Monday, July 14, 2008
LIKIZO YA J.LOPEZ NCHINI ITALIA
Jennifer Lopez na Marc Anthony hivi karibuni walikuwa wakipunga upepo katika Mji wa Portofolio, Nchini Italia wakifurahia likizo yao, waliyopewa kampani kubwa ya wanamitindo wawili wa huko Italia inayomilikiwa na Stefano Gabbana na Domenico Dolce.
Hawakuwaacha mbali watoto wao mapacha, Max na Emme ambao walizaliwa Mwezi Februari, mwaka huu. "Ni mama mzuri kiasi cha kushangaza, nina jisikia sifa kuwa naye," alisikika akisema Anthony hivi karibuni katika The Billy Bush Show. "Ni wa thamani sana hata kumwangalia tu,” aliongeza.
Mc Anthony alisema kuwa wanawakuza mapacha wao bila nyanya, hivyo wanapeana zamu kwa masaa katika kuwalea. Anthony ana ‘shift’ ya kuanzia saa 4 usiku mpaka 2 asubuhi.
"Tumeshazoea na tunapata wasaa mzuri,” alisema baba mzazi huyo. "Ananitegemea nimsaidie na kwa hilo hapati taabu.” Katika mwezi wa Mei, J. Lo aliliambia jarida la Us magazine.com kuwa mapacha wao wako ‘bomba’.
Lakini alisema kuwa hakuwa na uhakika kama anaweza kuwa mama mzuri. "Kwa kweli sijui hilo, kwa sababu maisha yangu yalipangwa toka siku nyingi zilizopita (miaka),” alisema J. Lopez. Tayari J. Lo ameshatia saini mkataba wa kucheza ‘movi’ ya Love and Other Possible Pursuits ambayo itaanza kuchukuliwa hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment