Thursday, July 10, 2008

HII NI MAKALA YA WAKUBWA TU.

MNAFAHAMU KUWA ASILIMIA 75% KATIKA MAPENZI NI ROMANCE?

Kwa watu wanaopendana hawahitaji kutumia nguvu kwani siku zote tendo hili hufanywa kwa hiari baina ya mke na mume, kuchunguzana ni wapi mwenzi wako ukimshika ama kumtomasa unaweza ukaamsha ashiki za mapenzi. Niwaeleze kitu kimoja ambacho wengi wetu mtakuwa hamkifahamu mwanaume anaweza akaridhika mara moja pale anapotokea kushinda goli lakini mwanaume ana uwezo wa kuendelea hata zaidi ya mara nne inategemea wewe mwanamke unamfanyia vipi mwenzi wako.


Ni kweli wengi wetu hatufahamu kabisa kuwa mapenzi hupendeza pale mnapochunguzana na kuelewa kwa ufahamu iwe kwa mume au mke, mume mfanyie mke wako kitu anachokipenda wakati wa tendo la ndoa, vile vile mke huna budi kutenda kile anachokitaka mumeo kwani ubunifu huchangia kudumisha penzi, kuna baadhi ya vitu ambavyo ni vigumu kuvifanya lakini unapogundua kwamba mwenzangu anapendelea kitu hicho basi uvumilivu huhitajika zaidi.

Najua mtakuwa mkijiuliza ni kwanini uvumilie na kufanya kitu ambacho wewe binafsi usingependa kukitenda, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba mapenzi ni staili, uvumilivu, ubunifu kiasi sio kujibweteka na kujisahau siku zote wewe uwe fundi kwa kila kitu kuanzia kitandani hadi idara nyingine usikubali jitahidi kwa kila hali.

Ushauri ninaowapa ni huu muwe tayari mmejiandaa kufanya tendo la ndoa, sio tu kwa sababu Fulani anataka hata, mke, mume mjiandae kwa tendo hili mfurahishana mnapokuwa faragha wawili, mnapokuwa katika hali hiyo siyo sehemu ya kukumbushana makosa, machungu, ama karaha zilizotokea nyuma, weak akili yako katika tendo hilo, fikiria kwamba uko na mtu umpendaye, kwani wakati huo ni mzuri wa kufaidi tendo la ndoa.

Tumekuwa na mazoea unapokuwa na mwandani wako wakati wa makasheshe basi wewe unaona kwamba hapo ndio muda mzuri wa kuanza kumlalamikia, hapana tunakosea, mapenzi yanahitaji fikira za kitu mnachokitenda. Unaweza ukamuuliza maneno mengine ya kumtia mtu ashiki, kwa mfano unaweza ukamwita kwa maneno matamu, “Darling nakupenda “ “Umekuwa ukinifurahisha mno tunapokuwa kitandani” “Fulani unanipendea nini” “Nikufanyie nini mpenzi wangu ili ufurahi” maneno hayo na mengine yanazidi kulipamba penzi lenu na wote wawili kufurahia.
Fuatilia Makala hii ili upate mambo ambayo huyajuii....

No comments: