Wednesday, July 2, 2008

Mwanaume ni mtoto ndani ya nyumba:

HII NI MAKALA YA WAKUBWA TU.
Jambo hili ni kweli kabisa tena asilimia mia moja, mwanaume ni kama mtoto ndani ya nyumba anayebisha basi azidi kubisha lakini huo ndio ukweli wenyewe na wengi wetu tumekuwa tukilidharau sana jambo hili na tunapokuja kugutuka tunakuta tumechelewa kwelikweli. Kuna baadhi ya wenzangu nilibahatika kupata malalamiko machache lakini siyaiti machache kwa sababu yanatokea mara nyingi mno katika maisha yetu ya ndoa ama mapenzi kati ya wawili wapendanao.

Wapendwa tukubali tusikubali lazima tuewe kwamba mwanaume siku siku zote ndani ya nyumba ni kama mtoto mdogo, hivyo basi kama wewe umebahatika kuzaa mtoto mmoja mwingine wa pili katika familia yako ni mwandani wako.

Wengi wetu tumekuwa tukisahau kabisa kuwa mwanaume ni mtoto kwa kila kitu kama ilivyo kwa mtoto ili akue vizuri ni lazima apate mahitaji yote muhimu yanayastahili katika maisha yake ya kila siku. kama kufuliwa nguo, kupikiwa chakula, kubembembelezwa , kupelekwa hiospitali pale anapojisikia vibaya, mambo hayo na mengine mengi, wengi wetu tumekuwa tukijisahau kabisa mara tu baada ya kuolewa na kuzaa watoto.

Si jambo zuri hasa kujisahau ndio maana siku zote nasema ndoa ni ndoa kwa kiswahili fasaha au ni sisi wenyewe, ndoa ni matendo, ndoa ni tabia ni ukaribu unyenyekevu , uvumilivu na ikibidi upole kiasi, nimesema kiasi kwani ukizidi sana.

Wengi wetu wanaweza kusema nimehanganyikiwa kwa kuwapa kipaumbele wanaume ndivyo ilivyo jamani, mkubali msikubali ni lazima mshuke chini kidogo na si kujikweza.Basi wale wenzangu na mie ambao wanabisha wajaribu kufanya niliyoyasema na baada ya muda wataona mabadiliko katika uhusiano ana maisha yao ya ndoa.

Mara nyingi nimekuwa nikiongea sana kuhusu mapenzi kati ya wawili wapendanao na ili mapenzi kati ya wawili wapendanao yawe mema na ya kupendeza siku zote lazima tukubali kufanya mambo yote yanayoweza kumfanya mambo yote mwenza wako kwa namna moja ama nyingine aone kwamba kweli unampenda na kumjali na si vinginevyo.

Nimeamua kutumia msemo wa hapo juu ili kuwakumbusha wale wenzangu waliojisahau mara tu baada ya kuolewa na kuzaa, ndio unaweza ukawa uko karibu na mtoto wako kwa sababu wewe tayari umeshakuwa mama lakini pia unaye mtoto mwingine ambaye ni mume wa familia yako, ujisahau na kumwacha pembeni eti kwa sababu tu ameshakuwa mama fulani? Hapo jibu unalo mwenyewe kichwani mwako.

Naomba twende na wakati tusizubae ni wajibu wa kila mwanamke kumtendea mwenza wake yale yote yanayostahili, kumjali na hata kumpenda kwa dhati.

Kwa hayo machache mtakubaliana nami kuwa mwanaume ni mtoto katika nyumba kwani huhitaji malezi kama vile mtoto mchanga ili kudumisha mapenzi au kuimarisha ndoa yako. Nitapenda mutoe maoni yenu katika Makala hii.

No comments: