Monday, July 7, 2008

CATALINA Y SEBASTIAN:

NGUGU WASOMAJI TAMTHILIA HII NIKO KWENYE BLOG YETU.


Karibuni katika safu yenu ya thamthilia, ambayo hukuletea muendelezo wa tamthilia mbalimbali zinazooneshwa katika runinga kwa hapa jijini, bila shaka ndugu wasomaji mnaridhishwa na kile ninachowapatia kama kuna mapungufu naomba mnikosoe kwani mi ni mwanadamu.
Leo tunawaletea Tamthilia ambayo inaoneshwa na televishion ya Channel Ten inayojulikana kwa jina la Catalina y Sebastian.

Kawa kifupi ndani ya Tamthilia hii tunaoneshwa binti mmoja anaitwa Catalina mtoto wa kwanza wa Adela na Gustavo, yeye anakuwa na mapenzi makubwa na kijana Eduardo. Hata hivyo mambo yanabadirika baada ya familia ya Catalina kutamani sana utajiri.

Adela mama wa Catalina,mwanamke ambaye anajivunia uchawi wake na mwenye maisha magumu katika familia anayoilea anamlazimisha mtoto wake Catalina kuolewa na mwanaume tajiri.

Gustavo – baba wa Catalina.anakuwa bwege anayeongozwa na mwanamke hii yote ni kutokana na ufukara alionao kiasi kwamba inafikia ata wakati gari lao linataka kuwekwa benchi bila ya msaada wowote.Tumaini lao linakuwa ni kwa mtoto wao Catalina ambaye wanatarajia kuwa ataolewa na tajiri.
Kwa upande wa washiriki wengine tutakutana na na Ricardo kaka wa Catalina ambaye hapendi kufanya kazi, yeye anapenda pesa tu.
Don Lupe yeye ni baba wa Sebastian bwana shamba na mfugaji anayependa maendeleo kutokana na kazi zake amekuwa mkakamavu asiyekubari kushindwa kitu.

Sebastian – mhusika mkuu mtoto wa Don Lupe aliyetoka masomoni nje ya nchi hivi karibuni.
Martina dada wa Sebastian, rafiki mkubwa wa , Emilia ambaye anataka kuwa karibu na Sebastianand ! ambaye anapoteza muda wake kuonesha kuwa anamuhitaji!.

Washiriki wengine ni Antonieta, yeye anamchukia Don Lupe, inaonesha kuwa anajua siri Fulani juu yake,anahisi huenda Sebastian si mtoto wa Lupe.

Eduardo – mpenzi wa Catalina! Yeye amecheza sehemu ambayo anamsaliti mpenzi wake kwasababu ya pesa pale anapolipata jimama lenye pesa anaamua kumbwaga mpenzi huyo.
Catalina anafanikiwa kukutana na Sebastian, Sebastian moja kwa moja anampenda Catalina na kumwambia baba yake afatilie binti huyo anatoka katika familia gani, Catalina yeye haimuingii akilini anaamua kutafuta kila njia ili kutoroka na kijana anayempenda naye ni Edwardo.

Catalina anakwenda kumuona Eduardo nyumbani kwake , Sylvia(jimama linalomsumbua Edwardo kutokana na pesa zake linakuwa huko), Edwardo kwa sasa anatakiwa kuamua moja kuwa ni Slyvia au Catalina , naye Sebastian, anamwambia baba yake kuwa atamuoa mwanamke mmoja tu naye ni Catalina, Catalina hampendi Sebastiani yeye ni Edwardo tu naye amepaona penye pesa je itakuwaje usikose kufatilia.
Chumbani kwa Catalina.

Catalina anaongea na dada yake kuhusiana na harusi yake na Eduardo hapo baadae.Anajua kwamba hatokuwa na gauni nyeupe kwa mara ya kwanza lakini baadae, kabla hawajaoana kwa sheria wazazi wake wanamkubari Eduardo kama mme wake, lakini anataka kuwa na harusi ya kanisani. Catalina anadhani kwamba Sebastian atakuwa amepata mwanamke mwenye tabia nzuri wa kuishi naye.

At the rancho
Carmelo anaongea na Miguel. Wanaongelea tabia zake mbaya. Ramiro anafika.wanaongea kuhusiana na Antonieta na jinsi alivyopata faida kupitia kwake. Hakuna njia, Josefa ni kama yeye.

Nyumbani kwa Antonieta.
Antonieta anaongea na Josefa kuhusiana na penzi la Sebastian na Emilia.Josefa anamuuliza Antonieta anawezaje kuongelea mapenzi kama hakuwahi kumpenda mtu yeyote. Antonieta anamwambia Josefa kwamba aliwahi kumpenda don Lupe na kwamba baadae alikuja akawa mchungu mwenye chuki kwasababu hakumpenda.
Nyumbani kwa Lupe.

Ramiro anafika akimuulizia Martina na don Lupe anamwambia kwamba yuko pamoja na Emilia. Nje, Martina anamuuliza Emilia nini alifanya kwa Sebastian kinachosababisha asitake kumuuona shamba.

Carmelo anaongea na Antonieta ambaye anamwambia kuwa ni vizuri angejijua kuwa ni mwanaharamu kuliko hilo jina lake.

Martina na Emilia wanaongea na maongezi yao yanavunjwa na don Lupe ambaye anafika na kutaka kujua walikuwa wakiongelea nini. Martina na Emilia wanaendelea kuongea ambapo Rufino na don Lupe wanaongea kuhusiana na wasichana. Rufino hataki Emilia ampoteze Martina.
Emilia anamwambia Martina kwamba, usiku uliopita, alilala katika kitanda cha Sebastian.
Nyumbani kwa Catalina

Sebastian anafika na kuwadha ni kwanini familia yao inaishi kama vile matajiri wakati ni maskini? Adela anajaribu kumuelezea Sebastian lakini Sebastian anamwambia kuwa hakuna aibu yoyote ya wao kuwa maskini. Adela kwa ukali anauliza umaskini? Nakumalizia kuwa kwa njia yoyote ile hawawezi kuwa maskini, na kudai kuwa wanayo pesa japo haipatikani wakati wowote." Sebastian anawaambia kuwa hakuwa na maana ya kuwapa pesa anataka Catalina ampende kama alivyo si kwa pesa yake na umiriki wa ardhi.Catalina kisha anauliza umesiki hivyo?

Catalina anaomba msamaha kwa Sebastian kwa kuwa na wasiwasi kisha wanaamua kusherehekea na kula chakula cha mchana nje. Catalina anataka familia yake waende pamoja.
Huko shamba

Emilia anafika pamoja na Martina.wote kwa pamoja wanaongea ujio wa baile na Emilia anasema anaenda kuhudhuria muziki pamoja na Sebastian. Ramiro anamwambia asihesabie kwasababu Sebastian anaweza kutokea kwenye muziki pamoja na mpenzi wake mpya kwasababu anampenda sana.
Nyumbani kwa Catalina

Familia ya Hernandez pamoja na Sebastian wanamsubiri Gustavo. Gustavo anafika akiwa na hasira. Anamshika shati Sebastian na kutaka maelezo juu ya mpenzi wa Sebastian aliyeko huko shamba. Sebastian anasema kwamba ana kitu cha kuficha ni kwamba hana mpenzi na kwamba anampenda Catalina na anataka awe mchumba wake. Anamuomba Gustavo kumuelezea anayetakiwa kuwa mpenzi wake.

Huko shamba
Carmelo anaongea na Petra na anataka kujua kama Antonieta anajua kitu chochote kuhusiana na baba yake. Petra anamuonya" ni bora ukaacha kulima kwasababu utajisikia vibaya kama utaongea naye.

Nyumbani kwa Hernandez
Sebastian, anamshukuru Gustavo kwa kumjua Emilia na kuiambia familia kwamba ni jirani yake ambaye anapoteza muda mwingi kujipendekeza lakini hana mpango naye. Adela na Ricardo wanaruka kukubariana na maelezo ya Sebastian. Sebastian ana hasira na anataka kwenda shamba kupata ufafanuzi kutoka kwa Emilia na kuwaomba waarishe chakula chao cha mchana kwa muda mzuri zaidi. Sebastian anaondoka na familia yake yote inavunjika moyo na kubaki wakijiuliza watakula nini?
Nyumbani kwa Alicia

Luis anafika na kuongea na Alicia kuhusiana na matatizo ya Catalina na Eduardo. Alicia anamwambia kwamba ana furaha kwani mwisho wamekuwa pamoja, Luis anamwambia kwamba sio rahisi kiasi hicho: Eduardo ana mwanamke mwingine, anataka kumuoa na kwamba, Alicia, anatakiwa kumwambia Catalina ukweli na kumshawishi aache kumuangaikia Eduardo.
Nyumbani kwa Hernandez

Adela na Ricardo wanajiandaa jinsi ya kumshawishi Catalina amuache Eduardo na kuolewa na Sebastian.wakadai kuwa hakuna kingine zaidi ya kumtafuta mwanamke mwingine na kumbambikia .
Nyumbani kwa Alicia.

Luis anamwambia Alicia jina la mwanamke ambaye Edwado anataka kumuoa ni Silvia na kwamba mara nyingi huwa wako pamoja. Anadai kuwa Edward ni mtu mbaya anataka pesa za Silvia. Alicia anahisi kwamba Catalina atakufa pale atakapogundua ukweli. Jikoni kwa Hernandez

Luisa anarudi kutoka sokoni akiwa na chakula,Catalina anawadha jinsi mama yake alivyopata pesa kwa asjili hiyo? Luisa anamwambia kwamba ni mwanamke,ambaye amepangisha nyumba na kulipa kodi yake. Ni aibu kwamba sirvienta anaweza kulipa kodi yake kwa muda maalumu na wao hawawezi kulipa kwa muda.

Huko shamba,
Sebastian anafika na kumuuliza don Lupe kama Emilia yuko nyumbani. Don Lupe anamwambia yuko chumbani kwa Martina.Don Lupe anataka kujua kitu gani kikubwa kilichotokea Sebastian akamwambia kuwa atamuelezea baadae.

nyumbani kwa Alicia
Luis anamuomba Alicia amwambie Catalina kuhusiana na Silvia na Eduardo na amsaidie kwasababu hii itamvunja moyo. Alicia anasema kuwa hajui itakuwaje kwani Catalina anampenda sana Eduardo.

Huko shamba
Sebastian anaingia ndani ya chumba cha Martina na kumuuliza Emilia kwanini aemwambia kuwa baba yake Catalina kuwa yeye ni mpenzi wake. Emilia anamwambia kuwa hajafanya chochote kwani hamjui baba wa Catalina labda amtafute. Sebastian akuamini jinsi Emilia alivyoruka.

Sebastian anaongea na Ramiro. Wanawadha ni mwanamke wa aina gani anayeweza ku ongea na baba wa Catalina, Sebastian anasema kuwa lazima atakuwa ni Emilia, kwani anaweza kufanya kitu kama hicho tokea alipombusu kwa mara ya kwanza alipomuona na kurukia kwenye kitanda chake .kwa upande mwingine, Sebastian anamwambia Ramiro kwamba kitendo hicho kimemuuma kwani Catalina aliposikia hivyo hakupatwa na wivu hata hivyo anaamua kumuoa japo anajua kuwa yuko na Edward.
Huko mazoezini.

Silvia anamwambia Eduardo kwamba,kama zawadi ya harusi anatarajia kumpatia zawadi ya gym yake .Akapata furaha na kuwaza iwapo atakuwa na Catalina."
Katika chumba cha Catalina.

Catalina anaongea na Luisa na kumuuliza iwapo atamuona Eduardo na mwanamke mwingine atavunjika moyo?

Chumbani kwa, Adela na Gustavo wanamuongelea Emilia pale Alicia alipogonga mlango akitaka kuongea na Catalina, Adela akamuonesha ni jinsi gani asivyompenda.

Alicia anamuomba Catalina kuongea naye faragha. Kuhusiana na Eduardo. Catalina anataka kujua ni kwanini ? kwasababu sitaki familia yako ikuone wewe ukiumia. Kwanini? Kwasababu Eduardo ana mwanamke mwingine.
Huko shamba

Rufina anajiandaa kutoa chakula kwa don Lupe pale Carmelo kwamba Antonieta alikuwa akimtafuta ili amsaidie kitu. "je Lupe ataongea na Antonieta, je anaweza kumuuliza mwanamke kuhusiana na baba wa Carmelo?" Don Lupe anamwambia Carmelo aondoke. "hata hivyo namchukulia kama kijana wangu, hilo alimtoshi?"
Nyumbani kwa Antonieta.

Josefa na Antonieta wanamuongelea Carmelo Antonieta anasema kama Carmelo ataendelea kumsumbua atawaambia watu wote mjini pale kuhusiana na uhana haramu wake.
Huko shamba:

Sebastian na don Lupe wanajiuliza ni nani aliyeongea na baba wa Catalina. Don Lupe anamwambia Sebastian kwamba hataki Sebastian aumie kwa ajili ya mwanamke na kwamba anadhani huenda Catalina akawa anampendea pesa zake.
Nyumbani kwa Catalina
Hataki kuamini kama Eduardo ana mwanamke mwingine. Ana uhakika kwamba huo ni mchezo mchafu wa wazazi wake ili kumsambaratisha na Eduardo. Alicia anasisitiza kwamba Eduardo atamuoa mwanamke huyo kwani ni tajiri na ukweli ni kwamba Luis amemwambia.

Catalina anamwambia Alicia aache kudanganya na kwamba anatakiwa kwenda kwenye mambo yake muhimu nyumbani kwa Eduardo.Anaenda kumwambia kuwa ameondok anyumbani kwa wazazi wake, na kwamba hana pa kwenda na kwamba ana uhakika kwamba Eduardo atakuwa na furaha kuwa naye nyumbani kwake na atamuoa. Kish aakamwambia Alicia kwamba ataona.
Nyumbani kwa Eduardo.

Eduardo na Silvia wanarudi nyumbani . wanapata chakula cha mchana na wako tayari kwenda kitandani. Eduardo anafikilia jambo jema ni kumwambia meneja wa majengo kwamba yeye hayuko pale iwapo Catalina ataenda kumuona.
Huko shamba

Don Lupe anamwambia Sebastian kwamba atamuajiri mpelelezi ambaye atamchunguza Catalina na familia yake ndipo Sebastian atamuoa " utafanyaje hivyo kwangu? Sebastian anauliza na kisha anadai kuwa baba yake anadhani yeye ni mpumbavu kiasi gani kwa mwanamke? Don Lupe anamwambia kwamba anataka kujua kama mwanaye yuko salama. "kwa vyovyote mimi si mtoto wako!"

Huko cantini
Carmelo, Ramiro na marafiki zake wawili wanakunywa. Carmelo anakunywa na kulewa. Ramiro anataka kuondoka lakini Carmelo anataka kila mmoja kujua siri yake. Ramiro anakubari kunywa. Carmelo anasema kuwa anajua yeye ni mtoto halamu wa Don Lupe na kwamba kwa sasa amehakikisha hilo.

Katika jengo la Eduardo
Catalina anafika meneja anamwambia kuwa Edwador hayuko ndani anajitolea kumfungulia huko ndani Catalina anaingia na kwenda chumbani ambapo anamkuta Edwador akimbusu Silvia kisha wanafungua kinywaji.

Tunaoneshwa Catalina akisema kuwa anamchukia Eduardo na kisha anafikilia kuolewa na mwanaume tajiri.
Catalina anagundua Eduardo na Sylvia "wanafurahia" harusi yao wanayoitarajia hivi karibuni kwenye chumba chao. Anaamua kutoka nje akiwa amefatana na Edward ambaye anamwambia aachane naye. Catalina anakasirika baada ya kugundua kuwa Eduardo ameamua kumsaliti kwasababu ya pesa ili kumaliza shida za familia yake. Eduardo anamuuliza Catalina kama amemaliza maongezi yake? Akaanza kumuuliza Edward kwa machozi ya maumivu na mwenye kuhisi kuwa anaonewa baada ya yote aliyomfanyia. Kwa hasira Eduardo anamwambia kuwa hawezi kuishi kwasababu ya mapenzi tu. Sylvia anaweza kumpatia chochote ambacho siku zote anakiitaji, kwa hasira Catalina anamwambia kuwa anamchukia, kisha anampiga kofi kisha akakimbia mbali na nyum ba hiyo.

Akiwa anaondoka zake nje ya nyumba ya Edward akasimama kwa muda na kujiapiza kuwa hatokaa akamuacha mtu akamuumiza tena kama alivyofanya Edwardardo.

Aliporudi nyumbani kwake Eduardo akamuhakikishia Sylvia kwamba amemalizana na Catalina. Akamuita muongo na kumwambia kwamba hatotaka kumuona tena. Kisha akampa kibao cha nguvu shavuni kabla hajatoka. Eduardo akabaki peke yake kwenye chumba chake.
Nyumbani kwa Catalina chumbani.

Adela anaingia ndani na kumkuta Luisa akiangalia TV. Adela anaamua kuizima TV na kumuuliza ni kwanini Alicia alikuja kumuona Catalina. Cha kushangaza Luisa akamwambia mama yake hafahamu ni kitu gani Alicia na Catalina walikuwa wakikiongelea. Adela anapata hasira kwasababu anaimani kuwa Alicia anaendeleza uhusiano wa Catalina na Eduardo. Kisha akamwambia mtoto wake kuwa ana uhakika kwamba Catalina hivi karibuni atakuwa mbali na Alicia.

Sebureni kwa kina Cata:
Adela anajaribu kumshawishi Gustavo kuvunja uhusiano wa Catalina na rafiki yake Alicia. Gustavo anaamua kumuacha aendelee kukasirika. Adela hawezi kuelewa Catalina ameona nini kwa mwanaume maskini kama Eduardo, wakati Sebastian ni mwaname mtanashati!

Jikoni kwa RANCHO

Rufino na Pachito wako jikoni Sebastian akiwa amekasirika anaingia ndani na kupata glasi ya juice. Anamwambia Rufina kwamba baba yake ameweka mpelelezi wa kufatilia mienendo ya Catalina. Rufina anamwambia kuwa Lupe anajaribu kumtafutia kitu anachokiona ni bora kwake. Sebastian anasisitiza kuwa pamoja na yote yeye ataendelea na msimamo wake kuwa anampenda Catalina na atakuwa naye. Anaamua kuondoka na kwenda cantini.
Kwenye mitaa ya jiji:

Catalina anatembea karibu na jiji akiwaza mambo yote na mipango waliyopanga na Edwardo na jinsi mambo yalivyokuwa mabaya.
Huko Cantini.

Carmelo amekunywa pombe nyingi kisha ameweka kichwa chake katika meza, anaongea na Ramiro kuhusiana na wazazi wake. Ramiro haamini kama ni mtoto wa Lupe. Sergio anaingia ndani Cantini Ramiro anamuuliza kama anaweza akapatikana mtu akampeleka Carmelo nyumbani. Sebastian anawaelekeza wanaume wawili wampeleke Carmelo, ambaye alikuwa amekunywa sana na kushindwa kutembea kwa miguu yake. Marcario anawasindikiza Sebastian anakaa na Ramiro.

Ramiro anataka kujua ni kwanini Sebastian ana hasira. Sebastian anamwambia amegundua kuwa baba yake alimsariti.

Sebureni kwa El RANCHO
Martina anamuuliza Lupe ni kitu gani kilimsababisha Rufina akapiga kelele. Lupe anamwambia binti yake amegombana na Sebastian.
Sebureni kwa ANTONIETTA.

Josefa anamuadithia Antonietta ugomvi wa Sebastian na Lupe kuhusiana na Catalina. Antonietta ana furaha kwamba baba na mtoto wako ndani ya ugomvi. Antonietta anadai kwua atalipiza, kama Catalina ataweza kurekebisha uhusiano kati ya Lupe na Sebastian. Ana mpango wa kumpatia Lupe husia wake."
Sebureni kwa El RANCHO

Lupe anamwambia Martina kwamba ameweka walinzi kuifatilia familia ya akina Catalina. Martina akamwambia kwamba amefanya vibaya na kwamba anadhani itakuwa ni mbaya kwa Catalina. Lupe anabaki na msimamo wake na kudai kuwa amefanya hivyo ili kuhakikisha kuwa Sebastian anapendwa kweli si kwasababu ya pesa.
Akamwambia Martina aongee na Sebastian kisha amueleweshe nia yake.
Itaendelea...

No comments: