Saturday, June 28, 2008

MADA

Mshindo wa Mwanamke ni nini?

Hivi kuna mshindo wa mwanamke? Huwa ukoje? Ni maswali magumu kwa mtazamo wa watu wengi, lakini maswali haya yana maana kubwa katika ulimwengu wa mapenzi.

Mwandaaji wa kitabu hiki ni mmoja wa watu wanaona maana ya maswali hayo, kwa kuwa tunazungumzia maswala ya maana au kwa lugha ya siku hizi ‘mambo ya pwani’ sina haya na nyie wapenzi wasomaji, nitawaeleza kiunagaubaga huo mshindo wa mwanamke unakuwaje?
Kwa maana tu, mshindo wa mwanamke ni kule kutoka kwa uteute ukeni au kama majimaji yanayonata kiasi, majimaji hayo hutokana na msisimko anaoupata mwanamke katika sakata zima la tendo la ndoa..

Wengine wanadai kuwa majimaji haya hutoka kwa msukumo Fulani wa haraka lakini wengine wanatanabaisha kuwa tendo hilo lazima liambatane au lihusike na kilele cha mwanamke, kwa maana ya kwamba majimaji hayo huashiria mwanamke amefika kileleni.

Kwa upande wangu ndugu zangu maana zote zinaweza kuwa sawa,lakini ukweli ni kwamba ni ngumu sana kwa mwanamke kufika kileleni.Sasa twendeni darasani kidogo, watalaam wa mambo ya mahaba wamefanya uchunguzi ili kupata uwiano wa mshindo wa mwanamke dhidi ya mwanaume.Hakika uchunguzi huu ulikuwa mgumu mno na kadri ilivyokuwa ngumu kufanya kazi hiyo, ndivyo ilivyokuwa taabu kupata idadi ya wanawake waliowahi kupata hisia za kufika kileleni.Hitimisho likawa kwamba, mshindo wa mwanaume ni rahisi zaidi kufikiwa ikilinganishwa na mwanamke.

Lakini pamoja na hayo, hakuna tatizo lolote la kiafya au maumbile kwa wanawake wanaofika kileleni na wale wasiofika kileleni, hivyo mashoga zangu msiojua hata raha ya kuwa huko ‘kileleni” msiwe wapweke kwa kuhisi mna matatizo ya kiafya, la hasha mu wazima tatizo ni kwamba mshindo wa mwanamke uko mbali shoga zangu!

Wasomaji wangu fuatilieni uhundo huu.

No comments: