Monday, July 7, 2008

NEVER SAY GOOD BY


NDUGU MSOMAJI FUATILIA TAMTHILI HII YA KUSISIMUA

Huu ni mwanzo wa Tamthilia hii ya kusisimua inaitwa Never Say Goodbye bila shaka walio wengi wameangalia katika televisheni yetu ya Taifa(TBC1) hivyo kitu hiki kitakuwa si kigeni kwenu. Karibuni katika uandishi wa mfululizo wa Tamthilia hizi.


Mwanaume anaweza kumpenda mwanamke mmoja mara kwa mara, bila ya kutambua ni yule yule wa awali? hii inawezekana kama mapenzi yale ni ya kweli kwa mwanamke huyo, na hasa mwanamke kama atajitengeneza na kuwa na sura tofauti tofauti ili mradi akitaka kulipiza kisasi kwa wale watu waliowahi kumuumiza kipindi cha nyuma.


Hii ni stori nzuri ambayo haiwezi kusahaulika. Stori ya mwanamke mdogo, aliyesalitiwa na kutelekezwa, ambaye baadae miaka ya mbele anakuja kutaka kulipiza kwa mambo mabaya aliyofanyiwa. Maki na Juan Francisco wanakutana wakiwa katika umri mdogo, pale walipokuja kutafuta pesa katika Benki ya kijiji nje ya mji maeneo ya mto wa Orinoco. Vijana hawa wanazidiwa na mapenzi na kujikuta wakipendana na kuwa pamoja, Maki anakuwa ni mpenzi wa Juan Francisco.


Ingawa Juan anampenda Maki kikweli kweli, lakini Juan Francisco anaficha ukweli kwamba kuna mtu mwingine amemposa.Kwa kudanganywa na baba mkwe wake, Juan Francisco anarudi katika maisha yake ya nyuma na kumuahidi Maki kuwa atarudi: " Kamwe sitosema kwaheri". Lakini muda ukaenda bila ya Maki kumuona, na kwa wakati huo huo akapata mtoto wa kike.


Wakati akimuona Juan Francisco kwa mara nyingine tayari ameshamuoa Fanny na walikuwa wamekuja kumchukua Florcita, mtoto wake, kutokana na familia ya Fanny kuwa na roho ya kikatili, wanamuingiza Maki katika uhalifu na kujikuta amewekwa jela bila Maki kutarajia.Kutokana na mshtuko aliokuwa nao na upekee, Maki akaamua kuendelea na maisha yake mwenyewe... wakati anaendelea kuhangaikia mipango mingine, akasaidiwa na Ricardo, mwandishi wa habari ambaye ni muigizaji ambaye atamsaidia katika maisha yake ya baadae.


Kwa msaada wake, Maki akatumia mwanya huo kupanga mpango wa kulipiza kisasi kwa wale waliomtia matatizoni na kuhakikisha anampata binti yake wa kumzaa. Kila mmoja alikuwa akijua kuwa Maki amefariki lakini alijitokeza kwa jina la Soraya, wakati mwingine Campanita na Consuela, majina matatu tofauti yaliyouchemsha vilivyo moyo wa Juan Francisco na kuuchanganya kwa sababu nia yake ilikuwa ni kumpenda Maki tu, na mtu ambaye angeubadili moyo wake.Je Juan Francisco atamgundua Maki kwa mchezo wake huo?
Anza kufatilia tamthilia ya kusisimua…

Siku ya kwanza ya mchezo tunaona kijiji chenye giza nene huko Peru– na mila zao,za kucheza muziki na burudani mbalimbali. Carlitos anafanya kila njia ya kumpata mwanaume mwingine na kusherehekea ushindi. Anamtania Maki, anasema kama atashinda atacheza naye. Kwa shingo upande anakubali kumuweka chini kwa kuchukua ushindi. Shahidi anatoa sauti kwa kilugha chao akiashiria mchezo umeanza, "Gano la machona!" Maki anamgonga mwanaume aliyekuwa akishindana naye. Watu wanampigia kelele, "Maki, Maki!


Juan Francisco anauliza kinachoweza kutokea kuwa biashara ya familia, anaunganisha maongezi hayo na dola 12,000 kupata chanzo cha safari yake, lakini anajikuta amegombana na Raul, wakati mpenzi wa Juan Francisco, Fanny,akiunga mkono ugomvi ule. Fanny anampigia simu Raul "primo" (anasema ukweli kwamba, ni kweli ni binamu yake), lakini pale inaonekana kuna kitu kati yao kinaendelea.


Kwa upande wake, wakati Juan Francisco anaongea na baba wa Fanny, Fanny anamshawishi Raul kwenda mbali,Raul naye anasema kwa ajili yake atafanya anavyotaka.Baba wa Fanny anakubaliana na Juan Francisco, Raul anakubali kuendelea na safari yake ya biashara.


Raul anampatia J.F. picha ya Agatha, mwanamitindo ambaye atakuwa kiongozi katika biashara ya urembo. J.F.anagomba na kusema, Agatha ni "muy friar" na anataka mtu ambaye amesomea kazi hiyo. Raul anatumia madaraka yake – wanagombana, lakini Raul hasemi hapana kama ndio jibu, baba yake anampa J.F. neno la mwisho kufanya kazi na Agatha. Baba yake mwisho anamuomba Raul kuungana nao katika chakula cha mchana kumpokea J.F. katika familia. Raul akajibu kuwa hawezi kufanya hivyo, kwamba ana miadi muhimu ya kibiashara mchana huo. Raul na baba yake wakaondoka, Fanny akamhakikishia J.F. kila kitu kitakuwa sawa.


Muda mfupi kabla Raul akamshangaza Fanny, ambaye alikuja nje ya chumba chake, akijaribu kushea penzi na Fanny, ambaye alikataa kuwa naye. Raul anasema kuwa anaweza kuolewa na J.F., lakini anaweza kuwa wake wakati wowote.Akamwambia aondoke, akasema kuwa J.F.anaweza kufika wakati wowote, ambaye alifika kweli, Raul akaondoka baada ya kumuona. J.F.anauliza viatu vya Raul vilikuwa vikifuata nini pale, Fanny akasema kuwa baba yake alikuja na viatu vile akaviacha pale.


Muda mchache baadae, kwenye meza, anakula chakula cha kumkaribisha J.F. kwenye familia, mama wa Fanny, Esther, anamuuliza J.F. kuhusiana na matarajio yake ya safari. Nje, mtumishi mdogo anamwambia Raul (ambaye anakumbuka jinsi Fanny alivyokataa kuendelea ) wanakula chakula cha mchana pamoja baadae anasema kuwa hatokula chakula hicho na familia. Kisha akampigia kelele kijakazi mdogo, akaongea maneno fulani ya kilugha Raul anaongea yeye mwenyewe "Fanny, utakuwa wa kwangu,haijalishi itachukua muda gani."


J.F. anafika hotelini anasema kuwa atakuwa pale kwa wiki mbili na msichana anayefanya kazi pale (Marina) anatokea na kugongana naye. Kanisani, Carlitos anamwambia mchungaji jinsi alivyokuwa mbaya na kununua msichana, kisha anamwambia kuwa anampenda Maki, mchungaji hakufurahishwa na jambo hilo. Akaendelea kuelezea habari za msichana huyo,mchungaji anamwambia inatosha." Mchungaji anakubali kumuandikia barua kwa ajili ya Maki.


Marina anakutana na J.F. anapokuwa anaondoka baada ya kupata chakula cha mchana(ndani ya boti dogo) akajaribu kuungana naye, lakini J.F. anaamua kuondoka peke yake. Baada ya kutembea ndani ya maji, akajivuta bichi. Maki yuko sehemu nyingine bichi, akamuacha ndani ya boti akiwa na dereva, Carlitos, huko bichi,anataka kuondoka. Anataka kubusiwa.anamwambia afumbe macho yake kisha anaondoka bila ya kumpa chochote. Wakiwa wanatembea, J.F. akamchafua usoni kisha kwa haraka sana akaanza kumpiga picha. akisema"Que maravillosa mujer" kisha akaanza kumpiga picha. Kwenye mkondo wa maji, pale alipokuwa akijipakaa mafuta.


Carlitos anarudi kwenye boti yake kanisani na kupata barua kutoka kwa padre, wakati Maki mazoezi. Akamjaribu J.F.kwa kumpigia kelele za kumtisha baada ya kumchunguza akampiga kichwani mara moja. Anavutiwa na mchoro wake kisha anamuliza kuhusiana na mchoro huo, pia anakuwa mpole kwake. Anaangalia katika kichwa chake na kukisafisha ili asije akapata madhara. Akajaribu kumbusu akaonesha kama vile mwenye woga na hasira.


Wakati mwingine, Carlitos anaandika barua kwa mchungaji kwa mkono wake mwenyewe. J.F. anarudi la lancha. Carlitos anarudi katika boti yake kumpitia Maki pamoja na Juan Jayo. Maki, anatembea bichi, anamuona J.F. akizama chini kwa boti anaamua kuogelea ili kumuokoa, na kumrudisha bichi,kisha akachukua mwezi kurudi katika hali yake. Carlitos na J. J. wanawapeleka kwenye boti. Carlitos anadhani kwamba anambusu J.F., na mbali na wivu, anaanza kuwaacha. J. J. anaruka ndani ya maji na kuogelea akielekea bichi na kumsaidia J.F. Carlitos ambaye anasumbua ndani ya boti,anaanguka baada ya kusoma barua, anasema kama hatokuwa na Maki, hakuna atakayekuwa naye na ataona.


Wakamchukua J.F. kumrudisha ndani ya boti kwa bahati mbaya akaacha simu yake ufukweni. Carlitos, akapandwa na wivu na kukasirika, akampa wakati mgumu Maki, naye Maki akampa kitu anachokiona kinafaa kwake. Carlitos amebeba kamela ya J.F. aiifanyia mazoezi, and it turns out lather, he steals it.


Ukirudi Lima, Fanny anatembelea kwa mtengenezaji maarufu wa filamu (Don Humberto?) kutoka Los Angeles ambaye alitaka kukutana na J. F. kuongea naye kuhusiana na mpango wa kutengeneza filamu.


Katika zahanati ya matibabu, J.F.anawaambia watatu kati yao kuwa amejigonga kichwa chake katika boti na jinsi alivyojipiga na kupoteza fahamu na jinsi Maki alivyookoa maisha yake. Carlitos bado ana hasira na yeye. J.J. anampatia J.F. lifti ya kurudi hotelini. Marina anamuuliza J.J. kitu gani kilichotokea kwani alikuwa akijilazimisha kwa Maki , "anajiachia" anaingiliwa na J.F. akajisemea kuwa hatomuachia mtu kuwa na J.F.


Carlitos anatoa mkanda kutoka kwenye kamela aliyotoka nayo kwenye boti. Anaona picha za J.F alizopiga akiwa uchi .anachuju za Maki, na kusema kuwa usiku huo atafanya kitu ambacho Maki hatokisahau.


Maki anamlipa mtu chakula cha usiku, ambaye anasema kuwa ni nusu tu, kisha anamwambia kuwa anafanya kazi kwenye hotel na usiku huo anatarajia kupata pesa nyingi. Akatoa pesa kiasi kama chanzo kwa matumaini ya kulipa deni kwa njia hiyo, hata hivyo Maki akakataa na kumuacha akiwa na hasira.


Usiku ulipoangukia eneo la mji Maki akajiandaa kwa huko hotelini Shebang hotel. Carlitos akamwambia Maki, akimuone picha zake za utupu pale alipokuwa akiogelea. Maki akadai kuwa hakujua kama anachukua picha. Hata hakumuamini, akaonesha wivu wake kwa mara nyingine, akajaribu kumpumbaza na kumfukuza kitu ambacho kinauma.Akamwambia kwamba watu wote kijijini watamjua jinsi alivyo.Marina anajaribu kuongea na Carlitos mbali na kufanya hivyo, kisha mchungaji akamwambia kama atafanya hivyo atamvunjia heshma.


Marina,Maki na Carlitos, wanavaa nguo za kawaida, wanacheza shoo ya matangazo live. J.F. anaangalia anamkazia macho Maki. Baadae usiku, Marina anashangazwa na J.F.,ambaye anauliza kuhusu Maki, na kumsababishia Marina kuwa na wivu. Marina akasema kuwa atakuja kwenye chumba chake amechelewa baadae. Wakati Carlitos anacheza na Maki,akakataa kuendelea kucheza. Carlitos akapata hasira, akatoa tangazo kwa kila mtu, kisha akazitoa picha chafu za Maki kwenye wimbi la watu. J.F. akachanganyikiwa,akamuita Carlitos pembeni,akagongana naye na kumuangusha chini.


Baada ya Juan Francisco kumgonga Carlitos, grasi ikavunjika na vipande vikasambaa hotelini kila kona.


Maki akakimbia nje ya hoteli na J.F. akamkimbiza. Akaenda nyumbani na J.F. akataka aingie ndani ili wajadiri picha hizo, akaelezea ni wapi alipiga kisha akamuomba msamaha.Amwambia kuwa hatokaa akamsamehe na kumwambia akae mbali naye milele. Akakaa nje na kusema kuwa hawezi kuondoka sasa hivi." Akazunguka kisha akaondoka zake.


J.F., akarudi hotelini, akapaya simu kutoka kwa Fanny kuhusiana na Don Humberto Aragon akakutana naye akiwa na familia yake kwa ajili ya chakula cha mchana." Aliporudi nyumbani kwake, chumbani kwake, Maki akafungua picha yake ya kasuku ambayo aliichora kwenye maji ya mtiririko ambayo alimpatia J.F. kama zawadi , lakini aliitaka irudi. Kwenye picha, ameandika never say good by."


J.F. anarudi nyumbani kwake Lima, anasalimiwa na mama yake. Anaongea na mdogo wake, Angie, na kumwambia kuhusiana na "un milandro" ambaye anamjibu kuwa yeye si milandro, jina lake ni Juan Rufian naye akasema kuwa ana dada yake ambaye ni mwanamitindo ambaye huwa anatamani kupata kazi kwa J.F lakini yeye alimwambia kuwa hawezi kupata kazi kwake bila kulala naye. Angie anamwambia awe makini, kwasababu Fanny ni mtu ambaye ana wivu.
Fanny anamwambia mama yake kuwa anampenda J.F., wanashea mipango yao, kwamba anamsaidia J.F. kupata project ya mikanda na kwamba atamuoa na kama hawezi, there will be "no pellicle".mama yake akaonekana kufurahishwa na wazo.


Marina anamwambia Maki asifanye chochote na mwanaume kama J.F., baadae J.J. (Juan Jayo) akakimbia, akarudisha ujumbe ambao J.F. alimwambia alipompigia simu kutoka Lima, akisema ni muhimu sana, pia akampa kipande cha karatasi akaandika namba yake. Padre Higinio anakuja na Carlitos, mchungaji anamlazimisha Carlitos kukaa chini ya magoti yake na kuomba msamaha kwa Maki kwa kile alichofanya hotelini na akaomba aendelee kufanya kazi na yeye kwenye la lancha.Maki kwa bahati mbaya akakutana na kipande cha karatasi cha namba ya simu ya J.F Marina anayeonesha kuwa na furaha anatokea.


Aliporudi Lima, J.F. akaelezea kwa Fanny jinsi alivyojigonga kwenye kichwa chake na kumwambia jinsi alivyopoteza camera yake (hata hivyo hakumtaja Maki). Marina anarudi kwenye hoteli na kupiga simu ya Lima na kuongea na mama wa J.F, anayesema ameenda kwenye chakula cha mchana, na akasema atakuja baadae.


Don Humberto, anakutana na J.F. na familia ya Fanny, akaelezea yaliyokuwemo kwenye mkanda, kwamba yanaweza kuanza mwezi wa pili au wa kwanza, wanaweza kufanikisha kwa mwenzi wa 8 na wa 12, bajeti itaghalimu shilingi dola milioni, etc. Wakakubaliana kwenye asilimia 50 na kupeana mkataba, kisha Saul akawa kama meneja mkuu kwenye film, akaweka wazi kwa baba yake Fanny ambaye aliwashtua Fanny na J.F., kutokana na Saul na J.F. kuwa maadui.
Kisha, peke yake, Fanny anamwambia J.F. anataka kuolewa naye na kusisitiza wataoana hivi karibuni na kwamba wataenda kwenye kundi ambapo Fanny anaangaikia rizki ili kutangaza kuwa wataoana hivi karibuni kwasababu chanzo cha biashara tayari., kutokana na woga kwa shingo upande anakubariana na hilo, Saul anaonekana kushtushwa na tangazo hilo.


Baadae, J.F., Fanny na mama yake wanakwenda pub, ambapo Leopoldo, baba wa J.F. anapiga gitaa la maana, pia wanamtangazia( pale alipopata mapumziko ya kupiga gitaa na kwenda kwenye meza yao, ndio wakamwambia kuwa wanaoana,hivyo Leopoldo akaagiza shampaini bora ili washerehekee. Mhudumu akamwambia J.F. amepata simu kutoka kwa Sauce, Fanny kwa mara ya kwanza akaonesha kushangaa, ndipo J.F.akaomba udhuru kujua itakuwa ni nani ambaye amepiga simu pale baa, japo ilikuwa ni karibu na usiku wa manane. Alijipa matumaini huenda akawa ni Maki, kwa niaba ya Marina, ambaye alisema Maki amemlazimisha, wakaanza maongezi mafupi, akiuliza kuhusu kazi zake, baadae Fanny akaja na kumuingilia J.F., naye J.F. kwa haraka akajifanya anaongea na mwanaume na kufanya mawasiliano na line ya uongo,na kumuacha hewani, infuriating Marina on the other end of the line.


Aliporudi mezani J.F.akachukua simu yake na kuipiga ,Fanny, akaanza kumshambulia akimlaumu. Akampigia Ramon kupanga mipango ya kukaa tayari kwa ajili ya kurudi Sauce kesho yake. Fanny,anapata hisia, akijiuliza kuhusiana na mpango wake wa kurudi Sauce, na kutangaza kuwa atakutana naye pale, na J.F. anachanganyikiwa pale alipomuangalia usoni baada ya kumwambia vile.


Siku inayofuata asubuhi, J.F. na Ramon wanafanya kazi nje na safari yao ndani ya mji wa Sauce, Fanny naye anakuja , anadai kuwa atokwenda Sauce pamoja na yeye, kama alivyokuwa akisafiri na Don Humberto kwenda Los Angeles kufanya kazi ya kuchukua taarifa za pellicle.


Kurudi Sauce kwecha chakula cha mchana ufukweni, J.J. anamuonesha Maki jinsi ya kunywa kinywaji kwenye chupa, anamtakia mema, akamalizia kunywa mpaka mwisho kisha akatupa kwenye maji. Carlitos anampatia J.F. camera kumpelekea Maki, anasema kuwa anahisi angerudi. Maki anasema sio yeye, lakini anakubaliana hilo. Ramon na J.F. wanaangalia ndani ya hoteli, alipoenda chini ya maji J.F.akakuta chupa ambayo Maki aliirusha na kumuelezea nje akaelezea kwa Ramon jinsi watu wanavyofanya ili kutimiza ndoto zao lakini zao zimetupwa kwenye maji. Maki akamchafua, wakabadirishana macho kila mmoja, wakagundua mapenzi yao kwa kila mmoja.


Maki anarudisha kamera kwa J.F. na anamshukuru yeye pamoja na Carlitos. Akaomba msamaha kwa kila mmoja kwa kupiga picha za uchi za Maki, akasema kuwa ni yeye aliyesababisha na alikuwa ameleweshwa na kuomba msamaha. Kisha akamuomba Maki kwa misaada miwili 1) ni kumkaribisha chakula cha mchana(mbele ya mlalamikaji Carlitos ili kumsababishia wivu. Na msaaha wa pili ni kufanya kazi na wao kama muongozaji ‘guide’, tokea alipojua eneo vizuri. Baada ya kuwa mkaidi na kuomba msamaha, mwisho akakubali baada ya kuambiwa na J.J. kisha , J.F. akamwambia Maki akamkumbusha mdogo wake, Angie.


Wakati huo huo. Tukirudi Lima, Angie anafanya mpango kwenye simu kukutana na muchacho kwa ajili ya wikiendi, na kwa niaba anamwambia jinsi anavyomuhisi mama yake kwamba ataenda kucheza na rafiki yake, Clarissa.


Wariporudi Sauce, Ramon akaongea na J.F. kuhusiana na jinsi alivyo ili kupata mwanamke mrembo na atakufa kwa ajili ya kuwa kwenye miguu yake lakini akauliza kama Maki atakuwa ni mdogo kwake. J.F. akasema jinsi alivyo na umri mkubwa, haijarishi . J.F.akasema yuko makini kwa Fanny na Ramon akamhakikishia, na hivi wanafanya kazi pamoja, hatomwambia Fanny kuhusiana na Maki, kisha akajisemea, " ni jinsi gani alivyo na furaha."


Ukirudi Lima, Saul akamkumbusha Fanny jinsi walivyojuana kwa kila mmoja na ilikuwa ni furaha pamoja na shangwe. Fanny akasema kwamba ilikuwa ni muda mrefu uliopita "criatura" kisha Saul, akamkimbiza kama kawaida yake na kumuuliza ni jinsi gani walikuwa na furaha Fanny akasema kuwa". Saul naye akamjibu kama alivyosema kisha akamwambia ilikuwa ni muda mrefu akaendelea kumchunguza akitaka kujua mambo yake, lakini Fanny akasema amechoshwa na mada hiyo kisha akamwambia kuwa anajua penzi lake kwa J.F.


Kurudi hotelini huko Sauce, Marina is flirting with Ramon, anamuuliza kama ni muigizaji, and seductively leads him up the stairs, with the owner of the hotel looking on from the check-in counter with total aggravation. J.F.anakuja nyumbani kwa Maki, kumpa maua. Maki anamuomba akae kimya kwani mama yake amelala, na kumuelezea kuwa mama yake ni mtu asiyeguswa kichwani. J.F.akasema kuwa atamwambia mama yake, kwasababu ana matatizo katika kichwa kama kawaida. J.F. anamwambia Maki jinsi alivyo mwepesi, lakini Maki anamwambia kuwa uhusiano huo utakuwa ni wa kazi anachotakiwa ni kumuheshimu na kumuuliza kama anakumbuka mara ya mwisho kilichotokea kwenye kichwa chake (akamkumbushia tukio lililotokea hapo nyuma.)


Huko Sauce, Maki anamuwekea Juan Francisco (J.F.) chakula cha mchana kwenye nyumba yake J.F. naye anakutana na mama yake Maki kwa mara ya kwanza na wakaonekana kupatana . kwa uwazi kabisa,mama wa Maki anamuwadha mume wake (baba wa Maki) bado yuko nao, na akaondoka na picha nzuri. Baada ya mama yake kusonga mbele, J.F.akaendelea kupata zaidi kupitia Maki, akamuuliza Maki kama anaamini kwa malengo, akasema baba yake alifanya. Akamuonesha barua yake iliyotoka kwa baba yake ambayo imefunguliwa na akampa moja afungue na baada ya kufungua akahisi ametokea kupenda kwa mara ya kwanza, moja afungue pale atakapofunga ndoa, na moja aifungue pale atakapopata mtoto wa kwanza. Pia wakaongea kuhusiana na dada yake J.F Angie na jinsi alivyo na umri mgumu. Maki akauliza Angie ana umri gani J.F. akasema kuwa Angie ni mtoto kama alivyo yeye. Maki akasema kuwa angependa kuwa rafiki wa Angie.


Wakati huo huo,wakarudi Lima Fanny anapofanyia kazi, akapanga mipango ya harusi na mama yake , ambaye ana mpango wa kuchora gauni lake la harusi na anapanga tarehe ya kufanya harusi hiyo ndani ya mwezi mmoja. Fanny na mama yake wanafurahia.


Huko Sauce, wakati Maki anachora picha ya , J.F. ambaye alimuomba Maki awe mwanamitindo kwasababu ya uzuri wake na kumuhakikishia kuwa atafanikiwa kuuteka mji wa Sauce. Maki akawa mbishi. J.F. anafanikiwa kumshinda na wanabusiana kwa mara ya kwanza. Maki anakubali kujaribu kuwa mwanamitindo wake, naye J.F. anamuonesha jinsi alivyoanza kuchukua picha zake.


Juan Jayo (J.J.), Carlitos, na Ramon wanaangukia kwa J.F. na Maki katika eneo ambalo J.F. na Maki wanafanya kazi. Carlitos hana furaha wakati wote na wivu wa kupindukia.Yuko tayari kuingia ndani ya boti na kuondoka baada ya wao kwenda mtoni. Hawawezi kukutana na mtu yoyote katika njiani kama radio na motor havijaanza kufanya kazi, hivyo basi wanashindwa kuendelea na boti kwenye mto wakati J.F. na Maki wanafanya kazi (zaidi ya kucheza ) pamoja, wanavyogombana kila mmoja mara kwa mara. Kunakuwa na matatizo kati ya Carlitos na J.J. kwenye boti yao. Mwisho, Maki anakuwa na wasiwasi na wao na kuwapigia kwenye radio na kuwaambia kuhusiana na tatizo na kwamba wako mbali, kuhusiana na muda kutoka sehemu waliyopo. Maki, anajua boti yake na kuwaelekeza wasichezee motor, kwa ajili hiyo wanatakiwa kuacha motor ikae kidogo kabla haijawashwa, na kama hiyo haitafanya kazi, wanatakiwa kusubiri kusaidiwa. Kutokana na kuchanganyikiwa,wanasubiri kwenye lancha wakati J.F. anaonekana anafurahia kukaa na Maki usiku wote peke yao. Akamwambia usiku huu atampenda kama mtu mwingine aliyempenda kabla.


Ndani ya nyumba ya makuti, wakiwa na dazeni ya mishumaa, J.F.akatoka kwa Maki, ambaye alisema kuwa ni mara ya kwanza. Asubuhi, Maki anaaamka mapema, na J.F.akauliza ni kwanini ana wasiwasi. Maki akaelezea woaga wake kuhusiana na kilichotokea naye J.F. akamhakikishia kwa upole na uwazi jinsi anavyomuheshimu wakajifungia na kukumbatiana kisha wakabusiana. Vijana watatu wadogo wanaamka, mwisho mashua ikaanza kufanya kazi wakarudi kumtafuta Maki na J.F. pale Maki na J.F.walipoingia ndani ya Carlitos akamwangalia Maki jicho baya Maki naye akamtema,akamwambia kuwa ana haki za kumfanyia hivyo baada ya kumuaibisha mbele za watu na kumdharirisha mji mzima, J.F. anamsindikiza Maki nyumbani na kumpa busu la kumuaga.


Mchungaji yuko nyumbani amekaa na mama yake Maki pale Maki aliporejea akamuuliza kuhusiana na "brillo" akamuangalia usoni,Maki akamwambia kuwa yuko kwenye mapenzi , padri alishangaa na kuendelea kumuuliza maswali zaidi kuhusiana na kufanya kazi na J.F., kwani anahisi huenda kuna kitu zaidi ya hicho alichosema, hivyo aliendelea kupeleleza na kufanikiwa kumpata Maki ambaye alikubali kuwa na uhusiano wa kimapenzi, "Fue mi primera vez". padre, akakasirika, akauliza kama hakumbuki kwamba aliongea kanisani. Anafikilia kuhusiana na kukuza uhusiano na kwamba Maki atapata maumivu kwenye penzi hilo. (inaonesha kama kuna mchezo Fulani unachezwa kwa Maki).


Tukirudi Lima, mama wa J.F., Lucila, anampigia Fanny simu asubuhi na mapema,ana wasiwasi na mtoto wake, Angie, ambaye hakuwahi kuonekana nyumbani ambapo alitakiwa kuwa usiku uliopita na J.F.akaangalia ujumbe wake, ambayo mke wake aliiacha kwa sauti nyembamba jinsi walivyooana, wakati J.F. siku zote ana ndoto kuhusiana na Maki. Akapata mesegi nyingine kutoka kwa Fanny, kwamba wana ugomvi mkubwa yeye na dada yake, Angie, hivyo anamuita Fanny arudi akasema kuwa, Juan Rufian, na akasema kuwa atarudi Lima haraka sana kushughulika na mambo ya maana. Kwa uhakika zaidi, Angie yuko na "malandro" a scruffy, squirrelly little squirt, who just can’t wait to show Angie "la camita".


Kurudi Sauce, Maki anavuta moja ya barua zake, moja wapo iliandikwa na baba yake ambayo alitakiwa kuifungua, pale alipoifungua akakuta penzi lake la kwanza. Akakaa kwenye kitanda,akaifugua na kuisoma, ndani ya barua hiyo baba yake akamwambia jinsi penzi zuri lilivyo, lakini akamuonya kwamba ndani ya penzi hilo pia kuna maumivu.


Carlitos anapata chakula mchana nje ya mlango pamoja na Marina (inaonekana kila mmoja ana wivu na mwenzake). Carlitos anamwambia jinsi alivyo na uhakika kwamba Maki na J.F. wako pamoja. Akaja na wazo kwamba–Marina bado ana namba ya familia ya akina J.F.huko Lima, Marina naye akakubali kuitumia kuuliza kama J.F. anaweza kuwa na mpenzi huko Lima.
Katika mchezo wa mwisho, J.F.anakwenda nyumbani kwa Maki kumwambia kwamba anarudi Lima. Maki ana wasiwasi na anahisi jambo Fulani, lakini J.F. anamhakikishia kwamba ana dharura anatakiwa kuhudhuria pamoja na dada yake baada ya kumaliza matatizo yao, atarudi. Maki, akaonekana mwenye kuumia na kukasirika, kwa ndani akasema , "Adios". J.F.naye akajibu, "No. Adios, no. Hasta pronto. Acuerdate que yo nunca te dire adios."

Juan Francisco,anarudi Lima na kukutana na Fanny. Anauliza alichokifanya kwenye safari yake ya mwisho kwenda Sauce, akasema anatafuta sehemu Fulani kwa ajiri ya filamu; hakuna kinachoshindikana, wakati ana furaha pale anapombusu Maki. Fanny anataka kupiga simu polisi kuhusiana na kupotea kwa dada yake, Angie, lakini Juanfra moja kwa moja anamuhisi Angie yuko na malandro, Juan Rusian (au Rufian), kwa muelekeo huo anarudi kwake. Akaja kwenye nafasi ya Juan Rusian na kumsukuma karibu, akamwambia akae mbali na dada yake na akamchukua Angie na kumpeleka mbali kujizuia labda anachokihitaji Maki ni kupata kaka mkubwa, ambaye atamuweka mbali!


Nyumbani kwa Fanny, waanakuwa na mpango wa kuanza kuwinda. Saul, anamtambulisha Agatha kwa Juanfra, na kusema Don Humberto ametoa oda kwamba Agatha atakuwa "protagonista" katika filamu inayokuja. Juanfra anampigia simu Don Humberto kwenye simu yake kuona kama ni kweli, Don Humberto anasema hapana , sio amri, hivyo Juanfra awasiliana na Saul, na Agatha anasema hana sehemu yoyote ya filam na kwenda mbali, kwa matatizo ya Sual. Fanny anamuuliza Juanfra ambaye atashiriki katika filamu na akasema mtu mmoja mwenye sura nyembamba,kama malaika mdogo, na mzuri kama mwenye sura mpya(kama kawaida yake akambusu Maki kwa mara nyingine).


Wakati mwingine, kutoka katika hotel ya Sauce,Marina na Carlitos pia hawana jambo zuri; Marina anampigia simu Fanny anapokea na kusema ni mpenzi wa Juanfra na kwamba hivi karibuni wataoana,Marina akashangaa na kuwa na furaha.


Aliporudi nyumbani kwa Maki, akaunguza barua aliyoandikiwa na baba yake, Marina akaingia, na kumwambia kwamba Juanfra si mtu mzuri kwake akampa habari mpya kwamba amepata habari mpya kuwa ana mpenzi mwingine na anatarajia kumuoa. Maki akataka kupiga simu Lima ili kupata ukweli. Marina akamwambia asubiri mpaka Juanfra arudi, na kumuuliza yeye pia. Maki anaogopa huenda asitokee tena.


Juanfra anamuaga Fanny, msichana ambaye alimpenda alipokuwa anaelekea Sauce. Pale walipokuwa wakipeana busu la kwaheli, Saul akawa anamuangalia Juanfra akiondoka, Saul anamwambia kuwa ni mkakamavu, lakini yule Jaunfra ni msaliti na anamwambia afungue macho yake kwani bado hajachelewa kurudi kwake. Anamjibu kuwa asirudie maneno yake tena.


Huko Sauce, Marina anakesha usiku mzima na Ramon chumbani kwake, akiwa amekaa katika kitanda chake,ambacho kimefunikwa na shuka, Marina, anaingizia maneno na kumwambia kuhusiana na Fanny, pia anamuuliza Fanny ni nani kwake na akampata Ramon ambaye alielezea zaidi ya maelezo aliyotakiwa kutoa Juanfra anafanya kazi kwa ajiri ya biashara na kwamba yule Fanny ni mtoto katika ile familia, kwamba Fanny ni mpenzi wa Juanfra pia ni bosi wake akaanisha kuwa na ile familia ni familia ambayo haina shida. Pale Ramon alipoenda kuoga, Marina anaanza kusachi na kufanikiwa kupata kitabu cha anwani na kupakaa rangi ya mdomo katika adresi ya Juanfra na Fanny ya huko Lima.


Ukirudi Lima, Saul anakutana na Fanny kwa ajiri ya kurudisha barua zote za mapenzi alizowahi kumuandikia miaka iliyopita. Kama alivyozihesabu,akamhakikishia kuwa zote ziko pale, Anasema unaweza kumuita mpenzi wake, lakini anataka kusoma zile barua kila usiku. Anasema kuwa haina maana, akasema kuwa alitakiwa kuzisoma na akampa ofa ya sigara. Kama alivyoweka uzio katika barua hizo mwisho akacheka, akiwaza yeye mwenyewe, " bado ninayo halisi." Alisema.


Huko Sauce, Maki kwa bahati mbaya anakimbilia kwa Ramon na Juanfra, ambaye alimpatia zawadi huko uwanja wa ndege, lakini ana hasira na yeye na kukataa kuifungua. Anataka kujua yale makosa, akaogopa kutoa majibu, akashindwa kutoa majibu yanayoeleweka. Mwisho aliporudi katika nyumba yake, akataka kujua kuhusiana na mpenzi wake, lakini Juanfra hakutaka kumpa jibu la moja kwa moja. Akamwambia kuwa anaweza kulipa pesa nzuri kwa ajiri yake, lakini hataki kufanya kazi kwake hata hivyo, na hataki pesa zake. Anaamua kwenda zake mbali, akisubiri kuujua ukweli.


Maki anakwenda hotelini kuongea na Marina akitaka kujua anayeseka ukweli na Marina naye anajiweka katika zambi kubwa, anajifanya kama ana hasira kuhusiana na hili kwa ajili ya Maki. Akajifanya kama analia, Akacheka baada ya kumaliza uongo wake. hivyo Maki anakwenda kumshauri padre huko iglesia, akimwambia kile alichokisema Marina, padre anamwambia kuwa anatakiwa kufungua macho yake, lakini yule Marina hakuwa na uhakika yeye mwenyewe.


Wakati mwingine, Marina, bado anatafuta mabaya zaidi anaandaa bahasha na kuweka picha mbaya ambayo Juanfra alichukua kwa Maki na kuipeleka kwa Fanny huko Lima. Uchunguzi wake unamwambia kuwa atafika kesho.


Huko kanisani, Maki anamuombea Virgin Mary, naye Juanfra anaonekana na anaamua kumwambia ukweli. Akauliza kama ni kweli ana mpenzi, na akasema kitu Fulani, kuhusiana na Maki akasema hawezi kumfatilia msichana ambaye unampenda. Akamuelezea mtu anayefanya naye kazi ni wa aina gani ni mtu mwenye pesa nyingi na ana binti wa kike jina lake ni Fanny na jinsi alianguka kimapenzi na amefanya mipango yote, lakini kwa hilo ana mapenzi mazito na Maki, ambaye hata hivyo hakununua habari. Akasema hawezi kuishi maisha ya huku na huku, na kwamba kile anachokifanya ni kibaya kwa Fanny. Juanfra anaendelea kuongea katika maongezi yake ya kimapenzi jinsi gani anavyompenda Maki. Mwisho anakubali kufanya kazi tena na yeye, lakini kazi tu, hivyo basi wakarudi kwenye boti, ambako Juanfra aliendelea kukua akiigiza kama hakuna kilichotokea, lakini Maki akabaki ana hasira na kusalitiwa. Juanfra mwisho akaamua kumpigia simu Fanny na kumwambia kuhusiana na Maki. Akampata Ramon ambaye alikubali kuwa mshauri wake, na wakaenda nyumbani kwa Maki usiku, ambako alimpata Ramon ajifanye kama shahidi kwamba alimpigia simu Fanny anaseme ukweli kuhusiana na yeye na Maki. Moja kwa moja anatafuta, maki ambaye hana hatia. It is obvious that Fanny still knows nothing of Maki.


Maki anakubali kufanya kazi tena na Francisco katika biashara zake huko Sauce. Wakati anajaribu kujenga uaminifu wake, Fanny anapiga simu yake,anaongelea mipango ya harusi, wakati Maki anamwangalia kwa kuhisi kitu Fulani kinaendelea na Francisco anaomba samahani kwamba kazi yake imeunganishwa na simu, kisha akampiga busu Maki.


Katika nyumba ya Maki usiku uliopita, mchungaji anawapa ushauri–padre anauliza ni lini harusi itaendelea –Francisco anakasema kuwa kuna kitu kimefanyika, ndani ya miezi sita.Padri kisha akawapa kihapo cha ndoa na kuhakikisha wanakuwa na mapenzi ya kweli, baada ya hapo Francisco akampatia pete Fanny. Baadae, Maki na Francisco wakapeana busu ambalo lilionesha kuwa wapendanao hao wana mapenzi makubwa.


Huko Lima, Saul anapokea bahasha yenye picha chafu kutoka kwa Marina huko Sauce ambazo Francisco alichukua kwa Maki. Akasubiri katika chumba cha Fanny na pale alipofika alichanganyikiwa baada ya kugundua kuwa yuko pale.akampatia bahasha, akamsababishia kuondoka chumbani, kisha akafungua bahasha hali iliyomshtua sana na kuhisi ugonjwa wa tumbo baada ya kuangalia zile picha.pale pia kukawa na ujumbe kutoka kwa Marina ukisema kuwa picha zile zinaelezea kile alichokuwa akikifanya Francisco huko Sauce.


Fanny, anakunywa kinywaji huku akiwa amechanganyikiwa,anaonesha picha kwa mama yake, ambaye alizichukua. Fanny anamwambia mama yake Esther kilichosababisha akaifanya harusi ikaribie ni kwasababu ana ujauzito wa Francisco, ingawa hakujua vizuri. Esther akafunga safari na kuelekea Sauce ambaye yeye mwenyewe aliona kuwa kuna ukweli juu ya mapenzi ya Francisco na Maki . Esther alipofika huko akaanza kuulizia kuhusiana na habari za Francisco na Maki, kitendo kilichoonesha kuwa mji mzima unazijua habari za watu hawa.


Baadae, wakiwa kazini, Maki anampatia Francisco saa pamoja na mkufu na kumwambia kuwa vilikuwa ni vya baba yake hivyo akamuomba afungue, ndani ya kwenye kidani hicho kuna picha ya Maki alipokuwa mdogo. Francisco anashindwa kukubali vitu vile kwani ni vitu muhimu ambavyo vinahitaji kuwekwa kwa uangalivu, lakini Maki anamsisitiza.


Esther anamuomba mtu ampeleke kwa Francisco ambako alienda kumsema Francisco na kumuuliza kuhusiana na picha za Maki na kuhusiana na umaarufu walionao jijini yeye na Maki kuwa ni wapenzi. Akasema kama hii itakuwa inaendelea, atatakiwa kuisahahu harusi yake Fanny ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwao. Francisco akakubali kuwa ni kweli. Esther anamkasirikia Francisco na kumfokea akitaka kujua kama Fanny anafahamu mahusiano yake na Maki, anasema hapana ndio mama yake anamwambia kuwa tayari ameshaziona picha. Francisco anataka kumwambia Fanny ukweli, kisha Esther anakamwambia kuwa Fanny ana ujauzito. Mama yake akamwambia kuwa akimwambia ukweli atamuua.


Huko Lima, Fanny anachanganyikiwa na kumeza dawa. Saul anajaribu kumsahaurisha, lakini anashindwa.anakwenda kitandani kisha Saul anampigia simu Ester. Anahesabu vidonge alivyokunywa kisha anahesabu muda na kudai kuwa zimebaki sekunde chache. Esther anamwambia Francisco, akichukua jukumu la moja kwa moja la sakata zima lilivyokuwa Fanny ni mtoto wa pekee ambaye ndio kila kitu kwake. Hakutaka Fanny atambue kamwe kuhusiana na uhusiano wake na Maki, kisha akamwambia kuwa anahitaji yeye ni kurudi Lima, na kwamba ataendelea kufanya filamu, lakini Saul atakuwa msimamizi wa mpangilio mzima wa filamu hasa hasa kile watakachokisema waigizaji,na wakati wowote atasafiri kwa ajili ya kuchukua matukio mbali kwa ajiri ya kuandaa makala, Fanny atatakiwa kumsindikiza.Fransisco akakubaliana na hilo wakati akiwa na ndoto za kuwa na Maki. Esther kisha akamlazimisha Francisco kukaa naye huko los Morichales, akimuweka ili asirudi kumuona Maki, ambaye alikuwa akimsubiri Francisco nyumbani kwake lakini hakutokea.


Francisco anarudi Lima, ambaye alihudhuria mkutano mkubwa kuhusiana na filamu inayokuja, ikitambulishwa na Fanny, pamoja na Don Marcos (baba yake Fanny), Don Humberto, Francisco, na Saul wakiwa wametulia kwa ajiri ya kile kinachotaka kutokea. Kima mmoja kati yao anasaini mkataba. Anayeanza kusaini anakuwa ni Francisco, anapata simu kutoka katika simu yake ya mkononi. Anaomba msamaha kwa kila mmoja ambaye amemuangusha kwa kisirisiri naye anakuwa ni Maki, ambaye alitaka kujua ni kwanini hakuonekana usiku bila ya kumuaga.


Francisco akamjaza samahani za kumwaga. Maki anataka kujua ni mwanamke gani alikuwa amemkabiri huku akimuita Malaya, Francisco akamwambia kuwa hakuwa na wazo juu ya mwanamke huyo na kudai kuwa huyo anaweza kuwa ni mmoja wa wafanya kazi wenzake. Hivi karibuni, Fanny akamkuta akiongea na msichana huyo na kumchukua kisha kupeleka kwenye mkutano, Maki akakasirika na kumwambia padre kwamba amemuweka hewani. Francisco mwisho akasaini mkataba, kitu ambacho kilimfurahisha Fanny.


Marina anamuonesha Maki ‘press release’ inayotangaza filamu, akamuonesha picha ya Juan Francisco akiwa na mpenzi wake, Fanny, na kwamba watafunga ndoa ya kanisani huko Lima mwezi huu, kitu ambacho kilimshua Maki.


Mwezi mmoja baadae huko Lima –kila mmoja anajiandaa kwa ajiri ya harusi, Maki anamchukua padri kumpeleka pale akijaribu kuvunja harusi. Akapiga simu ya Francisco dada yake Francisco, Angela akaipokea simu ile na kumwambia Maki wanakaribia kuoa.Maki aliyekuwa analia akisaidiwa na padre,kutafuta kanisa.Angela anamwambia kuwa wakimpata dereva anaweza kumpeleka pale, na kanisa lao linajulikana, hivyo wakachukua cab. Wakiwa njiani kwenda harusini, Maki akazimia. padre akaiongoza cab iwapeleke zahanati,ambako daktari alimpima na akasema kuwa inaonekana kama vile ameshtuliwa mishipa ya fahamu. Maki, kwa mara nyingine anatumia simu ya daktari kumpigia simu Francisco. Baada ya kumkosa kwa hasira akasema kuwa haitaji kumuona tena na kujiona mpumbavu baada ya kuliamini penzi lake!"
Francisco na Fanny wanaoana, kwa furaha ya kila mtu Fransisci na Fanny wanatangazwa kuwa mke na mume.


Ukirudi clinic, daktari anarudi na vipimo zaidi na kumtamkia Maki kuwa hivi karibuni ataitwa mama.
Baada ya sherehe kuisha, Angela na mama yake wanasikia ujumbe wa Maki kwa Francisco Angela anaamua kuufuta bila ya kumuachia Francisco ausikilize.


Badae, Don Marcos anataka kumjua msichana mwenye pesa anavyofanana, akasema kuwa ni msichana mzuri, anataka kujua kama ni mwanamitindo aliyebobea. Esther na Saul wanasema kuwa ni msichana wa kawaida tu kutokea huko Sauce. Francisco na Fanny wanarudi nyumbani kutoka katika fungate yao,Fanny naye akawa anajihisi mwenye kuchoka na kizunguzungu.


Francisco, akiwa pekee, anatoka na kuangalia saa yake kisha anaangalia picha ya Maki, Fanny akamuita kutoka katika chumba chake, kutokana na maumivi aliyokuwa nayo. Kama familia wakawa wanasubiria habari kutoka kwa daktari kuhusiana na ugonjwa wa Fanny ambaye alikuja na kudai kuwa amegundua Fanny amepoteza mtoto, familia yake ikaumia kwani ilionekana kama vile kuna kitu wamepoteza.


Wakati Francisco anamweleza Fanny, Maki, akiwa kanisani, anafungua barua aliyowahi kuandikiwa na baba yake kwamba pale atakapokuwa na mtoto wa kwanza.mbele ya mtoto wake Virgin Mary,akasoma kwa sauti barua hiyo. Ilikuwa ikisema " Kuwa na mtoto ni zawadi kubwa katika maisha, na kuongelea ilivyo zawadi kubwa, na inahitaji majukumu. Akamuomba Virgincita msaada wa kuwa baba na mama.


Saul anamwambia Esther kwamba Francisco ana saa ya Maki ikiwa na picha yake, mkufu mzuri wa saa hiyo. Fanny baadae anaiona saa na kumsema "Juanfra". Akasema uongo na kudai kuwa aliinunua saa hiyo huko Sauce. Akamuomba kuiona na kutaka kujua ni mtoto gani alikuwa katika picha hiyo,akasema kuwa hajui ni nani. Ndipo Fanny alipomuelezea kuhusiana na picha chafu, pamoja na siku ambazo alikuwa huko Sauce,alipata simu kutoka kwa Saul, ambaye alimwambia kuwa muigizaji katika pelicula ni mzuri na ndiye msichana wa huko Lima. Akajikuta akiwa na wivu na kumwambia Francisco alale katika chumba kingine kwa siku hiyo.


Mpelelezi Saul anaenda Sauce na kukutana na Marina,wakagonagana. Usiku ule na kupaegesha karibu na nyumba ya akina Maki, ambako alimwambia Saul kila kitu alichotaka kujua kuhusiana na Maki.akamwambia habari ya jinsi mama yake alivyopoteza fahamu,jinsi baba wa Maki alivyofariki miaka iliyopita,na kwamba alikuwa kiafanya kazi ndani ya bahari . akamwambia kuwa anavyomuona Maki, anaonekana kama ni mjamzito. Marina anazidi kuelezea jinsi alivyo mtoto wa Francisco ana jinsi Maki alivyolia mwezi mzima na kupoteza hamu baada ya Francisco kuondoka. Saul akafikilia yeye mwenyewe jinsi Francisco alivyoweza kumpatia mimba msichana Maki mwanamitindo wa kimataifa na jinsi anavyoweza kumsambaratisha kwa hayo machache aliyoyapata. Wakampanga kaka wa Marina, Carlitos,ambaye alikuwa amekunywa,na kumwambia kuhusiana na Maki pamoja na wivu aliokuwa nao juu ya Francisco.


Saul anampigia simu Esther na kumwambia habari za Maki kuwa ana ujauzito kati ya miezi mine au mitano na kwamba baba yake ni Jaun Francisco Moreno. Esther anataka kujua kama Francisco anajua,Saul anadai kuwa ni lazima atakuwa na mpango wa kurudi Sauce. Esther akawa anawadha jinsi mtoto wake alivyojiingiza katika matatizo.


Carlitos anamuomba Maki kumuomba msamaha,ambaye alifanya hivyo, kisha anafanya naye kazi kwa mara nyingine,lakini hakutaka kufanya kitu chochote na yeye kuhusiana na mapenzi.
Fanny anakunywa pombe kwa wingi,Saul anazidi kumpamba na kuchukua vidonge kwa ajiri ya mishipa, lakini mama yake anaumia na kusema "Mungu wangu, haina maana kuwa ni lazima utakunywa chupa zima ya pombe." Wakamtembelea mtaalamu wa magonjwa ‘gynecologist; ambaye alimwambia kwamba atakuwa na maumivu katika phalopian tube, lakini anao uwezo wa kupata ujauzito, hivyo ajaribu kuendelea kutafuta, na wanaweza kutumia ukaribu walionao lakini aendelee kutumia dawa ya mishipa. Fanny anahisi kuwa amesambaratika na kuisha, na bila ya kumpatia mtoto Francisco ndoa yao itakuwa imeharibikiwa.


Huko Sauce, Maki mwisho anaenda leba kujifungua. Juan Jayo na mwanaume mwingine wanamsaidia kupata mtoto wa kike wakati huo Carlitos,akiangalia na kupata mshtuko wa nguvu na kutembea kisha akisema kuwa ni mtoto wa shetani.


Miezi miwili baadae, nyumbani kwa Maki mchungaji anatembelea. padre anampatia Maki ujumbe kutoka Lima kuwa wamefurahishwa na kazi yake baada ya kumuona kwenye soko la filamu. Mchungaji anauliza kama anaweza kuwa ni Francisco,na Fanny akasema kuwa namba zao ni tofauti, na kwamba kwa sasa hana analoweza kufanya na mpenzi wake huyo wa zamani, kwamba ameamua kumlea Florcita yeye mwenyewe.


Wakati huo huo, Francisco anasoma maoni katika gazeti na Filamu yake inapata maoni mabaya.
Fanny anapata matumaini yake baada ya kuona hapati siku zake kwa mwezi huo. Saul anaingia katika chumba chake, anampatia kinywaji. Francisco anaingia ndani na kumfokea, akimwambia kuwa anajaribu kumuingiza Fanny katika pombe kali. Saul anasema kuwa Francisco anapoteza dola milioni nne katika filamu ambayo imefanya vibaya. Baada ya kumwambia hivyo wakabadirishana maneno ambapo Fanny alimuamuru Saul aondoke ambaye alimwambia kuwa ataenda kumwambia mama yake kati ya Francisco au (Saul) mmoja wao aondoke nyumbani kwao moja kwa moja au watafanya kazi kwa pamoja. Saul anamwambia aendelee kumuhifadhi Fransisco,lakini ndie yeye anayewapa wasichana ujauzito. Baada ya kusema maneno hayo akaondoka ndani ya chumba, Fanny akauliza, unasemaje.Francisco akaendelea kuandaa vitu vyake kwa ajili ya safari, Fanny akaonekana kuguswa na neno lile japo hakuwa na uhakika.


Maki anaenda kanisani kupiga simu Lima na kuongea na muandaaji wa filamu, anayeitwa Luis Lima, ambaye anataka aje Lima, kukutana naye ambaye atamlipia gharama zote. Akakubaliana na kufurahi lakini ahakikishe kuwa ana kitu ambacho atamuhusisha Juan Francisco, akamuakikishia kuwa hawezi.


Maki anaondoka kwa safari yake kubwa ya kuelekea Lima pamoja na mtoto wake, huku akisindikizwa na padre,wakati akimchunga Carlitos, pale alipokuwa akiwaangalia wakati wa kuondoka.


Marina anampigia simu Saul, akimpatia jina la "Papi", na kumpa habari za Maki kutembelea jijini Lima kwa ajiri ya kukutana na Luis. Saul anakwenda kuongea na Esther, na kumjaza habari zote alizopata kuwa Maki anatarajia kuja Lima katika mazungumzo ya wananchi ni kikao kimoja na kile anachotembelea Francisco.


Mwisho wa mchezo, Ramon anatoa habari kwa Francisco kwamba Luis Lima amemuomba kufanya projecti ya filamu yeye na mwanamitindo ambaye ni Maki. Francisco akashangaa baada ya kugundua kuwa Maki anakaa katika hoteli moja na yeye.

Fanny na Juan Francisco wanarudi kutoka katika fungate yao huko Greek Isles. Fanny ana furaha kwasababu ni mjamzito. Kisha anachanganyikiwa baada ya kupoteza mtoto wake. hata hivyo anagundua kitu kutoka kwa ‘gynecologist; kwamba mbegu za Francisco ziko salama: yeye ndie ana tatizo katika mrija wake, hivyo anabaki kujiuliza ni lini atafanikiwa kupata mtoto. Kupitia michezo yote miwili,anajaribu kutafuta ujauzito, akidhani anaujauzito kumbe si mjamzito,hiyo inamfanya alichukulie kwa umakini swala hilo.


Ramon anatoa habari kwa Francisco kwamba ameombwa kuwa mpiga picha wa projecti kwa muandaaji mmoja jina anaitwa Lima (Nafikili hilo lilikuwa ni jina lake). Habari mbaya kwake ilikuwa ni mwanamitindo anayekuja kufanya projecti hiyo alikuwa ni Maki. Na kwamba amempatia mahitaji yote ikiwa ni pamoja na kumlipia pesa za safari dola 1,000 kwa ajili ya kuingia katika jiji la Lima kukutana na muandaaji huyo na kwamba atafikia katika hoteli sawa na Francisco na Ramon. Muandaaji huyo alimuona Maki kwenye mashindano ya urembo ambayo yaliandaliwa na Francisco alipokuwa muandaaji huko Sauce katika Casa Paris,na yeye pamoja na wengine wamevutiwa na mwanamitindo huyo. Mwanamitindo huyo amekuja hotelini pamoja na padre na mtoto wake wa mwezi mmoja. Ramon pia akatoa habari kwa Francisco kuwa Maki ana mtoto mdogo,anayekadiliwa kuwa na umri wa miezi miwili.


padre anamsisitiza Maki kununua nguo nzuri, kisha akaenda kukutana na muandaaji kwa ajili ya chakula cha usiku katika jiji kubwa. Muandaaji huyo anamchangamkia Maki sana kutokana na uchangamfu wake. Francisco anawaangalia vile wanavyokula kwa wivu wake anajaribu kuongea na Maki baadhi ya mambo lakini Maki hakutaka kuwa naye karibu kwa chochote. Anamwambia kuwa anaye mwanaume anaishi naye, kwa kupata ukweli kabisa akataka kwenda kukutana na huyo mwanaume na kugundua kuwa ni yule padre. Francisco anajaribu kumbusu moja kwa moja, lakini anakimbia. Hivyo anaomba msamaha, akajikuta akipandwa na wivu. baadae, akakutana na muandaaji, ambaye alimtaka Maki akae kihasara hasara lakini alikataa, na akatafuta muelekeo mwingine ambapo alitafuta sababu nyingine ya kumfanya akae hivyo alivyotaka.


Francisco amechanganyikiwa kwasababu kazi yake imekuwa mbaya. (baadae anagundua kuwa ni bora angeishi na mwanamke maskini wa kijijini, na kumuendeleza akawa mwanamitindo maarufu kuliko kumuoa Fanny kwa ajili ya pesa za familia yake.


Wakati huo huo Fanny anajaribu kutafuta mtoto kwa nguvu zote lakini hafanikiwi. Unywaji wake unamsababishia mambo mabaya zaidi. Anampigia simu Francisco hotelini awe upande wake, lakini anakataa, kutokana na mambo yake muhimu kwa ajili ya Maki. Francisco mwisho anarudi nyumbani na kumkuta Esther, mama wa Fanny, ambaye anamkaribisha kwa maneno makali akimwelezea jinsi Fanny anavyomuhitaji kwa sasa.


Esther, mama wa Fanny, anagundua kitu kutoka kwa Saul, ambaye amepata habari kutoka kwa mtu wake wa karibu, Marina kutoka huko Sauce, kwamba Maki amekuja Lima kukubali kazi aliyopewa na kwamba amekuja na mtoto wake mdogo. Esther anajisikia anajihisi kuogopa baada ya kusikia hivyo na kujikuta akimuonea huruma binti yake, na kuofia kwamba Francisco na Maki wataungana, na kumuagiza Saul ahakikishe wawili hao wanapotea (wawili hao ni Maki na mtoto wake). Baada ya kufanya hayo, Saul atatangazwa kuwa makamu wa raisi wa familia katika kampuni, kitu ambacho Fanny hakitaki pale atakaposikia. Saul anasema kuwa anaweza kutafuta njia ili kumuweka Maki jela kwa kumuundia njama ya dawa za kulevya pamoja na ukahaba, lakini ili kufanya haraka, anahitaji pesa nyingi. Esther anasema kuwa hakuna matatizo atamuwezesha ili aweze kufanikisha.


Saul anaenda Sauce kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo na kuungana na watu wengine wawili, Marina na kaka yake,Carlitos,katika mpango huo ambao anawaahidi kuwalipa vizuri.wanapanga aidha wamuue Maki na mtoto wake au wampangie njama ya dawa za kulevya ambayo ni rahisi. Carlitos anafanikiwa kupata begi la dawa za kulevya ambalo analipeleka katika nyumba ya Maki. Pale Maki aliporudi nyumbani katika kijiji cha Sauce, tayari dawa zilikuwa zimeshapandikizwa. Watu watatu wakawa wanaangalia kwa mbali nyumba ile wakati Marina akipiga simu polisi, na kuwaambia kuna kitu kibaya ndani ya nyumba. Polisi hao wakatokea na kukuta cocaine kisha wakaanza kumkamata Maki.


Wakati polisi wanamchukua Maki kwa tuhuma zake nje ya nyumba, mama wa Maki anamuangalia mtoto ambaye alikuwa amelala chini ndipo moto ulipoanza kuteketeza nyumba. Juan Jayo anakimbia kwenda kumuokoa mtoto, lakini polisi hamuachii Maki aondoke, hivyo wanamsukuma Juan Jayo ambaye anaenda kumuona mama yake aliyeko nje ya nyumba inayoungua moto, mchezo mwingine unamuonesha akiwa amelala hospitali kitandani, akiwa amefungwa na bandeji akionekana kama mwanamke aliyeunguzwa na moto mkali. Mchungaji yuko upande wake wakati wote. Maki anachanganyikiwa iwapo mama yake atafariki. Cha kwanza hawezi kuachia kitu kile kitokee kwa mtoto wake, lakini baadae inajulikana kuwa Juan Jayo amemkinga salama.


Francisco mapema mno anajaribu kufanya mawasiliano na Padre, ambaye alimpa ushirikiano mdogo, lakini kutokana na baadhi ya maneno padri anapata uhakika kuwa Maki ana mtoto mdogo na Francisco ndio baba wa mtoto. Baadae, Francisco anapiga simu hotelini kuongea na Marina, lakini anaongea na msichana mwingine badala yake ( hakuwa na uhakika wa jina lake). Anamwambia Francisco habari mbaya,Francisco anaamua kwenda Sauce.


Francisco anampata mama yake kabla hawajaenda Sauce anaahirisha chakula chake cha usiku na Fanny usiku wa siku hiyo.analazimika kutunga uongo kwamba kuna tatizo limemtokea mama yake katika familia yao, lakini kutokana na kuchanganyikiwa kwa Fanny hatokubali.Baadae, Fanny anawasikia Saul na Esther wakiongea na kugundua kuwa kuna kitu kinaendelea. Mwisho,
Francisco na mama yake wanaenda Sauce kumtembelea Maki. Anambeba mtoto kwanza, ambaye padre alimhakikishia kuwa ni mtoto wake. Francisco anafurahishwa na mtoto mdogo.Mwanasheria analipwa na watu wa kijijini ili kumuokoa Maki kwenye kesi.


Francisco mwisho anaenda kumtembelea Maki kwenye chumba cha hospital, na wakaomba msamaha kwa kila kitu. Akamtambulisha kwa mama yake, na ikakubarika kwamba mama wa Francisco atamlea mtoto mpaka afya ya Maki itakapokuwa nzuri na kesi ikishaisha. Maki akawapatia mtoto na hakusema maneno yoyote, inafurahisha, pale Francisco alipoondoka chumbani, hakusema kwaheri.


Usiku wa manane, Maki anakimbilia nje ya wodi na kutoroka.Anaenda katika nyumba yake iliyoungua na kusoma kwa mara ya pili barua aliyopewa na baba yake, ambayo alimwambia kuwa aisome pale atakapopata mtoto wake wa kwanza.


Akiwa nyumabani kwake baada ya kutoroka hospitali, Maki aliyekuwa ameungua vibaya sana na kuzungushiwa bandeji kwenye majeraha, anaandika katika picha ya marehemu baba yake maneno yasemayo hivi karibuni nitajiunga na wewe. Anachukua kipisi cha barua alichomuandikia kisha anaenda katika kishamba kidogo na kukizika chini, kisha anahakikisha hakionekani. Siku ya pili iliyofuata, mvulana aliyekuwa akivua samaki aliyekuwa juu ya daraja anamuona pale alipokuwa akifukia kijibarua kile na kumfatilia ambaye aligundua mtu yule alikuwa ni Maki.Anakimbilia kijijini kutoa habari kwamba Maki ameonekana. Muda kidogo mwanaume aliyevaa Magamba aliyekuwa na safari yake anamuona Maki kwenye daraja lilelile, anarukia ndani ya maji , kisha anaogelea mpaka nchi kavu kuona kama Maki bado ni mzima au la, anapata msaada kutoka kwa, Jacko ( mwanaume ambaye anaweza kuongea lakini hawezi kusikia), ambaye alimtaka amsaidie kumtoa kwenye maji . kiboksi chake kidogo kikaanguka ndani ya maji.


Mwanaume ambaye baadae alikuja kugundua kuwa ni Ricardo, anampeleka Maki kwenye kijumba kidogo,ambako alimpatia huduma ikiwa ni pamoja na damu kwasababu alikuwa na damu sawa na yake.Anamfanyia usafi katika majeraha yake ya moto kisha anamfunga bandeji mpya.Maki anamuelezea kwamba kutokana na kuzidiwa na maisha aliamua kujiua mwenyewe. Hata hivyo baada ya Ricardo kumuokoa anamwambia kuwa kwa sasa hataki kufa tena.


Anamuelekeza Jacko kuingia chini ya boti. Wakati huo huo , kila mmoja akiwa na hamu ya kuamka , hasa Francisco, ambaye alikuwa akirudi kutoka Sauce. Anaungana na padre na kamishna wa polisi wanaenda kumtafuta Maki. Kijana huyo anawaonesha sehemu alipomuona Maki, na hakukuwa na dalili ya kuwepo pale, lakini wakakuta kibahasha kidogo cha barua kikiwa kimezama ndani ya maji.hata hivyo walihisi huenda ameenda sehemu kula. Kamishna anapiga simu kwa watafiti wote. Hata hivyo hawakufanikiwa kwani walichogundua ni kwamba atakuwa amefariki. Kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa na habari hizo hasa hasa padre.


Baada ya Maki kumwambia Ricardo, kila kitu kilichomtokea naye anamuelezea maisha yake na kwamba yeye ni mwandishi wa vitabu na alikuwa akiandika kitabu kuhusiana na eneo lile, na mbali na hilo pia amekuwa na miaka mitatu akisomea madawa pia ni muigizaji, ambaye amejichanganya katika mambo mengi. Maki anamuomba aende kumwambia padre kwamba yuko hai pamoja na Marina. Akidai kuwa ndio watu ambao wanaweza kumfichia siri yake na kwamba watakuwa na wasiwasi na yeye. Ricardo anakwenda kanisani kumfahamisha padri ambaye anapata nafuu baada ya kusikia habari hiyo. Padre anataka kufahamu ni kwanini Ricardo anamsaidia Maki, unyenyekevu huo utawashangaza wengi,ingawa anatakiwa kumsaidi na inavyoonekana ni lazima amsaidie tu.Anampatia Ricardo picha ya Maki, ambaye alichanganyikiwa kwa uzuri wake.Padre pia anampatia picha ya baba yake ambayo marehemu alimpa mwanaye,ambayo itamfurahisha kuwa nayo. Ricardo pia akaenda hotelini kumuona Marina, ambaye alimpatia habari za kuwepo kwa Maki, anamwambia kuwa yeye ni mwandishi wa kujitolea aliyeamua kumsaidia Maki, ambaye mwisho alidai kuwa padre anajua kuwa Maki yuko salama.


Carlitos ambaye anajuta anakwenda kwa mchungaji kukiri jinsi alivyochanganyikiwa, anakiri jinsi alivyopandikiza dawa za kulevya nyumbani kwa Maki.Padre alikuwa karibu yake, na kujikuta akishtushwa na habari hizo na kumshangaa kwa habari hiyo kitendo ambacho kinamaanisha hawezi kumwambia mtu yeyote mambo hayo. Carlitos anampa sababu ya kufanya hivyo padre, lakini anashindwa kuwataja washirika wake, Marina na Saul.


Siku iliyofuata, Ricardo anaaga kwa Jacko, na kwenda zake Germany, ambapo wiki mbili baadae, Maki anabadirishwa sura, yote hayo yanafanywa na Ricardo kwa kujitolea. Pale walipotoa bandeji, akaonekana mtu mwingine na mrembo zaidi. Ricardo mwisho anamfundisha jinsi ya kuishi na watu na kisha anampatia jina lingine la, "Soraya".Akawa na mipango mingi kwa akawa na mipango mingi juu yake, kwa haraka zaidi akawa mwanamitindo maarufu katika bara la Ulaya, na alikuwa akipamba juu ya magazine mbalimbali miongoni mwa Magazene za huko .

hivi ndivyo alivyoanza kuonesha muvi miaka sita mbeleni.


Baada ya Maki kujulikana kuwa amefariki, Francisco anarudi Lima, ambako Fanny alikuwa tayari kumpa taraka. Sasa akajua kuwa Maki amefariki na kumshukuru Saul, na kwamba Fransisco ni baba wa Maki. Hata hivyo akawa anaishi kwa kunywa pombe huku akiwa na presha kutokana na uwezo wake mdogo wa kushika ujauzito. Francisco anamfata na kumuomba msamaha na kumuahidi kuwa atokaa mbali naye tena. Anamuomba Fanny amkubali mtoto katika nyumba yao.mwisho, Fanny anakubali,lakini anaomba wasafiri kwa muda mrefu ili watakaporudi kila mmoja ajue kuwa ni mtoto wake wa kumzaa", Francisco anakubali mpango wa Fanny. Esther alikuwa akiheshimu matakwa ya Fanny, Lakini Fanny anamhakikishia kuwa hicho ndo anachotaka kufanya. Saul kwa hasira anamfokea Fanny kwa uamuzi wake, na hii inamsumbua sana, anaendelea na wazo lake juu ya Fanny.


Fanny anatokea kumpenda mtoto mpaka hapo anapofikisha umri wa miaka sita, Florcita ana miaka sita au saba hivi.


Soraya alitokea kuwa maarufu katika jamii , Ricardo anamuuliza iwapo atataka kurudi Peru, anasema anataka kurudi. Alikuwa na mipango mingi ya kuweka wazi kila kitu na kujulikana,lakini hakuweka kuweka wazi mipango yake yote,kasoro yake alikuwa akitaka Soraya alipize kisasi.mara ya kwanza,alitaka kumrudisha mtoto wake.Pindi atakapofika tu, akaenda kupaki pale alipomuona mtoto wake na alijua kuwa ni Florcita. Alifanya kioja kikubwa kisha analia kiasi cha kumuogopesha binti yake, ambaye kila alipokuwa akimuona anaogopa. Soraya aliamua vizuri kwani aliona kuwa haitopendeza katika familia na kwa binti yake kumchukua mtoto, kwasababu amekua akiwajua hao ndio wazazi wake na kwamba hamjui mama yake wa ukweli.


Ricardo na Soraya wanaishi na mmoja wa katibu muktasi wa Ricardo, Fabiola, mtu ambaye ni mgeni kwao. Alionekana kumfahamu Soraya kama mtu mwingine, lakini hakuweza kufahamu alikuwa ni nani. Pia alionesha wivu kwa Soraya na siku zote aliigiza kama mtu mgeni. Mwanzo alikuwa ndani ya gari na Soraya pia alioneshea kaburi la aliyekuwa mke wa kwanza wa Ricardo. Kitu ambacho Ricardo aliamua kukizima kwani alikuwa hataki kukiongelea, na kitendo hicho kilimfanya apandishe hasira, na kumnyamazisha Fabiola, kwa kuonyeshea kaburi la mke wake wa kwanza kwa Soraya.Anamuuliza kama alimueleza Soraya kilichotokea au alimwambia ilikuwa ni Ajali, Soraya anamwambia kuwa kati ya yote hayo hakuna kilichosemwa. Ricardo hivi karibuni anatangaza mipango ya kumuoa Soraya, Fabiola anamwambia kuwa amekasirishwa na habari hizo. Ricardo anamtishia kumrudisha kwa baba yake lakini anambembeleza asifanye hivyo.Wakaishia kwenye busu la nguvu.Ricardo akajikuta anashangazwa na jambo Fulani kwa muda hivi.


Don Marcos, baba wa Fanny, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Agatha, aliyekuwa muigizaji. Inaonesha kuwa hata, Saul alikuwa na uhusiano nae, pia alikuwa akijua uhusiano huo na Don Marcos,hivyo basi walikuwa na mpango wa kutumia kismati cha Don Marcos. Wakati Don Marcos na Agatha wakiwa pamoja, akaugua ugonjwa wa moyo.baada ya kutafuta msaada wa matibabu, Agatha anaondoka chumbani, Saul bila kujua akampigia simu. Don Marcos akaipokea simu hiyo na kusikia maongezi yake,anagundua mipango yao, ndipo alipogundua ni mpwa wa aina gani aliyenaye na kumbe muda mrefu alikuwa akitumiwa.Baadae katika akiwa katika kitanda ambacho alifia, Don Marcos anamwambia Fanny asimuamini Saul, kwamba ana tabia mbaya na kwamba anaishi kwa kufanya biashara zake.


Fanny, ambaye muda mwingi amekuwa akiishi kwa muenendo wake wa kunywa pombe na kutokana na wivu kupindukia,anajikuta ameweza kufanya biashara na kufanikiwa kuiendesha siku hadi siku, alikuwa akijiandaa kumfukuza Saul, pale alipomuita muongo,akajifanya kama vile alitaka kuacha kazi,anaamua kumuweka kama makamu wa raisi.


Familia ya akina Fanny iliyokuwa ikiendesha biashara inajikuta imeingia katika wakati mgumu huku wakiwa hawamuamini Saul). Ricardo anajipatia dili kupitia mwanasheria wake, ambaye ni mwanasheria wa familia ya Colmenares, kuendesha biashara ili kuirudisha sehemu yake.anamtambulisha Soraya kwenye familia, baada ya kumuona watu wote wanachanganywa na uzuri wake pamoja na uchangamfu anaouonesha kwao (hasa hasa Francisco),Ingawa hakuna mtu aliyemtambua kuwa ni Maki. Ricardo ameandika kitabu kinachoitwa, "Soraya", ambacho kina picha yake juu, na kuwapa kopi yake. Francisco ndiye atakayekuwa mpiga picha wa project yao akiwa na Soraya, ambaye hapotezi muda kupiga picha yake. Fransisco anatokea kuchanganywa na binti huyo kama alivyochanganywa kwa mara ya kwanza na Maki pale walipokutana huko Sauce.


Marina, ambaye anachanganywa na Saul ambaye hajawahi kumpeleka Lima kama alivyomuahidi, mwisho anaenda katika mji mkubwa. Soraya, anasikia kuwa Marina yuko pale kama anavyojua Francisco,ambaye alikwenda kukutana na Marina kujua kilichotokea huko Sauce kabla hajaondoka na kabla hajaoa kama kulikuwa na habari yoyote kuhusiana na Maki. Francisco anamuuliza kama bado uchunguzi unaendelea, Marina kwanini waeendelee kuchunguza wakati Maki ameishia. Francisco anaendelea kusumbuliwa na maneno ya Marina kumuita Maki changudoa, na kudai kuwa Maki alikuwa bikra wakati wanafanya mapenzi. Marina anasema kuwa wazo la kwamba yule alikuwa ni bikra halijui. Marina anamhakikishia kwamba Maki alikuwa ni muuza dawa za kulevya.Anamuuliza Francisco kama mtoto anajua kuwa Maki ndiye mama yake,naye akajibu kuwa Florcita anajua kuwa Fanny ndiye mama yake mzazi. Marina pia anaenda kwa Saul mwanaume anayemzuzua.


Dada wa Francisco, Angie bado anafanya dhambi na Ruffian, Juan Russian. Anaiba pesa kutoka kwa baba yake, Francisco naye anakwenda ufukweni kumrudisha nyumbani, Angie anasema kuwa amejiazima pesa,Juan Russian anaonekana na kumuoneshea bastola. Francisco anakazana kuitupa bunduki mbali, na kumlazimisha kuondoka, na kumpeleka Angie nyumbani kwake.baadae, Angie anadhani huenda ni mjamzito, kitu ambacho kitakuwa kibaya kwake,lakini kipimo cha mimba baadae kinaonesha hakuna ujauzito. Angie, anafanya kazi kwenye mgahawa wa baba yake (Leopoldo) na anakaa mbali na Juan Russian,akijiandaa kurudisha maisha yake. Leopoldo anampa kazi kijana mdogo aitwaye Alex kufanya kazi katika mgahawa na kufanya maigizo. Alex anajikuta katika wakati mgumu, na Leopoldo,ambaye ana moyo mkubwa, anampeleka ndani na kumpatia sehemu ya kuishi mpaka atakapokuwa sawa. Angie anaonekana kumpenda Alex. Kwa furaha zaidi mama wa, Fanny, Esther, anamuona kijana akiimba usiku mmoja kwenye baa,akamtupia macho ya kumpenda. Anamuuliza Alex kama atapenda kuimba katika matayarisho ya muziki.


Ricardo anakitu cha kumshangaza Fanny – amemuunganisha Soraya/Maki kwenye simu pamoja na padre, aliyesema anakuja Lima hivi karibuni, ambapo wataweza kukutana. Wote wana hamu ya kuongea pamoja. Hii yote ni mipango ya Ricardo kumfanya Soraya awe na furaha, ikiwa ni njia ya kuendesha maisha yake kwani mwisho wa siku anamuhitaji kwa matumizi yake mwenyewe. Lakini ushawishi wake unakuwa ni wa kishetani ili kukamilisha hazima yake.
Mwisho wa mwezi Oct. 3 katika tamthilia hii, Ricardo anafanya maonesho na Soraya ya kucheza na kuimba nyimbo za kiarabu. Wakati Soraya anatengeneza mwili wake kwa ajili ya kucheza, Juan Francisco akajikuta anambusu huku Fabiola akiangalia kitendo kilichomuumiza kutokana na wivu alionao, Saul anamfatilia Soraya, Fanny anamuangalia kwa woga (anashtushwa na muonekano wake lakini agundui kama Francisco anavutiwa na Soraya), Ricardo anafikiria mwenyewe kwamba amemuweka Soraya huru katika maisha yake na kujisemea kuwa " Atakuwa wa kwangu" , "na hatokuwa wa Francisco" Anajisemea..


Saul anapata wasiwasi bada ya kujua kuwa wawili hao wanakwenda Sauce, hivyo anamuweka Marina kuwafatilia nyendo zao, Fernando na Soraya na kuchukua picha kama ushahidi pale atakapowaona wakiwa katika hasara. Marina akawa hajisikii huru kufanya hivyo, bila ya kuwa na kaka yake Carlitos, ambaye kwa sasa ni mtafutaji huko jijini ‘Pescadores’ Sauce. Marina kamera yake inakuwa na matatizo anamwambia Saul angekuwa na kamera ya digital.
Fanny anakasirika pale anapogundua kuwa Ricardo hajaenda na wao huko Sauce, anawaacha Fernando na Soraya peke yao huko Sauce. Fanny mwisho anamtumia Saul kama wakala wake iwapo atagundua kitu ampe habari.


Ramon anamwambia Fernando awe mwangalifu kwa Soraya. Anasema kuwa alipokuwa na uhusiano na Maki, alikuwa hajaoa. Kwa sasa ameoa ana mtoto na mtoto mdogo.
Fernando na Soraya wanafika Sauce, na anaendelea kumwambia Soraya jinsi alivyo mrembo, na hiyo inafanana na alivyokwenda huko Sauce kwa mara ya kwanza alipokutana na Maki. Soraya anaendelea kuuliza maswali kuhusiana na uzoefu wake pale. Carlitos, Juan Jayo, na meneja wa hotel wote wanaonekana kuvutiwa na Soraya, inaonesha kama vile wanamfahamu. Juan Jayo anamwambia Fernando na Soraya jinsi alivyozisikia habari za kusikitisha za Maki na mtoto wake , Florcita, ambaye alichukuliwana Fernando.Akadai anakasirishwa na Fernando kwa tabia yake na kwamba atampa mimba Soraya na kuchukua mtoto wake.


Wakati huo huo, Esther bado anampa ukweli mpenzi wa Angie. Esther anamvuta na kwenda naye bichi kwenda kurekodi nyimbo nyimbo studio. Angie mwisho anaondoka akiwa na hasira baada ya kuona kinachoendelea kwa akina Esther, na kuwaza kuwa anaendelea kwa maana hiyo hakutakuwa na chumba kwa ajiri yake.


Hii ni Tamthilia tamu kabisa na hii nimewaletea kwa kifupi, iwapo nitapata zaidi nitawafahamisha zaidi msichoke kusoma kama una swali au ungependa kupata tafsiri ya

tamthilia Fulani ambayo uliipenda unakaribishwa…

Tunaomba maoni yenu kwa kupitia tamthilia hii..

No comments: