasi, Uwazi, Amani, S&C Magazine na The Bongo Sun.

Akizungumza katika ofisi za Global Publisher's zilizopo Bamaga Sinza Jijini Dar es Salaaml leo mara baada ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo, Meneja Masoko wa tiGo Bw. Kelvin Twisa, alisema kuwa uhusiano wa kiabiashara uliopo baina ya makampuni hayo umeleta ufanisi zaidi na kwamba utaimarishwa ili kuleta tija zaidi.


Aidha, Twisa alisifu magazeti yanayochapishwa na Global Publishers kuwa ni magazeti pendwa yanayosomwa na jamii kubwa hivyo yanaweza kuleta tija zaidi kwa kutangaza biashara katika vyombo hivyo. "Jamii kubwa inapenda kuyasoma magazeti haya. Ni magazeti ambayo yanakubalika. Nililigundua hilo hata kabla ya kujiunga na Kampuni ya tiGo na nilipofika tiGo nilishauri tutangaze biashara yetu kupitia magazei haya na kumekuwa na ufanisi mkubwa kibiashara, " alieleza Twisa.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Bw. Eric Shigongo alisifu uhusiano mwema uliopo baina ya kampuni yake na tiGO na kueleza kuwa ni wa kujivunia. "Tumekuwa tukishirikiana na Tigo kwa kipindi kirefu na tutaendelea kushirikiana nao katika nyanja nzima ya biashara. Ninajivunia sana kushirikiana na tiGo," alieleza Shigongo.

Naye Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema kuwa kampuni yake imezidi kukua siku hadi siku ambapo awali ilikuwa ikichapisha gazeti moja tu la Uwazi lakini sasa ina magazeti sita ambayo hutolewa kila siku isipokuwa Jumapili tu. Pichani Meneja Masoko wa tiGo Kelvin Twisa (Kushoto) aliyetembelea ofisi za Global Publishers leo hii akibadilishana mawazo na mwenyeji wake Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Abdallah Mrisho katika ofisi zake zilizopo Bamaga Jijini Dar es Salaam.

No comments: