Thursday, July 10, 2008

Njemba ajifungua bila operesheni

Yule mwanaume raia wa Marekani aliyeushangaza ulimwengu kwa kushika ujauzito, Thomas Beatie (34), hatimaye amejifungua kwa njia ya kawaida na si kwa operesheni kama baadhi ya watu walivyotarajia.

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa, Thomas alijifungua kama wanawake wengine wanavyojifungua kufuatia kushindwa kuibadili sehemu yake ya uke baada ya kujibadili jinsia.
Thomas alijifungua Jumapili iliyopita katika Hospitali ya St. Charles iliyopo mjini Bend, jimbo la Oregon nchini humo huku taarifa zikidai kuwa, mtoto wake huyo anaendelea vizuri. Wachunguzi wa mambo wanaeleza kuwa, mke wa mwanaume huyo aitwaye Nancy ndiye amekuwa mstari wa mbele kumsaidia mumewe huku baadhi wakidai kuwa, huduma anazompatia ni pamoja na kumkanda kwa maji ya moto.


“Mkewe anaonesha kufurahi, labda kwasababu mwenyewe sasa hivi hana uwezo wa kuzaa ndio maana, anampa huduma zote anazostahili kama mjamzito,” liliandika gazeti moja la nchini humo. Naye Thomas ameripotiwa kumfanyia mwanae ‘shopping’ ya nguvu ikiwa ni pamoja na kumnunulia vigauni (kama anavyoonesha ukurasa wa mbele) na midoli ya kuchezea.

Awali, Thomas alikuwa na jinsia ya kike akiitwa Tracy Lagondin lakini alipofikisha umri wa miaka 20 alijibadilisha na kuwa mwanaume kisha kumuoa Nancy huku akiacha viungo vyake vya uzazi kama vilivyo.

Hata hivyo, baadaye alipandikizwa mbegu za kiume kitaalamu na kufanikiwa kupata ujauzito kisha kujifungua mtoto huyo.

No comments: